Habari kuhusu Uingereza
Wiki ya Wanablogu wa ki-Caribiani 2016 Yalenga Kukuza Sauti za Eneo Hilo Mtandaoni
Wanablogu wa Caribiani wapo, na wana sauti zinazostahili kutambuliwa.
Kutana na Joshua Beckford Aliyehudhuria Chuo Kikuu cha Oxford Akiwa na Umri wa Miaka 6
Blogu ya Omg Ghana iliripoti kuhusu mafanikio bora ya kielimu ya Joshua Beckford: Katika umri wa miaka 8, wewe pengine ulikuwa unafanya mazoezi ya michezo au ulikuwa ukifanya maandalizi ya kujiunga...
Filamu 14 za Mazingira zenye Kuvutia
TVE (Televisheni inayohusika na Mazingira) yaonesha video 14 bora za washindani waliofika fainali kwenye shindano la kimataifa la filamu bora ya mazingira. Washiriki kutoka sehemu mbalimbali za dunia wametengeneza filamu...
Gambia Yajitoa Jumuiya ya Madola, Yaiita Jumuiya Hiyo ‘Ukoloni Mambo-Leo’
"Gambia haitakuwa mwanachama wa taasisi yoyote ya ukoloni mambo-leo," nchi hiyo ya Afrika Magharibi ilitangaza katika tamko lake la wiki hii.
Kadri Liberia inavyotulia, vijana waanza kuzungumzia ngono
Kadri Liberia inavyoendelea kutoka kwenye vita ya kutisha ya wenyewe kwa wenyewe, wengi wanahofu mchanganyiko wa umaskini uliokithiri na maamuzi yenye hatari ya ngono vitaongeza kiwango cha VVU/UKIMWI na idadi ya mimba zisizotarajiwa.
Dunia Nzima: Lugha 2,500 Zinapotea
Ramani shirikishi ya lugha zinazopotea, inayoonyesha lugha 2,500 kati ya 6,000 ambazo ziko hatarini, imezinduliwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO). Shirika hilo la kimataifa linawaomba watumiaji wachangie kwa kutuma maoni kwenye mradi huo ambao unawatia mashaka wanablogu wengi wenye nia ya kuhifadhi tamaduni.
India: Filamu ya Slumdog Millionaire Yanyakua Tuzo za Oscar
Filamu ya Danny Boyle, Slumdog Millionaire, iliyotokana na kitabu chenye maudhui ya India imefanya vyema katika sherehe za 81 za tuzo ya Academy. Wahusika wake kutoka Uingereza na India walitia...
Bahrain: Raha na Karaha za Kusoma Ng'ambo
Ingawa Bahrain ina idadi kadhaa ya vyuo vikuu, vya umma na binafsi, raia wengi wa nchi hiyo hupata fursa ya kwenda ng'ambo kwa masomo ya shahada ya kwanza na hata zile za juu, mara nyingi kwa kutegemea ufadhili. Moja ya matatizo ya kwanza wanayokumbana nayo huko ughaibuni ni kwamba watu wachache tu hufahamu ni wapi Bahrain ilipo. Katika makala hii tunafuatilia uzoefu wa wanablogu watatu ambao ndiyo kwanza wamekwenda ng'ambo kwa masomo: kule Japan, Uingereza na Marekani na mwanablogu wa nne ambaye anasoma India kwa kipindi fulani hivi sasa.
Macho ya Kimataifa kwenye Uchaguzi wa Marekani
Kadiri uchaguzi wa Marekani unavyokaribia, ndivyo kadiri macho ya kimataifa yanavyozidi kuelekezwa katika sera za nje za taifa hilo na wagombea wake wakuu. Kazimiradi kama vile ile ya Collective Journalism inayofanywa na Current TV (Uandishi wa Habari wa Umma wa Current TV) na Global Voices' Voices Without Votes (Mradi wa Global Voices - Sauti Zisizo na Kura) zimechukua jukumu la kukusanya taarifa na kuzipa mtazamo wa kimataifa katika masuala ya ndani ya sehemu fulani tu ulimwenguni.