Dunia Nzima: Lugha 2,500 Zinapotea

Ramani shirikishi ya lugha zinazopotea, inayoonyesha lugha 2,500 kati ya 6,000 ambazo ziko hatarini, imezinduliwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO). Shirika hilo la kimataifa linawaomba watumiaji wachangie kwa kutuma maoni kwenye mradi huo ambao unawatia mashaka wanablogu wengi wenye nia ya kuhifadhi tamaduni.

Mkutubu, Iglesia Descalza anablogu:

Nikiwa mmojawapo wa watu wanaopenda lugha, ninasikitishwa ninaposoma habari zinazotoka wakati wa kutolewa kwa Kitabu kipya cha ramani ya lugha zilizo Hatarini kutoweka Duniani cha UNESCO. Kwa mujibu wa kitabu hicho cha ramani, kilichozinduliwa kwenye mkesha wa Siku ya Kimataifa ya Lugha (21 Februari), karibu ya lugha 200 zina wazungumzaji pungufu ya 10 na lugha nyingine 178 zina wazungumzaji kati ya 10 na 50.

Takwimu zinaonyesha kuwa kati ya lugha 6,000 zilizopo sasa, zaidi ya 200 zimetoweka katika vizazi vitatu vilivyopita, 38 ziko hatarini kabisa, 502 ziko hatarini sana, 632 ziko hatarini bila ya shaka na 607 haziko salama.

Wazungumzaji wa mwisho wa lugha wanapofariki, na lugha pia hufariki. Lugha ya Ki-Manx katika kisiwa cha Man ilitoweka mwaka 1974 wakati Ned Maddrell, mzungumzaji pekee wa lugha hiyo alipofariki wakati lugha ya Ki-eyak huko Alaska Marekani, ilikumbana na maangamizi mwaka jana kilipotokea kifo cha Marie Smith Jones.
[…]
Inatubidi tuuenzi uwingi wa kibaiolojia, uwingi wa tamaduni na rangi za watu, pamoja na uwingi wa lugha kwa sababu tunapoteza mambo mengi mno kadiri tunavyozidi kumezwa na jamii moja kubwa nyeupe, inayoongea Kiingereza.

Huku lugha zinazopotea nyingi zake ni zile za watu watu wa makabila wanaokumbwa na utandawazi na utaifa wa dola, Daniel Moving Out, blogu ya mwanablogu wa kireno anayeishi uingereza kwa sasa, inasema siyo lugha zote “zisizo rasmi” ambazo zinakufa.

[…]

Lugha ya Ki-Galisia inasikika kama vile ni mchanganyiko wa Kihispania na Kireno, kana kwamba ni lugha iliyotokana na Kireno na kuboreshwa na misamiati na lafudhi za Kihispania. Lugha hiyo asili yake ni Ki-Galisia na Kireno cha zama za kale, na ilikuwa ikizungumzwa katika jimbo lote la Portucale […]

Wiki hii, kitabu cha ramani za lugha cha UNESCO kilitolewa, na kudai kwamba Ki-Galisia ni moja ya lugha zenye nguvu ambazo si lugha kuu katika nchi yoyote. Inalindwa na Ki-Kastilia (Kihispania cha kawaida) kutokana na kuwa karibu na Ureno kijiografia.

[…]

Blogu hiyo inaandika muhtasari wa takwimu mbaya zaidi:

[…]

Lugha 199 zina wazungumzaji wa asili pungufu ya kumi na wawili. Katika Indonesia, wazungumzaji 4 waliobakia wa Ki-lengilu wanaongea miongoni mwao [peke yao]; Ki-Karaim nchini Ukraine kinatunzwa na watu 6 tu. Zaidi ya lugha 200 nyingine zimetoweka katika vizazi 3 vilivyopita. Ki-Manx, kutoka Kisiwa cha Man, hapa uingereza kilitokomea na mzungumzaji wake pekee mwaka 1974.

Lakini si kila mmoja anayejali kupotea kwa lugha. Akitoa maoni kwenye blogu ya TED blog, Magnus Lindkvist anasema:

[…] kwa nini tunaendelea kuzikumbatia lugha za kale ambazo hakuna anyetaka kuziongea tena? Vipi kuhusu mamia ya lugha mpya za ‘Ki-programu’ (agh. kwenye tarakilishi) ambazo zimechepuka katika miongo iliyopita? Au aina mbalimbali za Kiingereza ambazo watu wanazipokea na “kuzichanganya tena” na kuzifanya zao wenyewew duniani kote? Hizi ni lugha za kweli na zinaonyesha uwezo zaidi ya Ki-Manx na Ki-Tirahi.

Abdullah Waheed, mzungumzaji asilia wa Ki-Dhivehi – lugha “rasmi” ambayo haina wazungumzaji wengi visiwani Maldives – anafafanua katika mfano mmoja ni kwa nini uhifadhi wa lugha ni muhimu:

[…]

Lugha ya Ki-Dhivehi ni ya muhimu sana kwa utambuzi wa watu wa Maldive kama watu na pia kama nchi, kwa sababu hilo ndilo jambo pekee tunaloshiriki wote na ambalo ni wengine wachache tu wanalo. Ni moja mkakati wa muhumi tunapoelekea kwenye maendeleo endelevu na uratibu muwafaka wa mambo yetu.

Mbali ya kuwa ni kitengo kilichotengwa kwa ajili ya waandishi peke yake, Ki-Dhiveli kipo katikati ya ya maisha yote ya kijamii, kiuchumi na kitamaduni. Ki-Dhiveli kinatuhusu sote. Kinatuhusu pale tunapotaka kutangaza uwingi wa tamaduni, na kupigana na ujinga, na kinahusu kiwango cha elimu, pamoja na ufundishaji katika miaka ya mwanzo ya elimu. Kinahusu katika mapambano kwa ajili ya ujumuishaji wa jamii , kwa ajili ya ubunifu, maendeleo ya kiuchumi na kulinda ufahamu wa watu wa makabila.

[…]

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.