Wiki ya Wanablogu wa ki-Caribiani 2016 Yalenga Kukuza Sauti za Eneo Hilo Mtandaoni

Screen shot from SiliconCaribe.com website.

Picha iliyopigwa kwenye tovuti ya SiliconCaribe.com.

Mjasiriamali wa teknolojia wa ki-Jamaika Ingrid Riley anaamini ni wakati muafaka kwa wanablogu wa eneo la Caribiani kuzama kwenye eneo hilo na kupaza sauti zao kwenye ulimwengu wa mtandaoni.

Yeye na kampuni yake maarufu iliyowahi kupata tuzo inayojishughulisha na teknolojia ya habari na kuratibu matukio kwenye eneo la Caribiani SiliconCaribe wanaanzisha Wiki ya Wanablogu wa Caribiani 2016 (#CBW2016) kuanzia Desemba 5-10, 2016. Mada katika tukio hilo la kwanza ni “Nguvu ya Ushawishi wa Mtandaoni ,” na lengo kuu ni kutengeneza jukwaa kwa ajili ya kuwatambua wanablogu wa Caribiani na wanablogu wenye asili ya eneo hilo. Wafahamike kuwa [wanablogu hao] nao wapo, na wana zo sauti.

SiliconCaribe Editor-in-Chief and founder of Caribbean Bloggers Week Ingrid Riley. (Screenshot from SiliconCaribe.com)

Mhariri Mtendaji wa SiliconCaribe na wanzilishi wa Wiki ya Wanablogu wa Caribiani Ingrid Riley. (Picha kutoka tovuti ya SiliconCaribe.com)

Asilimia sitini ya harakati hizo zitafanyika mtandaoni, ambako wanablogu chipukizi, wataalam wa kidijitali na wenye nguvu ya ushawishi watatangazwa wasifu wao na kufanyiwa mahojiano.

Tukio hilo la wiki nzima zitaratibu mikutano ya wanablogu itakayoandaliwa na wanablogu wenye asili ya Caribiani. Odessa Chambers, mmiliki wa blogu ya mitindo ya maisha na burudani accessjamaica.com ataandaa mkutano jijini Kingston, Jamaica. Mel Gabriel, anayetoka Visiwa vya Port of Spain [Bandari ya Uhispania] ambaye ni mwandishi, mhariri na mmiliki wa blogu ya CaribbeanLookBook.com, atakuwa ni mwenyeji mwenye asili ya Trinidadi. Mkutano wa New York meetup utaandaliwa na Mikelah Rose, mwanzilishi wa StyleandVibes.com. Jijini London, mkutano utaandaliwa na Ursula Barzey, mwanzilishi wa blogu ya safari za Caribiani na starehe CaribbeanandCo.com.

Tukio hilo la Wiki ya Wanablogu wa Caribiani ni fursa nzuri kwa waandishi na wachambuzi wa ki-Caribia kutengeneza habari za Facebook, alama ishara za Twita na hata kusambazwa kwa twiti zao, na hivyo kuanza kuleta tofauti kwenye mijadala ya kimataifa mtandaoni.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.