Jumuiya ya Mashoga Nchini Guyana Yaandaa Maandano ya Kwanza Kujivunia Ushoga

Picha ya Bendera ya Upinde wa Mvua kutoka kwa Jaime Pérez, CC BY-NC 2.0.

“Eneza Upendo na sio Chuki” ni kauli mbiu iliyosikika wakati wa maandamano ya kwanza ya wapenzi wa jinsia moja nchini Guyana ambayo yalifanyika juni 3, 2018. Ni tamasha ambalo liliwapa fursa jumuiya ya wapenzi wa jinsia moja kutoka nje ya nguo iliyowaficha na kudai haki zao ya kuona fahari ya vile walivvyo na wale waliochagua kuwapenda:

Shamrashamra zilianzia Viwanja vya Mapinduzi katika mji wa Georgetown, na washiriki walikuwa wamevaa nguo zenye rangi za upinde wa mvua na walikuwa wakicheza mziki wa soka wakati wakiandamana kwa mshikamano kupinga chuki na unyanyapaa:

Mapenzi kinyume na maumbile (ambapo mara nyingi hufahamika kama “umende” katika nchi nyingi za ki-Carribean) bado ni haramu nchini Guyana, pamoja na ushindi mkubwa katika shauri la Caleb Orozco huko Belize mwaka 2016, na hivi karibuni katika kesi ya Jason Jones huko Trinidad na Tobago, ambapo kesi zote inadhaniwa kuwa ni uhalifu dhidi ya katiba kufanya ngono kinyume na maumbile. Sio kuwa kesi zote hazikuwa na utata and mrejesho hasi, ukanda mzima — na vivyo hivyo na maandamano ya mashoga huko Guyana.

Raia wa mitandaoni walipiga kelele za kupinga. Katika bandiko moja huko Facebook, Yolanda Adams aliacha maoni yenye ukakasi kwamba anaangalia ni kwa kiwango gani dini inayo nafasi  katika jambo hili:

Mheshimiwa Rais kuwa na msimamo wako, kama unaunga mkono jambo hili, nchi italaaniwa kwa sababu Mungu yuko kinyume kabisa na jambo hili. Alishaliharibu taifa tayari kwa sababu ya kitendo hiki na bado hajabadilika. Huu sio wakati wa kumpendeza mwanadamu, jukumu lako la kwanza ni kuwalinda watu wasio na hatia, watoto. Kwa sababu kama hautafanya hivyo basi utakwenda kumjibu Mungu.
Kwa hiyo usifanye maamuzi kwa sababu ya kura, ni Mungu alikuweka hapo na sio mwanadamu.
Kwa hiyo, Mungu kwanza.

Pia Shanna Leaona Patterson alipinga kuondolewa kwa sheria:

Hii serikali itafanikiwa ikiwa itahalalisha matumizi kidogo ya bangi kuliko mwanaume-kinyume hivyo inabidi ifanye maamuzi kwa hekima.

Wa-Guyana huwaita mashoga “mwanaume-kinyume.”

Mtumiaji wa Facebook Brenda Oliver alikuwana haya ya kusema:

Watu wanajaribu jambo ambalo halitakaa lipitishwe Guyana. Guyana sio Marekani

Mtumiaji mwingine wa Facebook alisema kuwa tukio hilo lilikuwa na mkanganyiko wa wazi wa sheria za nchi na kulikuwa na majadiliano mengi kuhusu hukumu za kidini. Mchangiaji mmoja alipendekeza kuwa nchi ina mambo mengi ya kushughulikia — kwa mfano–mahusiano ya kiasili, ambayo ni ya msingi zaidi. Waliokuwa wanaunga mkono maandamano au angalau wale waliohifadhi maoni yaowalionekana kuwa wachache.

Hata hivyo kwa jumuiya ya mashoga ya Guyana, tukio hili ilikuwa ni hatua ya kwanza dhidi ya ukandamizwaji wanaokutana nao kwa sababu ya mrengo wa kujamiiana na utambulisho wao wa kijinsia. Mbunge Priya Manickchand, ambaye anaunga mkono juhudi za jumuiya hiyo, alisema kuwa “watu wanapaswa kufanya maamuzi yao wenyewe”, na serikali haina nafasi vyumbani mwa watu.

Kauli yake ilivuta kuungwa mkono mtandaoni. Mtumiaji wa Facebook Shannon Andre Persaud aliandika:

Siwezi kweli kuwavumilia watu wanaopinga Jamii ya Mashoga. Ni hatua ya kupendeza kuona jambo hili limepokelewa nchini Guyana ingawa sio bila vikwazo vya watu mbumbumbu. Lakini badala ya kuendelea kujihusisha na watu wenye ubaguzi na wasio na elimu nimeamua kujitenga nao na tatizo limeisha! Upendo ni upendo ❤ Na dunia hii ingependeza ikiwa hakuna ubaguzi na chuki na kukiwa na upendo mwingi na utu. #isupportthelbgtqcommunity

Pia kulikuwa na utetezi huko Twitter:

Maandamano hayo ni moja kati ya mifumo ya jamii kupigania haki sawa. Joel Simpson, mkurugenzi mtendaji wa Chama cha Kijamii kinachopinga Ubaguzi kutokana na namna ya kujamiina (SASOD) aliyeandaa maandamano hayo alikuwa na ujumbe kwa maafisa wa serikali–Jumuiya ya Mashoga inatarajia kuona vitendo.

Hata hivyo, bado kuna upinzani mkubwa. Katika mkutano siku moja kabla ya maandamano ya mashoga, wajumbe wa Jumuiya ya Wachungaji wa Georgetown walielezea kukerwa kwao na kutishia kutokupiga kura wakati wa uchaguzi. Jumuiya ya Kikristo ambayo inachukua asilimia 60% ya watu wa Guyana na ukichukulia mamlaka nyingine kikanda, inashawishi kuibadilisha sheria iliyopitwa na wakati ya ushoga. Jumuiya hiyo ilitishia hata kuyazuia maandamano hayo lakini kuliwepo na polisi wa kutosha hivyo hakuna tukio lililoripotiwa.

Simpson, aliyehudhuria mkutano kama mwakilishi wa jumuiya ya mashoga alionesha kuwa wananchi mashoga bado wanasubiri ahadi ya uchaguzi wa mwaka 2015 ambapo waliahidiwa mabadiliko ya sheria:

Tu wapiga kura na raia walipa kodi kama raia wengine…Hatudai kitu chochote maalum… Tunastahili kufurahia ulinzi dhidi ya unyanyapaa.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.