Takriban majira ya saa 12 za jioni (GMT +2), Idhaa ya Kiingereza ya Al Jazeera iliripoti kuwa shule moja ya Umoja wa Mataifa ilipigwa wakati makombora mawili ya vifaru yalipolipuka nje ya shule hiyo. Shule hiyo, iliyopo Jabaliya, ilianza kutumiwa kama makazi ya raia wa Gaza waliozikimbia nyumba zao au waliopoteza makazi yao. Kwa mujibu wa idhaa ya Kiingereza ya Al Jazeera, zaidi ya watu 40 wameuawa. Katika idhaa ya televisheni ya Kiingereza ya Al Jazeera (inayopatikana duniani kote kupitia Livestation.com) ilitangazwa kuwa jeshi la Israeli, IDF limepewa ramani za setilaiti, GPS, za mashule ya Umoja wa Mataifa.
Blogu ya Philistine iliripoti kwa haraka juu ya tukio hilo:
Waganga na maafisa wa afya wanasema idadi ya waliofariki kutokana na shambulio hilo la anga la Israeli nje ya shule ya Umoja wa Mataifa kwenye ukanda wa Gaza imefikia 30.
Shambulio hilo lilitokea kama yadi 10 hivi (mita) nje ya shule huko kaskazini mwa Gaza. Ni shambulio la pili la Israeli lililopiga shule ya Umoja wa mataifa katika masaa machache yaliyopita.
Mkurugenzi wa hospitali Bassa Abu Warda alithibitisha vifo 30 kutokana na shambulio la pili.
Katika mashambulio yote mawili, shule hizo zilitumiwa kama hifadhi ya watu waliopoteza makazi yao kutokana na mashambulizi ya Israeli.
Afisa mmoja wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa amelaani unyama huo na kutaka uchunguzi ufanywe.
Israeli haijatoa maoni yoyote.
Blogu ya Syria News Wire kadhalika iliripoti kwa haraka ikieleza:
Watu 40 wamefariki baada ya Israeli kutupa makombora kwenye shule ya Umoja wa Mataifa huko Gaza. Wapalestina 400 walipewa hifadhi shuleni hapo na Umoja wa Mataifa.
Mtumiaji wa huduma ya Twita domoniccampbell, aliyeko mjini London, alitoa maoni makali kuhusiana na taarifa hiyo:
Mtumiaji wa Twita wa Kifini haloefekti anaelezea kustushwa kwake na uhaba wa shutma kuhusu shambulio hilo: