Habari kuhusu Ureno
Rais wa Angola Aamsha Hasira Kwenye Mahojiano Yake Akidai Hakuna Njaa Nchini Kwake
"Leo kuna chakula cha kutosha Angola, hakuna mtu anayeweza kusema eti Angola ina njaa. Kilichopo ni utapiamlo," alisema Rais wa Angola kwenye mahojiano.
Mkutano: Kutengeneza Dunia Halisi ya Sauti za Dunia kwa Hadhira Halisi

Katika toleo hili la GV Face tunakutana na jopo la magwiji wa wawezeshaji wa mikutano ya Global Voices kutoka Misri, Pakistan, na Ureno.
Mwandishi wa Guinea Atoweka Kiajabu nchini Angola
Yuko wapi Milocas Pereira? Swali hili linarudiwa rudiwa kupitia blogu mbalimbali kwa majuma kadhaa sasa, lakini majibu yamekuwa vigumu kupatikana. Katika mitandao ya kijamii harakati zililipuka kuzishinikiza mamlaka za nchi ya Guinea kuchunguza mazingira ya kupotea kwa mwandishi huyo na mhadhiri wa Chuo Kikuu miezi sita liyopita katika jiji la Luanda, alikokuwa akiishi tangu mwaka 2004.
Cape Verde: Midahalo Kuhusu Vijana na Siasa Inayoendelea Huko Ureno
Kuna kundi la raia wa Cape Verde ambalo huandaa mikutano mjini Lisbon ili kujadili uhusiano kati ya vijana na siasa, kama anavyoeleza Suzano Costa katika video [pt] kama ilivyowekwa tena na...
Dunia Nzima: Lugha 2,500 Zinapotea
Ramani shirikishi ya lugha zinazopotea, inayoonyesha lugha 2,500 kati ya 6,000 ambazo ziko hatarini, imezinduliwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO). Shirika hilo la kimataifa linawaomba watumiaji wachangie kwa kutuma maoni kwenye mradi huo ambao unawatia mashaka wanablogu wengi wenye nia ya kuhifadhi tamaduni.