Mwandishi wa Guinea Atoweka Kiajabu nchini Angola

Yuko wapi Milocas Pereira? Swali hili linarudiwa rudiwa kupitia blogu mbalimbali kwa majuma kadhaa sasa, lakini majibu yamekuwa vigumu kupatikana. Katika mitandao ya kijamii vuguvugu lililipuka kuzishinikiza mamlaka za nchi ya Guinea kuchunguza mazingira ya kupotea kwa mwandishi huyo na mhadhiri wa Chuo Kikuu miezi sita liyopita katika jiji la Luanda, alikokuwa akiishi tangu mwaka 2004. Katika kikundi cha Facebook “SOS, STOP! – Queremos a Jornalista Milocas de volta” (Tunahitaji Mwandishi Milocas arudi) [pt] tayari kina wanachama 5,775.

Hivi karibuni, Rais wa Chama cha Jumuiya ya Wahamiaji wa Guinea-BIssau waishio Marekani, Celina Spencer, pia alizindua madai yaliyoelekezwa kwa Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, kujaribu na kupata msaada wa kujua aliko mwandishi huyo.

Alishiriki mahojiano kadhaa, akichambua majanga kadhaa ambayo yamekuwa yakitokea hivi karibuni ndani ya nchi ya Guinea-Bissau. Hususan, kuhusika kwa serikali ya Guinea na uwepo wa majeshi ya Angola yaliyoingizwa Guinea-Bissau kwa ajili ya mafunzo maalumu [habari ambazo Global Voices iliziripoti wakati wa mapinduzi ya Aprili 2012]. Haijulikani ikiwa kutoweka kwake kunahusishwa na mahojiano hayo au la. Ni hakika hata hivyo, alivamiwa na watu wasiojulikana. Baada ya hayo, akijisikia kutishiwa mjini Luanda, alitafakari na kumdokeza siri hiyo kwa rafiki kuwa alitamani kurudi nyumbani.

Katika mahojiano na televisheni ya Angola, mwanzoni mwa mwezi Januari, Profesa huyo alizungumzia hali ya mambo nchini Guinea-Bissau baada ya kifo cha Rais Malam Bacai Sanhá. Baada ya hayo, Milocas Pereira alisema kwamba alianza kujisikia kuwa kwenye shinikizo kubwa [pt].

Mnamo NOvemba 3,Sindicato dos Jornalistas Angolanos (Umoja wa waandishi wa Angola) [pt] ulidai kwamba mwandishi wa Guinea “amefanyiwa ugaidi” jijini Luanda:

Milocas Pereira foi agredida no início do mês de Maio por desconhecidos antes de ter comunicado a algumas pessoas com quem falou a sua intenção de deixar Angola, na sequência desta agressão, que foi apontada pela própria como sendo a causa mais próxima da sua decisão.

Milocas Pereira alishambuliwa mwanzoni mwa mwezi Mei na watu wasiofahamika, baada ya kuwa aliwasiliana na watu wake wa karibu aliokuwa amezungumza nao kuhusiana na nia yake ya kuondoka Angola. Alibainisha kuwa shambulio hilo lilikuwa ni sababu ya uamuzi huo.

Kwa mujibu waRadio “Sol Mansi” [pt], mwandishi huyo hakuwa na mashaka kuwa shambulio hilo lilikuwa na msukumo wa kisiasa:

Ela estava a correr risco de vida, pelo que a única solução que tinha era abandonar imediatamente Angola, para regressar ao seu país. Aconselhada pela sua amiga a denunciar publicamente a agressão, MP disse que preferia não o fazer. Aconselhada ainda a ir para Portugal, MP disse que não confiava nos portugueses e que se sentia melhor na Guiné-Bissau com os responsáveis de transição.

Alikuwa akikimbia hatari ya kupoteza maisha yake, na ufumbuzi pekee aliokuwa nao ulikuwa ni kuondoka haraka Angola, na kurudi nchini mwake. Akishauriwa na rafiki yake kutangaza kushambuliwa, mwandishi huyo alisema hakutaka kufanya hivyo. Baadaye akashauriwa kwenye Ureno, hata hivyo alisema hakuwa anawaamini Wareno na kusema alijisikia afadhali angeenda Guinea-Bissau kuwa na wale wanaohusika na wakati huo wa mpito.

Mwezi Oktoba uliopita, akitoa tamko katika kituo kile kile cha radio, Waziri wa Nchi kwa Masuala ya Jamii nchini GUinea-Bissau, Idelfrides Gomes Fernandes alithibitisha habari [pt] kuhusu uwezekano wa kutoweka kwa mwandishi kwa mara ya kwanza. Miezi Minne ya kutoweka kiajabu, familia iliamua kuwasiliana na mamlaka zinazohusika, lakini majibu pekee waliyoyapata ni kimya.

Katika toleo lake la 2 mwezi Novemba, the Novo Jornal (Gazeti Jipya) (Angola) lilitoa ukurasa mzima kwa habari za kupotea kwa mwandishi.

Katika toleo lake la 2 mwezi Novemba, the Novo Jornal (Gazeti Jipya) (Angola) lilitoa ukurasa mzima kwa habari za kupotea kwa mwandishi.

Miezi miwili iliyopita, Bartolomeu Capita wa taasisis ya National Movement of Cabinda (Vuguvugu la Kitaifa la Cabinda) aliandika katika tovuti yao Peace & collaborative development network kwamba Milocas Pereira inawezekana iliamuriwa auawe nchini Angola:

Hakuna aliyemwona Mama Pereira wala kusikia kutoka kwake kwa zaidi ya mwezi sasa. Na alikuwa akifundisha katika Chuo Kikuu cha Angola. Mashaka yamekuwa makubwa na yanahitaji kushughulikiwa. Wanazuoni wenzake wanahofia kuwa huenda ameuawa, baada ya kuwa alionyesha nia ya kufanya uchunguzi wa masuala ya namna utawala dhalimu wa Angola unavyohusiana na nchini ya Guinea Bissau.

Habari za kutoweka [pt] kwa mwandishi huyo mwenye umri wa miaka 58 zilikuwa hadharani wakati ambao familia yake -ambayo ilijaribu kurahisisha uchunguzi wa polisi- ilianza kupoteza matumaini kuwa Milocas alikuwa hai bado. Kaka wa Mhadhiri huyo, Carolos Pereira, anayeishi Lisbon, aliiambia Sauti la Marekani [pt]:

O que nos chega [de Luanda] é isso, está desaparecida desde finais de Julho. Suspeitamos de muita coisa. Que ela tivesse dado com muita coisa e tivesse necessidade de fugir, de esconder ou que tenha havido alguma retaliação.

KInachotujia [kutoka Luanda] ni kuwa, alitoweka tangu mwishoni mwa mwezi Julai. Tunahisi mengi. Kwamba huenda alikumbana na vingi na akaamua kuimbia nchi, akajificha au alifanyiwa vitendo vya kuliza kisasi.

Kwenye blogu ya Rispito [pt], raia wa Guinea Samba Bari anadhani kuwa kutoweka kwa mwandishi huyo ni changamoto nyingine kwa serikali ya mpito na kuwa hali hiyo inaweza kuongeza misuguano kati ya serikali ya Guinea isiyotambuliwa na Luanda na serikali ya Angola.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.