Mahojiano aliyoyafanya Rais wa Angola João Lourenço na RTP, Kituo cha Televisheni ya Taifa ya Ureno ambapo alisema kuwa hakuna njaa nchini kwake yamesababisha ghasia miongoni mwa wananchi.
Katika mahojiano ya dakika 30 yaliyorushwa Machi 4, mwanahabari wa Kireno kwa RTP Áfrika alirejea ripoti ya UNICEF iliyosema kuwa wananchi wanakufa kwa njaa nchini Angola. Rais Lourenço alikataa kuwepo kwa njaa nchini mwake, wakati akikubali kuwa kuna utapiamlo. Alisema:
A nossa luta é lutar para reduzir os índices de pobreza, devido aos longos anos de conflito armado. Hoje há oferta de bens alimentares em Angola, não se pode dizer que existe hoje fome em Angola, é uma questão de alguma má nutrição.
Mapambano yetu ni kupunguza kiwango cha umaskini uliotokana na kipindi kirefu cha vita. Kwa sasa kuna chakula Angola, huwezi kusema kuna njaa [kali] kwa sasa, ni suala la utapiamlo kidogo tu.
Rais João Lourenço alisema haya siku chache kabla ya kutembelewa na Rais wa Ureno Marcelo Rebelo de Sousa, na siku chache kabla ya Kasisi wa Kikatoliki na mwanaharakati wa haki za binadamu kukosoa vifo vya Waangola kwa sababu ya njaa katika maeneo yanayokabiliwa na ukame.
Mwanaharakati Manuel Mapanda anayefahamika zaidi kama Dago Nível, alihoji kuhusu kauli ya Rais :
Como é que o senhor vai dizer que não existe fome em Angola? Não leu a Denúncia do padre Jacinto Wacussanga sobre a morte de um Angolano por fome? Será que nos Gambos e no Curoca já não há fome? Assim que Jlo assumiu a presidência a maioria dos Angolanos passou a ter a cesta básica, e a fome foi eliminada?
Inakuwaje mwanaume anaenda kusema hakuna njaa Angola? Hakusoma ukosoaji wa Kasisi Jacinto Wacussanga kuhusu vifo vya Waangola kwa sababu ya njaa? Ina maana huko Gambos na Curoca hakuna tena njaa? Muda ule ule Jlo [João Lourenço] alipochukua madaraka ya Urais Waangola walipata mahitaji yao muhimu na njaa ikafutiliwa mbali?
Wakati wa mahojiano hayo mabaya, pia Mkuu huyo wa nchi ya Angola alieleza kuhusu kusudio lake la kukomesha rushwa ambapo ni sehemu ya mpango wa chama wakati wa uchaguzi:
Ninguém pode garantir que daqui para a frente não haverá corrupção e, que não haverá corruptos, mas que não ficarão impunes tal como sempre foi. Não haverá mais intocáveis, segundo João Lourenço. Esse tempo ficou para trás.
Hakuna mtu anayeweza kuhakikisha kuwa kuanzia wakati huu na kuendelea kutakuwa hakuna rushwa na hakutakuwa na watu wala rushwa lakini hawatabaki bila kuadhibiwa. Kulingana na João Lourenço, hakutakuwa tena na wateule wasioguswa. Kipindi hicho kilishapita.
Mwaka 2018, Regional Forum for University Development (FORDU), Jukwaa la Maendeleo ya Vyuo Vikuu lenye makao yake makuu huko kusini mwa Angola, lilitengeneza makala (ambapo hakuna nakala ya mtandaoni) iliyokuwa na jina la “Angola, nchi iliyo hatarini”. Makala hiyo ilionesha idadi kubwa ya watu wakitafuta chakula katika majalala katika maeneo ya katikati ya mji wa Huambo eneo ambalo makala hii ililenga na katika makao makuu ya nchi Luanda.
Huko JM. Notícias, ukurasa wa Facebook maalum kwa ajili ya kushirikishana habari kulikuwa na ukosoaji wa wazi dhidi ya maoni ya Rais:
Precisamos reconhecer que ainda há muita gente em Angola vivendo á [sic] margem da sociedade, problema que dificilmente se resolverá se não haver uma promoção de programas de inclusão social credíveis, onde é cobrado e prestado contas. E não com este nascer de uma nova elite de gatunos tipo quem não se safou no outro tempo, que aproveite á [sic] brecha agora em que o artista principal e financeiro da nação é o J.Lourenço.
Olha que os principais desafios estão ai mesmo diante dos vossos próprios olhos, em vencer os problemas nas áreas da saúde, educação, habitação, etc, que pelo menos já deveriam dar alguns sinais mesmo que tímidos, mais [sic] nada se vê .
Tunahitaji kutambua kuwa bado wapo watu wengi amba
o wanaishi maisha magumu nchini Angola, tatizo ambalo ni vigumu kulitatua ikiwa hakutakuwa na mpango wa kuaminika wa kukuza ushirikishwaji wa jamii ambapo ndipo inawajibika. Na sio kwa kuzaliwa kwa wasomi wapya wahuni wanaochukua fursa kwa kuwa mlango uko wazi kwa sasa kwa kuwa jemedari mkuu na mwezeshaji wa nchi ni J.Lourenço.
Ziangalie chamgamoto kuu ziko mbele ya macho yako, kukabiliana na matatizo katika sekta za afya, elimu, nyumba n.k. ambapo ingetakiwa iwe imeshaanza kuonesha dalili tayari hata kidogo, lakini hakuna chochote kinachoonekana.