India: Filamu ya Slumdog Millionaire Yanyakua Tuzo za Oscar

Filamu ya Danny Boyle, Slumdog Millionaire, iliyotokana na kitabu chenye maudhui ya India imefanya vyema katika sherehe za 81 za tuzo ya Academy. Wahusika wake kutoka Uingereza na India walitia kapuni zawadi 8 ikiwemo ile ya Picha Bora. Kwa hakika ilikuwa ni siku ya India, kwa kuwa filamu nyingine fupi ‘Smile Pinky’ pia ilishinda tuzo ya Oscar.

Sehemu ya waigizaji wa filamu ya Slumdog Millionaire wakiwa Hollywood – picha kwa hisani ya mtumiaji wa Twita KaushiK™,kwa idhini ya hati miliki za umma.

Watu duniani kote waliangalia sherehe za kutoa tuzo. Wengine walikuwa wakiblogu moja kwa moja, kama vile Sepia Mutiny. Kulikuwa na mamia ya jumbe za Twita zinazoandikwa kila dakika wakati wa matangazo ambapo kama sauti ya Raajesh ilivyosema:

Prerna wa No Borders and Binaries aliandika:

Majeshi ya wavamizi wa Kihindi pamoja na maswahiba wao wenye viza za kitalii wamenyakua tuzo inayotamaniwa na kuthaminiwa ya Oscar huku dunia ikiangalia. A R Rahman aliwashangaza na kuwachangamsha wote kwa kipaji chake cha muziki wakati akiongea pia sentensi za lugha ya Kitamil. Hii ni Marekani, Kiingereza-kitupu!!

Kadhalika kulikuwa na wale ambao hawakupenda Wahindi kuvamia sherehe za Oscar:

Lakini wanablogu wengi wa Kihindi waliupokea ushindi wa Slumdog Millionaire kwa furaha ya wastani. Tumewakilisha mchanganyiko wa maoni ya Wahindi wengi kuhusu filamu hii katika makala ya mwanzo ya Global voices. Wakazi wengi wanaoishi kwenye vitongoji visivyo na mpangilio mjini Mumbai ambko filamu hii ilichukuliwa, wameipinga kwa sababu wamepachikwa jina la mbwa koko wa mitaani au ‘slumdog’ katika filamu hiyo:

Mwanablogu, Meera Sinha anaandika:

Pamoja na hisia kwamba filamu ya Slumdog Millionaire haitakiwi kuchukuliwa kama filamu kielelezo ya umasikini wa Wahindi, imekuwa ni jambo la kusisimua kuiona India ikiwa katika mwangaza baada ya filamu hiyo kunyakua tuzo 8 za Oscar. Ninashawishika kuandika zaidi, lakini ni budi niingie kwenye chereko na kuepuka kuandika zaidi kero zangu zinazoihusu filamu hiyo.

Bloga Great Bong wa Random Thoughts Of A Demented Mind kadhalika hakuvutiwa:

Sababu moja, filamu ya Slumdog Millionaire kwa makusudi na kwa ufanisi mkubwa inagusa hisia ambazo waamuzi wa tuzo hiyo wanajulikana kuwa nazo. Ili kufaulu mtihani, sio lazima uwe mahiri zaidi – hata mtu wa wastani anaweza kufanya vizuri kama unaufahamu “mfumo” na akifanya yale ambayo yanatarajiwa. Filamu ya Slumdog Millionaire imefanya vizuri sana kwenye jambo hili.

Hitesh Bagai anajiuliza katika ujumbe wa Twita:

Lekhni wa The Imagined Universe anajaribu kupata sababu ya kwa nini Wahindi wanaichukia filamu ya Slumdog Millionaire:

Najiuliza ikiwa pingamizi letu kuu kwa filamu hii ni kwa sababu inaonyesha sehemu ya India ambayo hatupendi kuitazama. Tungependa kushangilia mafanikio yetu ya uchumi na ongezeko la watu wa tabaka la kati. Tungependa kuonyesha maduka makubwa ya kisasa na majengo ya vioo. Filamu hii haionyeshi utajiri wa watu wa India wa tabaka la kati. Inaonyesha India nyingine ambayo wengi wetu tunaifahamu fika, au tusiyopenda kuifikiria – India ya masikini iliyobakia masikini pamoja na maendeleo ya kiuchumi ya hivi karibuni.

Shripriya Mahesh wa Tatvam (Ukweli wa ndani) ameipenda hiyo filamu na anaandika:

Ni kwa nini mtengeneza filamu yeyote ajitwike mzigo wa kuuwakilisha mji au nchi? Hatengenezi filamu ya matukio ya kweli. Kuna hadithi ya kusimulia. Inahusisha picha ndogo ya mtazamo wa mji. Kutokea kwenye mtazamo wa maisha ya mhusika. Kazi ya mtengeneza filamu ni kusimulia hadithi hiyo kwa uwezo wake wote. Na hivyo ndivyo Danny Boyle alivyofanya. Na mimi, nimeyapenda matokeo.

Prerna anongelea uwezo wa India na anahitimisha:

Ndio, imembidi Mkurungenzi wa filamu kutoka Uingereza kutengeneza filamu yenye ‘maudhui ya India’ ili kuwapatia tuzo ya Oscar mafundi wa Kihindi ambao wamekuwa wakifanya kazi nzuri kwa miongo mingi (yaani akina Gulzar, A R Rahman, Pookutty). Slumdog Millionaire haiwezi kuzikaribia filamu za orodha-A za Bollywood ukichukulia uzoefu wake katika maudhui ya mapenzi yanayoshinda fedha. Na hii sio moja ya kazi bora zaidi za Rahman au Gulzaar. Wakti huo huo, ni jambo zuri kuwaona hawa mahiri wa muziki, hatimaye wanapata kutambuliwa ulimwenguni kutokana na filamu ambayo ni ya Kihindi. Hata hivyo, HIYO isiwe ndio kielelezo cha mafanikio. AR Rahman haihitaji Hollywood; Holywood inamuhitaji yeye.

Hongera kwa Slumdog millionaire na kwa Muhindi yeyote anayeipokea filamu hii kama filamu ya Kihindi.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.