Habari kuhusu Uandishi wa Habari za Kiraia kutoka Mei, 2014
Mazungumzo ya GV: Ukoaji wa Mafuriko Uliowezeshwa na Watu Nchini Serbia
Juma hili tunazungumza na marafiki waishio Serbia wanajihusisha na jitihada za ukoaji. Je, ni hatua zipi zinazochukuliwa na wananchi na serikali? Na kwa nini mitandao ya kijamii iko hatarini?
Polisi wa Masedonia Wawalazimisha Waandishi Kufuta Picha za Ghasia
Ghasia, zilizofumuka baada ya kuuawa kwa kijana wa miaka 19, zilisababisha misuguano kati ya watu wenye asili ya Albania na Masedonia kwenye jiji la Skopje.
Mwimbaji Mwingine Akamatwa China kwa Kuusifu Utamaduni wa Kitibeti
Kufuatia kukamatwa kwa mwimbaji wa Kitibeti Gepe nchini China,hapa ni mtiririko wa matukio ya jinsi hiyo sambamba na video za nyimbo husika kwenye mtandao wa YouTube.
Rwanda: Mema, Mabaya na Matumaini
Ingawa Rwanda imepiga hatua kubwa katika kuponya majeraha ya mauaji ya kimbari ya 1994, makundi ya utetezi yanaripoti vitendo vya uvunjaji wa haki za binadamu.
Sisi Ashinda Uchaguzi wa Rais Misri; Mpinzani Pekee Sabahi Ashika Nafasi ya Tatu
Jenerali Abdel Fattah Al-Sisi ameshinda urais kwa kishindo, huku akimbwaga mpinzani wake wa pekee Hamdeen Sabahi, ambaye ameshika nafasi ya tatu. Baada ya siku tatu za zoezi la upigaji kura, Sisi ameshinda kwa asilimia 93.3 ya kura zote. Hamdeen alipata asilimia 3 wakati asilimia 3.7 zimeharibika.
Je, Madaraka ni Matamu Kiasi cha Watawala wa Afrika Kushindwa Kuyaachia?
Gershom Ndhlovu anaangalia sababu za kwa nini watawala wa Afrika hawataki kuachia madaraka: Kumekuwepo na tetesi, dondoo na hata uvumi kuhusu afya au basi udhaifu wa afya ya Rais wa...
Changamoto za Elimu kwa Karne ya 21
Mikel Agirregabiria kwa kujifunza kutoka kwenye filamu Dead Poets Society aliweza kubainisha [es] mahitaji ya sasa ya elimu: Elimu katika karne ya 21 yahitaji kushughulikia masuala ambayo hayakuwa bayana siku...
Wanafunzi Waandamana Nchini Chile Kudai Mageuzi ya Kielimu
Katika maeneo kadhaa nchini Chile, maandamano ya wanafunzi kudai elimu ya bure na kushirikishwa kwenye mabadiliko yanayoendelea nchini humo yalifanywa Mei 8, 2014. Hata hivyo, yalikabiliwa na bughudha za hapa na pale.
Macau: Watu 3,000 Wazunguka Baraza la Wawakilishi Kukwamisha “Muswada wa Walafi”
Taarifa zaidi zinapatikana kwenyetaarifa yetu ya awali ya GV.
Naibu Waziri Ajinyonga baada ya Kushindwa Uchaguzi Nchini Malawi
Blogu ya City Press inaandika kwamba kujinyonga kwa Godfrey Kamanya, Naibu Wairi wa Malawi, baada ya kushindwa kukitetea kiti chake cha ubunge kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Mei 20, 2014 : Matangazo rasmi ya...