Habari kuhusu Uandishi wa Habari za Kiraia kutoka Mei, 2014
Uchaguzi wa Malawi 2014
Malawi inapiga kura kumchagua rais siku ya Jumanne Mei 20, 2014. Fuatilia taarifa za moja kwa moja kwenye mtandao wa Twita @Malawi2014 na @MEIC_2014.
PICHA: Watu 20,000 Waandaman huko Macau China Kupinga “Muswada wa Ulafi”
Muswada utampa mkuu wa serikali jimboni Macau, nchini China, kinga ya kushitakiwa kwa makosa ya kijinai wakati akiwa madarakani na ataaendelea kupata mshahara wake hata baada ya kuondoka madarakani.
Watu Wenye Ulemavu Kugombea Katika Uchaguzi wa Umoja wa Ulaya
"Sisi ni kikundi cha watu walioathirika, moja kwa moja au kwa namna moja au nyingine na ulemavu au lugha nyingine magonjwa nadra, tumeungana kwa lengo moja — nalo ni kuboresha maisha ya wale walioathirika."
Mapigano ya Wanakijiji Kugombea Ardhi Yasababisha Maafa Nchini Madagaska
Blogu ya L'Express Mada ilitoa taarifa kwamba kijiji kizima cha Andranondambo kilichoko Kusini mwa Madagascar kiliharibiwa [fr] kufuatia mapigano ya wanakijiji yaliyosababishwa na mzozo wa kumiliki ardhi. Vita vya wenyewe kwa wenyewe, ambayo ilidumu kwa siku tatu kati ya Mei 20-22, ilipoteza maisha ya wanakijiji wote. Akikumbuka tukio hilo, mmoja...
“Hatujaweka Mkazo vya Kutosha Kwenye Afya ya Vijana”
Ripoti ya hivi karibuni kutoka kwa Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu afya ya vijana duniani inabainisha kwamba: Sababu kubwa za vifo vya vijana duniani ni ajali za barabarani, VVU?UKIMWI, na kujiua. Duniani kote, wastani wa vijana milioni 1.3 walipoteza maisha yao mwaka 2012. Ripoti inaongeza vile vile kuwa :...
Jamaika: Alama Zinapoashiria Kikomo
Blogu ya Active Voice imetoa mkusanyiko wa twiti zenye mitazamo ya kupendekeza ufumbuzi kuhusu kampeni ya #bringbackourgirls inayodai kurudishwa kwa wasichana waliotekwa na magaidi wa Boko Haram.
Simulizi za Jinsia na Wajibu
Kwenye blogu ya EnGenerada kuna tafakari ya kina [es] juu ya ujenzi wa utambulisho wa jinsia na masimulizi yanazyohusishwa na wanawake na wanaume. Wanahitimisha kwamba, licha ya kuwa ndugu katika hali halisi, wanafanya kazi kama utaratibu wa kawaida wa kijamii. Makala iliyopitiwa upya hapa ni sehemu ya pili ya #LunesDeBlogsGV...
Baada ya Miezi Sita, Waathirika wa Kimbunga Haiyan Waendelea Kudai Msaada na Haki
Miezi sita baada ya kimbunga kikubwa kuharibu mamiliaoni ya makazi katika eneo la katikati ya Ufilipino, wahanga wanaendelea kuomba misaada na kutendelewa haki. Kuna madai ya kukosekana kwa mpango wa kurejesha hali kuwa ya kawaida.
Wajibu wa Kisayansi katika Mawasiliano
Katika mfululizo mpya wa Cosmos, Víctor R. Ruíz anaonyesha jinsi ambavyo kutafuta maarifa ya kisayansi limekuwa ni jukumu la kijamii na kisayansi katika nyanja za umma: Kabla na wakati huo, makampuni binafsi na serikali yalikuwa na ajenda ambazo daima hazikuwa zikiambatana na maslaha mapana ya jamii. Makampuni ya mafuta yaliendelea...
Gharama na Faida ya Kombe la Dunia Nchini Brazil
Blogu ya Daniel Bustos kutoka Colombia kuhusu uchumi wa Kombe la Dunia nchini Brazil na baada ya kugusia suala lisilo epukika la rushwa, inasema: Hatimaye, Brazil itatumika kama “panya” kwa mataifa ya Amerika ya Kusini ambayo yalikuwa na ndoto kuwa siku moja itaandaa tukio hili kubwa, itatumika kuuliza kama Brazil...