Watu Wenye Ulemavu Kugombea Katika Uchaguzi wa Umoja wa Ulaya

Kundi jipya la kisiasa linalowakilisha watu wenye ulemavu au magonjwa nadra limejiwasilisha kwa Uchaguzi wa Umoja wa Ulaya leo Mei 25.

Licha ya vyama vikubwa, maarufu, kuna wagombea wachache wa chama kama Movimiento Red (Harakati za Mtandao), Primavera Europea (Mapinduzi ya Ulaya), Vox, Podemos (Tunaweza), na Recortes (Punguza). Zaidi ya hayo, mwaka huu harakati mbadala, tena mpya kabisa zimeanzishwa, zinazofahamika kama Chama cha Wapiga Kura wenye Ulemavu na Magonjwa Nadra-DER [es]. Lengo lao kuu sio kutetea itikadi yoyote, ila kuboresha hali ya maisha kwa watu wanaoishi na ulemavu au magonjwa nadra.

Eduard Carreras, cabeza de la agrupación DER

Eduard Carreras, mkuu wa DER.

“Sisi ni kundi la watu walioathirika, moja kwa moja na ulemavu au ugonjwa nadra, tumeungana na lengo moja – kuboresha maisha ya wale walioathirika”, alisema Eduard Carreras, mgombea wa kundi hilo, kijana mwenye umri wa miaka 25 kutoka Girona, Hispania, anayeugua ugonjwa wa kudhoofu kwa misuli.

Jukwaa la uchaguzi[es] linajumuisha masuala kama ajira, kwa vile wao wanathibitisha kwamba vijana wenye ulemavu huwa na kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira kinachozidi 60%, na hivyo kuzuia kujitawala kwao na uhuru. Pia jukwaa hilo linalenga kupigania upatikanaji wa huduma za usafiri katika maeneo ya makazi, msamaha wa kodi kwa ajili ya huduma kama magari au dawa, kuongeza utafiti wa magonjwa nadra, na kuboresha, miongoni mwa mambo mengine, afya, elimu, na kwa wale walioathirika kuchukuliwa vyema na jamii.

[Kikundi hicho] hakitetei wala kukataa chama au itikadi yoyote. Lengo lao tu ni kulinda jukwaa lao la uchaguzi, ambayo kwa mujibu wa Carreras, ni “lengo kuu lililowaunganisha.” Aliongeza: “Sisi si chama haswa. Hatuna itikadi, ndio sababu njia yetu ni tofauti na vyama vikuu. “

Carreras amehakikishia kwamba “fedha zatakiwa kutumika katika mambo muhimu” na kwa sasa wao tayari wameonyesha hayo baada ya kupata saini 15,000 zilizohitajika kuweza kugombea katika uchaguzi, hawakutumia hata senti kwenye matangazo. Anaelezea:

Vamos a intentar convencer de que es necesario actuar rápido y tomarse en serio nuestros problemas, y vamos a denunciar a todo el que ponga obstáculos. Si nuestras propuestas son rechazadas, serán los que las rechacen quienes tendrán que justificarse ante sus ciudadanos. Estamos dispuestos a sumar, y serán bienvenidos quienes se sumen a nuestras propuestas.

Tutajaribu kuwashawishi kwamba ni muhimu kuchukua hatua ya haraka na kuchukulia matatizo yetu kwa umakini zaidi, na tutakemea kila kitu kitachoweka vikwazo kwa hili. Kama mapendekezo yetu yatakataliwa, wale watakaoyakataa na itawabidi kujieleza wenyewe mbele ya wananchi wao. Tuko tayari kujiunga na juhudi za watu wengine na kuwakaribisha wale ambao wataungana na mapendekezo yetu.

Hapa chini ni video kuhusu maono ya Kikundi hicho cha Wapiga Kura wenye Ulemavu na Magonjwa Nadra [es]:

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.