· Novemba, 2013

Habari kuhusu Uandishi wa Habari za Kiraia kutoka Novemba, 2013

Kufuatilia Kongamano la Dunia la Demokrasia 2013

  29 Novemba 2013

Kongamano la Dunia la Demokrasia kwa sasa linafanyika mjini Strasbourg, Ufaransa kwa mara ya ppili tangu lianze. Kauli mbiu ya mkutano wa mwaka huu ni “kuunganisha Taasisi na Wananchi katika Kizazi hiki cha dijitali”. Fuatilia mada nne na warsha 21 za mkutano kupitia alama ashiria #CoE_WFD. 

Wanasayansi Kutoka Duniani Kote Wakusanyika Nchini Brazil

  27 Novemba 2013

Jukwaa la Sayansi Duniani (WSF) linajumuisha mamia ya wanasayansi kutoka duniani kote wiki hii nchini Brazil, kujadili wajibu wao katika karne ya 21 na kusisitiza umuhimu wa ushauri wa kisayansi katika maamuzi ya kisiasa na kiuchumi. Brazil imekuwa mwenyeji wa matukio kadhaa ya kujadili kuondoa umaskini na maendeleo endelevu kutoka...

VIDEO: Serikali Yaharibu Misikiti Nchini Angola

Uharibifu wa misikiti isiyopungua 11 katika miezi miwili iliyopita nchini Angola imechochea athari ya hasira kwenye mtandao. Kwa mujibu wa Voz da América [pt], Mamlaka ya Angola ilisema kuwa sababu ya uharibifu ni ujenzi kinyume cha sheria na ripoti&nyingine kuongeza kwamba mchakato wa kuhalalisha Uislamu na dini nyingine katika nchi haijawahi...

Mkutano wa Global Kampala, Uganda

Sauti Chipukizi  25 Novemba 2013

Mkutano wa Global Voices umepangwa kufanyika Novemba 23 jijini Kampala, Uganda, kuwaleta pamoja wanachama wa jamii hii kushirikisha mawazo.

Sera ya Taarifa ya Uwazi Yahitaji Kuboreshwa zaidi Nchini Japan

  22 Novemba 2013

Pamoja na kuwa serikali ya Japan inajitahidi kupiga hatua katika uboreshaji wa sera yake ya uwazi, nchi hii bado ina safari ndefu, kwani imeshika nafasi ya 30 kati ya nchi 70, kwa mujibu wa orodha liyoandaliwa na Asasi ya Ujuzi Huru. Masahiko Shoji wa Asasi ya Ujuzi Huru nchini Japani aandika:...