Tuzo za kwanza za uandishi wa kiraia nchini Uganda (SMAs) zilitolewa kwa mara ya kwanza Novemba 15, 2013 kwenye kituo cha Teknolojia kiitwacho The Hub, kwenye mtaa wa maduka ya Oasis jijini Kampala, Uganda.

Bango la Tuzo za Uandishi wa Kiraia za mwaka 2013.
Malengo ya tuzo hizo, ambayo iliandaliwa na BluFlamingo, yalikuwa:
Tuzo hizi za Uandishi wa habari za kiraia za tukio la kwanza linalotafuta kuwaleta pamoja watu binafsi na mashirika ambayo yako mstari wa mbele linapokuja suala la kutumia vyombo vya habari za kiraia kwa minajili ya burudani, kuleta mabadiliko, kubadilishana mawazo, kutengeneza jumuiya na kuwasiliana na wateja mtandaoni.
Tuzo hizo zinalenga kuwatuza watu na mashirika yanayofanya jitihada za dhati kuupa nguvu uandishi wa kiraia ili kuhusika na kujenga jumuiya mtandaoni kuanzia kwa watumiaji wa mtandao wa Facebook mpaka watumiaji wa mtandao wa twita na wanablogu wanaojituma.
Tukio la kwanza kama hili lilifanyika Novemba 15 2013 na liliwaleta si tu watu wanaojua masuala ya kidijitali, lakini pia mashirika makubwa yaliyo mstari wa mbele katika uandishi huu mpya na wale walioshiriki katika kukuza uandishi wa habari za kiraia nchini Uganda.
Washindi wa kila kundi walikuwa kama ifuatavyo:
Tovuti bora ya burudani – BigEye
Mwandishi bora wa Burudani – Moses Serugo
Mwanablogu bora – Beewol
Kampuni kubwa bora – MTN Uganda
News & kampuni ya habari – NTV Uganda
News & habari za watu – Songa Stone
Huduma za Umma bora – Mamlaka ya Jiji la Kampala
Ubunifu bora – Matatu
Huduma bora za wateja – Airtel Uganda
Haki za jamii – Wanasheria pekupeku Uganda
Tuzo ya Udhibiti ya Majanga – Shirika la Taifa la MajiSafi na MajiTaka
Shirika bora la kuchapisha habari – The Red Pepper
Radio bora – Power FM
Runinga bora – NTV Uganda
Mtu maarufu – Anne Kansiime
Upigaji picha – Echwalu Photography
Kampeni bora ya uandishi wa kiraia – 40 & tabasamu 40
Chaguzo la Jaji – Proggie Uganda
Washindi walipendekezwa kupitia upigaji kura wa mtandaoni na baadae walichaguliwa na jopo la Majaji watano.
1 maoni