Mkusanyiko wa Makala za Kuvuliwa Madaraka kwa Mbunge Maarufu Nchini Tanzania

Ben Taylor aweka mkusanyiko wa makala zinazohusiana na kuvuliwa madaraka kwa Zitto Kabwe,mbunge maarufu na kijana wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema. Zitto:

[…] alivuliwa nyadhifa zote rasmi na viongozi wakuu wa chama mapema siku ya ijumaa asubuhi. Zitto Kabwe hatakuwa tena Naibu katibu Mkuu wa chama wala naibu kiongozi mkuu wa kambi rasmi ya upinzani.

Sababu ni ipi? Mwenyekiti wa chama, Freeman Mbowe, alieleza kuwa, Zitto aligundulika kuwa ni miongoni mwa waliohusika na njama za kumpindua mwenyekiti wa chama hicho na kuichukua nafasi hiyo (na bila shaka kuwania kiti cha Rais), pamoja na makosa mengine ya uvunjaji sheria ndani ya chama.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.