Mkutano wa Global Kampala, Uganda

gv-meetup-logo-gvmeetup-400Mkutano pili wa Global Voices utafanyika jijini Kampala, Uganda Novemba 23, 2013 katika sehemu iitwayo Hive Colab.

Mkutano huu unawalenga kimahususi mamia ya waombaji wa ufadhili mdogo Sauti Chipukizi kutoka nchini kote Uganda. Kwa miaka mitatu iliyopita, tulipokea maombi mengi kutoka Afrika Mashariki, hii ikiwa ni pamoja na kona zote za Uganda. Tunatarajia kwamba mkutano huu utasaidia kuwezesha mahusiano ya kirafiki baina ya marafiki.

Mkutano utawaleta wengi wa wanachama wa jumuiya hizi kushirikishana uzoefu na kusaidia kuwezesha mitandao ya kimahusiano miongoni mwa wale wenye kupenda yanayofanana au wenye maoni yanayoendana. Ukiwa umeandaliwa na wanachama wetu wawili Maureen Agena (@maureenagena) na Rosebell (@RosebellK), pamoja na wanachama wengine wanaojitolea wa GV, mkutano huo utajikita kwenye masuala yafuatayo:

  • Kuelezea kazi za Global Voices, Rising Voices, Advox, na Lingua, na namna jamii ya Uganda inavyoweza kuhusika na miradi hiyo,
  • Kubainisha njia nyingine ambazo jamii ya mahali hapo inaweza kushirikiana miongoni mwao kwa kubadilishana utaalamu na nyenzo ma kujadili miradi na mawazo,
  • Kujadili namna mitandao ya kijamii inavyoweza kutumika katika kazi zao, ikiwa ni pamoja na kupata uzoefu kutoka kwa washiriki.

Kwa kuwa lengo la mkutano huu ni kwa ajili hasa ya waombaji wa zamani wa ufadhili, mwaliko ulitumwa awali kwa makundi hayo, na nafasi zote zimejaa. 

Fuatilia tukio hilo kupitia mtandao wa twittwe kwa anuani hii#GVMeetup na kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na: rising [at] globalvoicesonline.org

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.