· Novemba, 2012

Habari kuhusu Uandishi wa Habari za Kiraia kutoka Novemba, 2012

Mkanganyiko wa Makubaliano ya OIC Kuanzisha Ofisi Nchini Myanmar

  30 Novemba 2012

Shirika la Ushirikiano wa Kiislam (OIC) limependekeza kuanzisha ofisi nchini Myanmar kwa lengo la kukisaidia kikundi kidogo cha Waislamu nchini humo. Serikali ilishakubaliana na mpango huu lakini ilibadili uamuzi huu mara baada ya kutokea maandamano ya kupinga uamuzi huo katika maeneo mengi ya nchi.

Mwanzilishi wa Kikundi cha Kijeshi Kilichofutwa Nchini Pakistani Ajitolea Kuisaidia Marekani.

30 Novemba 2012

Wakati kukiwa na makelele na uharibifu mkubwa huko ukanda wa pwani ya mashariki mwa Marekani unaotokana na kimbunga kikubwa kijulikanacho kwa jina la Sandy, Hafiz Mohammad Saeed, mwanzilishi wa shirika la kijeshi lililofutwa la Lashkar e Taiba (LeT) na kiongozi wa Jaamat ud Dawa (JuD) ajitolea kutoa misaada ya kibinadamu kwa Marekani ili kufidia uharibifu.

Mradi wa Tafsiri: Kauli ya Linda Uhuru wa Intaneti Ulimwenguni

GV Utetezi  20 Novemba 2012

Katika siku saba zijazo, Wafasiri wa Kujitolea wa Mradi wa Lingua wa taasisi ya Global Voices watakuwa wakitafsiri makala maalumu ambayo ni harakati ya utetezi unaofanywa na umma mtandaoni na ambao unasaidia kulinda haki za watu kwenye mitandao ya intaneti na kuzitaka serikali zilizo wanachama wa Muungano wa Kimataifa wa...

Watoto wa Mitaani Bangladesh Wakabiliwa na Unyanyasaji

  13 Novemba 2012

Jumla ya watoto wa mitaani nchini Bangladeshi wanakadiriwa kufikia 400,000. Karibu nusu ya idadi hiyo wanaishi katika Jiji la Dhaka. Asilimia kubwa ya watoto hao ni wasichana. Wasichana hao wa mitaani huishi katika mazingira yenye hatari nyingi hasa unyanyasaji na dhuluma nyingine.