Watoto wa Mitaani Bangladesh Wakabiliwa na Unyanyasaji

Pale inapotokea umekwama kwa dakika chake katika taa za barabarani katika mji mkuu wa Bangladeshi Dhaka, bila shaka utaona watoto wakijazana kwenye madirisha ya gari lako. Miongoni mwao kuna wale watakaokuwa wamebeba maua; wengine marundo ya vitabu, wengine magazeti na hata wapo wale wanaouza pipi. Wote wanafanya kila linalowezekana kuwavutia wasafiri barabarani ili wauze bidhaa zao. Sura hii ya kuhuzunisha inatawala mitaa mingi ya jiji la Dhaka. Katika jiji hili watoto hao hujulikana kwa jina la Pothoshishu. Ni huko mitaani ndiko wanakojipatia riziki.

Jumla ya watoto hao wa mitaani nchini Bangladeshi inakadiriwa kuwa laki nne (karibu nusu milioni). Karibu nusu ya idadi hiyo wanaishi katika jiji la Dhaka peke yake. Miongoni mwao, walio wengi ni wasichana. Watoto hawa wa kike wanakabiliwa na unyanyasaji na vitendo vingine vya dhuluma dhidi yao.

Street girls Mili and Brishti

Wasichana wa mitaani Mili na Brishti wanajitafutia riziki kwa kuuza maua. Picha na Firoz Ahmed. Hakimiliki Demotix (21/1/2012)

Mwezi Machi, 2012 Unnayan Onneshan alichapisha ripoti iliyopewa kichwa cha habari “social connection of the street girls in the context of Dhaka city, Bangladesh” [pdf] yaani ‘Uhusiano wa kijamii wa wasichana wa mitaani katika muktadha wa jiji la Dhaka, Bangladeshi. Utafiti unaonyesha kwamba wengi kati ya wasichana hao wa mitaani (37.50%) hujipatia riziki kwa kuuza maua. Asilimia 18.80 kati yao hulazimishwa kujihusisha na ukahaba, asilimia 6.25 hufanya kazi katika viwanda vya nguo, asilimia 6.25 huwa ombaomba, asilimia 12.50 hufanya kazi za kuuza duka na asilimia 6.25 ni wachuuzi wa magazeti. Karibu nusu ya wasichana hawa wana kipato cha kujikimu tu kipatacho kama Tk. 101-299 (dola za Marekani 1.25 hadi 3.75, kama Tsh2,000 – Tsh5,000). Kipato cha kila siku cha asilimia 43.75 ya wasichaa ni Tk. 300 (dola $3.75, sawa na Tsh5,000) na zaidi. Lakini hao ni wale ambao wana bahati sana, kwa sababu asilimia 6.25 ya wasichana wa mitaani hupata chini ya Tk. 100 (dola 1.25, sawa na Sh2,000) kwa siku. Karibu asilimia 45 ya wasichana hawa hawapati hudma zozote za afya katika vituo vya afya vya serikali. Wasichan 3 kati ya 10 hawajawahi kupata elimu ya aina yoyote katika taasisi zinazohusika na elimu.

Wakawake wengi nchini Bangladeshi wako kwenye hatari ya kufanyiwa dhuluma kama vile ubakaji, kuuwawa, kuchezewa, mahari na hata kumwagiwa tindikali. Lakini watoto wa mitaani wasio na makazi katika jiji la Dhaka wanakabiliana na hatari hizi kila siku. Kielelezo hiki kimechukuliwa kutoka kwenye ripoti iliyotajwa hapo juu, inayoonyesha takwimu za ukatili wanaofanyiwa wasichana wa mitaani:

Takwimu kuhusu vitendo vya ukatili dhidi ya wasichana wa mitaani

Neelkabyo anaandika kuhusu hali ilivyo mbaya inayowakabili wasichana wa mitaani hapa Jukwaa la Addar Asor:

Pale inapokuwa vigumu kuhakikisha usalama wa mabinti zetu katika nyumba zetu wenyewe, suala la kufikiri kuhusu asilimia 25.7 ya wasichana wanaoishi mitaani kwa hakika ni la kuogofya sana.

Nizam Kutubeeanaandika kupitia Prothom Alo Blog:

Hivi karibuni kumekuwepo na majadiliano mengi kuhusu sheria za kudhibiti vitendo vya ukatili vya ngono. Lakini hakuna anayelipa uzito suala la usalama wa wasichana wa mitaani. Hawa daima hufanyiwa dhuluma za kingono kwa sababu huwalazimu kulala mitaani pasipo kuwa na ulinzi wowote. Lakini hakuna mtu serikalini anayeonekana kujali kuhusu watoto hao.

Living under the open sky.

Kuishi pasipo na makazi rasmi katika eneo la wazi. Picha na Auniket. Hakimiliki ya Demotix (6/4/2012).

Mwanablogu Maa alichukua vipande vya wimbo maarufu wa KiBangla ili kujaribu kuweka wazi suala hili na kuomba kwamba watoto hawa wapatiwe makazi salama:

Hebu jua jipya liyaangazie malisho haya ya kijani, hebu ulimwengu na uwe mahali salama pa kuishi

Hebu tuufanye ulimwengu uwe mahali salama kwa watoto, je, hili ni jambo kubwa sana ninaloliomba?…

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.