Uharibifu Nchini Syria Katika Picha

Makala hii ni sehemu ya habari zetu maalum kuhusiana na Mgogoro wa Syria 2011/12.

Wapiga picha wa Syria kutoka katika maeneo mbalimbali ya nchi wanafichua, kutuma sehemu mbalimbali na kuweka kumbukumbu ya machafuko katika picha zinazoonesha uharibifu uliotokea. Pamoja na ufinyu wa vitendea kazi vya utoaji habari, habari zinazotoka Syria zinaonesha hali ya kutisha inayowakabili wananchi wa tabaka la chini kabisa na huku wakishuhudia nchi yao inavyoraruliwa na kuachwa vipande vipande. Pamoja na kuwa hakuna nyenzo za kuweza kuonesha picha hizo zinapatikana wapi wala idadi ya wahanga, zifuatazo ni baadhi ya picha chache zinazoonesha namna miundo mbinu na makazi ya watu yalivyo athiriwa.

Miongoni mwa mamia ya wapiga picha, Yazan Homsy ‏ ametushirikisha matukio ya uharibifu wa makazi. Anajitambulisha kama:

يزن الحمصي – ابن حمص العدية – ناشط في الثورة السورية من حي الخالدية ثورة حتى النصر أو الشهادة …

@YazanHomsY: Yazan Homsy, mtoto wa jiji la Homs, mwanaharakati katika mageuzi ya Syria kutoka katika eneo la Khalidya . Mapinduzi mpaka mafanikio au kufa kishahidi.

Alituma picha zake katika ukurasa wake wa Facebook, akielezea uharibifu wa majengo katika jiji la Homs. Zifuatazo ni picha zake mbili miongoni mwa picha alizonazo, zilizotumiwa kwa ruhusa.

Homs: siku 139 za kuzingirwa kwa majengo 14 jijini Homs. Ni miezi sita na wanajeshi wa Assad walitumia kila aina ya milipuko na mabomu ya kutupa katika kuharibu maeneo mbalimbali ya jiji la Homs yaliyokuwa yamezingirwa. Chanzo: Ukurasa wa Facebook wa Yazan Homsi . Imetumiwa kwa ruhusa.

Soko la zamani jijini Homs baada ya kulipuliwa kwa bomu na kuunguzwa. 06/13/2012. Chanzo: Yazan Homsi Ukurasa wa Facebook wa Yazan Homsi. Imetumiwa kwa ruhusa.

Mtandao wa Habari wa Syria S.N.N [ar] pia umekuwa tayari wakati wote kuweka picha kwenye mtandao huo zikionesha uharibifu katika majiji muhimu matatu ambayo ni Aleppo, Homs na Damascus
Zifuatazo ni baadhi ya picha kutoka katika mtandao huo:

Syria – Homs – 10/21/2012 – Uharibifu uliotokana na majeshi ya Al Assad kutupa mabomu – Picha na Mohammed Ibrahim – MTANDAO WA HABARI WA SHAAM | Muwasilisha habari (108) SNN . Imetumiwa kwa ruhusa.

Syria – Homs – 10/21/2012 – Uharibifu uliotokana na majeshi ya Al Assad kutupa mabomu – Picha na Mohammed Ibrahim – MTANDAO WA HABARI WA SHAAM | Muwasilisha habari (102) SNN . Imetumiwa kwa ruhusa.

Syria – Homs – 10/19/2012 -Uharibifu uliotokana na majeshi ya Al Assad kutupa mabomu – Picha na Mohammed Ibrahim – MTANDAO WA HABARI WA SHAAM | Muwasilisha habari (39) SNN . Imetumiwa kwa ruhusa.

Syria – Aleppo – Jiji la kale – 13/10/2012 – Uharibifu na moto kufuatia kutupwa kwa bomu katika msikiti (12) wa Umayyad. Picha kutoka Mtandao wa habari wa SHAAM| SNN Imetumiwa kwa ruhusa

Syria – Aleppo – 09/23/2012 – Uharibifu uliotokana na kutupwa kwa bomu la kushtukizwa pamoja na kombora zito. Picha kutoka Mtandao wa habari wa SHAAM| SNN Imetumiwa kwa ruhusa

Syria – Damascus – Tadamon – 07/09/2012 – Uharibifu katika maeneo ya karibu yaliyotokana na mabomu yaliyotupwa na majeshi ya Assad (6). Picha kutoka Mtandao wa habari wa SHAAM| SNN Imetumiwa kwa ruhusa

Syria – Damascus – Erbeen – 29/10/2012 – Jengo lililoharibiwa kufuatia majeshi ya Assad kutupa mabomu kwa wakazi waishio jijini humo. Picha kutoka Mtandao wa Habari wa SHAAM| SNN. Imetumiwa kwa ruhusa.

Makala hii ni sehemu ya habari zetu maalum kuhusiana na Mgogoro wa Syria 2011/12.

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.