Maelfu Watia Saini Pendekezo la Zawadi ya Nobel na Kusherehekea Siku ya Malala

Binti wa miaka 15 Malala Yousafzai alipigwa risasi mnamo tarehe 9 Oktoba 2012 wanamgambo wa kundi la TTP (Tahreek-e-Taliban Pakistan) [Kundi la Tabiban la nchini Pakistani] kwa sababu tu alikuwa mwanaharakati asiyeogopa aliyetetea elimu kwa ajili ya wasichana huko Swat. Malala hivi sasa anazidi kupata nafuu akitaraji baada ya hapo kurejea katika maisha ya kawaida kama wasichana wengine wa umri wake. Hivi sasa hayupo tena katika hatari ya kupoteza maisha kwa sababu ya shambulio lile, ingawa kupona kabisa kutachukua muda.

Pendekezo la Zawadi ya Nobel ya Amani

Kumetolewa pendekezo na mwanamke mmoja raia wa Uingereza mwenye asili ya Pakistani anayeishi katika jiji la Birmingham, Shaida Choudry, kumpendekeza Malala Yousufzai kutunukiwa Tuzo ya Nobel. Pendekezo hili kuhusu Malal kutunukiwa Tuzo ya Nobel kunaweza tu kufanikiwa endapo ‘wanasiasa katika nchi yake’ wataunga mkono. Shaida Choudry anawataka William Hague, David Cameron, Nick Clegg na Ed Miliband kuchukua wajibu huo na kuupa msukumo.

Hadi sasa watu wapatao laki moja wametia saini pendekezo hilo. Sababu kwa nini zawadi ya Nobel itunukiwe kwa Malala imeelezwa waziwazi:

Tuzo ya Nobel kwa Malala itapeleka ujumbe wa moja kwa moja kwamba ulimwengu unafuatilia na kuwasaidia wale wanaotetea usawa wa kijinsia na haki za binadamu, ikiwemo haki ya elimu kwa wasichana.

Neno ufunguo la #Malala kwenye Twita limesambazwa na zaidi ya watu elfu tano. Neno ufunguo #Nobel4Malala limesambazwa na kiasi cha watu mia tisa katika siku tisa. Akieleza sababu zake za kutia saini kwenye pendekezo hilo, Farina Alam anaandika akisema:

…Malala ananipa matumaini

Stephen Furlong anatoa maoni akisema:

“Ujasiri na imani kubwa hivyo katika umri huo mdogo hauna budi kutambuliwa na kutumika kama njia ya kuwatia moyo na kama kielelezo cha matumaini kwa vijana na wazee kila mahali ulimwenguni”

Kuadhimisha Siku ya Malala

Umoja wa Mataifa umetangaza kuisherehekea tarehe 10 Novemba (Jumamosi) kama Siku ya Malala. Watu kote ulimwenguni walimshangilia Malala kama kielelezo cha wasichana wapato milioni 32 ambao hawana fursa ya kupata elimu. Nchini Pakistani, maandamano ya kumwunga mkono Malala yalifanyika katika majiji ya Islamabad, Lahore, na Karachi. Siku hii iliadhimishwa katika nchi zaidi ya 100 kote ulimwenguni.

Lakini katika mji anakotokea Malala hakuna shughuli za nje ya nyumba zilizofanyika yote kwa sababu ya kuhofia uwezekano wa shambulizi la kigaidi.

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukuaji wa elimu ulimwenguni, Bw Gordon Brown alikuwa nchini Pakistani siku ya Ijumaa (tarehe 9 Novemba) ili kujadiliana kuhusu mustakabali wa elimu ya wasichana nchini humo. Akizungumza na Shirika la Habari a AFP alisema kwamba nchi haiwezi kuendelea endapo tu ni asilimia 2 ya bajeti za nchi inatumika kwa ajili ya elimu. Zinahitajika juhudi zaidi ili kubadili hali hiyo ya mambo.

Vuguvugu la MQM (Muttahida Quami Movement) [Vuguvugu la Umoja wa Kitaifa] lilisherehekea rasmi Siku ya Malala katika kituo chao cha kisiasa kinachoitwa nine-zero:

MQM celebrating Malala Day

Wanachama wa Vuguvugu la MQM likisherehekea Siku ya Malala. Kutoka Twita @SahilMQM

Kainat – rafiki yake Malala waliyekuwa pamoja wakati shambulio lilipotokea — alisema — kwamba bado ana woga mwingi mno na hulia sana kila mara anapolikumbuka. Kwa bahati mbaya, hakukuwa na sherehe huko Swati kwa sababu ya hatari ya shambulio la kigaidi.

Ili kuonyesha upendo wake kwa Malala, msichana mwenye miaka 11, Bushra Siddique, anaandika kwenye blogu yake:

Kwa maoni yangu, Malala ni kama mwale wa mwanga na matumaini kwa nchi ya Pakistani. Mwenyezi Mungu Amlinde!

Mwitikio kwenye Twita

Salman Ahmed anatuma twiti:

@sufisal: “Kuielimisha akili bila kuuelimisha moyo ni kazi bure.” ― Aristotle#Malala Day

Somuya Singh anatuma twiti:

@soumyasinghs#Pakistanyaadhimisha Siku ya Malala… Watoto Maskini#children watapata fedha taslimu endapo watahudhuria shule. Tuombe ili waende kweli shuleni. jifunze kitu #learn ..

Ali Salman Alvi alitoa maoni kwamba watetezi wa magaidi wamekuwa wakijaribu kupuuzia kitendo cha kishujaa cha Malala:

@alisalmanalvi: Kwenye Mitandao ya Kijamii ilikuwa ni Malala akipambana na Al-Qaeda na wapambe wao (watetezi wa kundi hilo la magaidi) katika Siku ya Malala. #Pakistan

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.