Habari kuhusu Uandishi wa Habari za Kiraia kutoka Disemba, 2009
Malawi: Wanablogu Wajadili Matetemeko ya Ardhi 30 Katika Wiki 3
Katika kile ambacho baadhi ya wataalamu wa miamba wamekieleza kama matukio ya nadra, Wilaya ya Kaskazini ya Karinga nchini Malawi imeshuhudia jumla ya matetemeko ya ardhi 30 katika wiki tatu zilizopita ambayo yamesababisha vifo 5, zaidi ya watu 200 kujeruhiwa na zaidi ya watu 3,000 kupoteza makazi. Wanablogu wamekuwa wepesi kushirikiana maoni.
Uganda: Rais Kuzuia Muswada Unaopinga Ushoga
Muswada Unaopinga Ushoga wa 2009 uliopendekezwa nchini Uganda bado unasubiri uamuzi wa mwisho utakaotolewa na bunge la nchi hiyo, lakini gazeti la Daily Monitor lilitaarifu Jumatano kuwa Rais Yoweri Museveni ameihakikishia Idara ya Mambo ya Nje ya Marekani nia yake ya kuukwamisha muswada huo
Morocco: Mwanablogu Mwingine Atupwa Gerezani
Mnamo tarehe 14 Desemba, siku ya Jumatatu, mwanablogu Bashir Hazzam na mmiliki wa mgahawa wa Intaneti Abdullah Boukhou walihukumiwa kifungo cha miezi minne jela kwa huyo wa kwanza na mwaka mmoja kwa huyo wa pili pamoja na kulipa faini ya MAD 500 (sawa na dola za Marekani 63) kila mmoja katika mahakama ya Goulmim.
Misri: Makao Makuu ya Kuzimu Duniani
Wanablogu na wanaharakati wengi wa Kimisri wamekuwa wakikamatwa na Usalama wa Taifa katika nyakati tafauti kwa sababu mbalimbali –za kweli au za bandia –Wa7da Masreya aliwahoji wanablogu mbalimbali na kuweka makala ya kina kuhusu mbinu za utesaji na hila za kisaikolojia ambazo wanablogu wale wamekuwa wakikumbana nazo kwenye makao makuu ya Usalama wa Taifa katika wilaya ya Jiji la Nasr.
China: Kujitoa Uhai kwa Msomi Mwingine tena – Kisa cha Yang Yuanyuan
YANG Yuanyuan, binti msomi mwenye miaka 30 aliyekuwa na shahada ya uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Shanghai Maritime, alijinyonga kwenye bafu la nyumbani kwake mnamo Novemba 25 mwaka huu. Siku...
Canada Imesema Nini? Upotoshaji wa Habari Kwenye Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi
Serikali ya Canada inasemekana imetoa tamko la jazba leo, ikikanusha upotoshaji wa habari zinazodaiwa kufanywa nayo kwa mujibu wa Jarida la Wall Street likidai kwamba Canada imebadili sera yake na itakuwa ikikubaliana na malengo ya kupunguza hewa ya ukaa.
Urusi: Simulizi Tatu za Umaskini Uliokithiri
Mwandishi wa habari mpiga picha wa Urusi, Oleg Klimov, anatusimulia visa vitatu vya umaskini uliokithiri ambavyo alipata kusikia habari zake wakati akisubiri treni katika kituo cha treni cha Syzran, jiji lililo katika eneo la Samara la Urusi.
Wapiga picha wa Kiafrika, waandishi na wasanii wapata sauti zao kwenye blogu
Kadri Waafrika wengi wanavyozidi kugundua nguvu ya kublogu kama zana ya kutoa maoni kwa kiwango cha dunia nzima, tarakimu ya wanablogu imeongezeka na pia maudhui yanayopewa kipaumbele. Kwa tarakimu hiyo ya kukua kwa blogu, wasanii wengi wa Kiafrika wamejiunga, na ongezeko kubwa likionekana kwenye blogu za mashairi kama ilivyo kwa upigaji picha unaochipukia na blogu za sanaa za maonyesho. Tunazipitia baadhi.
Tunisia: Mwanafunzi Atupwa Gerezani kwa Kuhojiwa na Chombo cha Habari
Wanaharakati nchini Tunisia wamezindua ukurasa wa Facebook na blogu ili kumuunga mkono Mohamed Soudani, 24, aliyetoweka mnamo tarehe 22 Oktoba 2009 nchini humo mara baada ya kufanya mahojiano na Redio Monte Carlo International na vilevile Redio France International. Tangia hapo marafiki walipata fununu kwamba alikamatwa na kutupwa korokoroni na kuteswa vibaya.
Iran: Maandano ya Siku ya Mwanafunzi kwenye YouTube
Maelfu ya waandamanaji hawakuujali utawala wa Kiislamu leo kwa kuandamana wakati wa siku ya mwanafunzi, wakiimba kaulimbiu dhidi ya Ali Khamenei, kiongozi wa Jamuhuri ya Kiislamu, na wakipinga sera ya mambo ya nje ya serikali.