Habari kuhusu Uandishi wa Habari za Kiraia kutoka Oktoba, 2010
Tanzania: Majumuisho ya Habari za Uchaguzi Mkuu wa 2010
Mnamo tarehe 31 Oktoba 2010, Watanzania watashiriki katika uchaguzi wa Rais wa Muungano, Rais wa Zanzibar pamoja na Wabunge na Wawakilishi katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Huu ni mjumuisho wa yale yaliyojiri katika blogu mbalimbali kuhusiana na uchaguzi huo.
Tanzania: Ulimwengu wa Blogu Wachambua Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2010
Ifikapo tarehe 31 Oktoba 2010, Watanzania zaidi ya milioni 19.6 watafanya uamuzi muhimu kuhusu hatma ya nchi yao. Watafanya hivyo kupitia uchaguzi mkuu wa nne chini ya mfumo wa vyama vingi. Wakati zimebaki siku chache kabla ya uchaguzi huo, ulimwengu wa blogu wa Tanzania nao unafuatilia kwa karibu yale yanayotokea katika kampeni za vyama mbalimbali.
Irani: Ziara ya Rais Ahamdinejad Nchini Lebanoni
Rais wa Irani, Mahmoud Ahmadinejad, amemaliza ziara yake ya siku mbili nchini lebanoni. Ilikuwa ni ziara yake rasmi ya kwanza tangu mwaka 2005 wakati alipochukua madaraka. Alikuwa na mazungumzo na maofisa wa Lebanoni na alizuru ngome za maswahiba wa Irani. Alipata mapokezi ya shujaa. Wanablogu kadhaa wa Irani walitoa maoni kuhusu ziara hiyo.
Moroko: Kupinga Mateso Sehemu Moja; Kupinga Mateso Kila Sehemu
Wanablogu wa Moroko wamekuwa wakionyesha kukasirishwa kwao juu ya tabia ya kutojali ya vyombo vya habari vikubwa na unafiki wa serikali yao kufuatia kifo cha kijana wa KiMoroko mikononi mwa wawakilishi wa serikali.
Urusi: Wanablogu wakutana na Balozi wa Irani, waepa kuhoji masuala nyeti
Mkutano kati ya wanablogu wanaoongoza nchini Urusi na Balozi wa Irani jijini Moscow, siku tatu tu baada ya mwanablogu Hossein Derakshan kuhukumiwa kifungo cha miaka 19.5 jela kwa kile kilichoelezwa kuwa ni "kufanya propaganda zinazoipinga serikali" ulizionyesha wazi juhudi zisizoeleweka za diplomasia ya mtandaoni ya Irani nchini Urusi. Vilevile ulionyesha jinsi maslahi binafsi ya kibiashara pamoja na mtizamo taharuki uliopita kiasi wa baadhi ya wanablogu maarufu wa Urusi.
Tanzania: Matumizi ya Vyombo vya Habari vya Kijamii kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2010 Nchini Tanzania
Tanzania inaelekea katika uchaguzi wake mkuu mnamo Oktoba 31 mwaka huu na hivi sasa kampeni za uchaguzi zinaelekea kileleni. Wakati kampeni zikipamba moto, wagombea wa nafasi ya urais, ubunge na udiwani wameanza kutumia zana mpya za mawasiliano ya jamii ili kuwasiliana na wapiga kura. Sanjari na mikutano ya kampeni, ambayo hulenga watu wengi zaidi, idadi ndogo ya wanasiasa wameanza kutumia zana za mawasiliano ya kijamii kama vile blogu, picha za video za mtandaoni, Facebook na Twitter ili kukuza mawasiliano na wapiga kura.