Irani: Ziara ya Rais Ahamdinejad Nchini Lebanoni

Rais wa Irani, Mahmoud Ahmadinejad, amemaliza ziara yake ya siku mbili nchini Lebanoni. Ilikuwa ni ziara yake rasmi ya kwanza tangu mwaka 2005 wakati alipochukua madaraka. Alikuwa na mazungumzo na maofisa wa Lebanoni na alizuru ngome za maswahiba wa Irani, Hezbollah, katika vitongoji vya kusini mwa mji mkuu na kusini mwa Lebanoni ambako alipata mapokezi ya shujaa. Wanablogu kadhaa wa Irani walitoa maoni kuhusu ziara hiyo.

Meybodema amechapisha picha kadhaa za ziara ya Ahmadinejad nchini Lebanoni na kumnukuu [fa] Sayyid Hassan Nasrallah, kiongozi wa Hezbollah, ambaye aliisifu Jamhuri ya Kiislamu na kumkaribisha Ahmadinejad.

Mwanablogu huyo alimnukuu Nasrallah akisema kwamba kinyume na propaganda zote, “Irani inawasaidia wanaokandamizwa”.

Sayeh Azadi alichapisha tena (tafadhali angalia hapo juu) kikaragosi kilichochorwa na mchoraji vikaragosi anayeongoza nchini Irani Nikahang kutoka kwenye Roozonline [fa] kikaragosi hicho kilikuwa na kichwa cha habari kinachosema “Ndoto za Ahmadinejad kwa Lebanoni”.

Z8unak anahesabu sababu zinazoeleza ni kwa nini watu wa Lebanoni walimkaribisha Ahmadinejad. Mwanablogu huyo anaandika [fa]:

Kwa nini mlishangaa kwamba Ahmadinejad alipokelewa vizuri mno nchini Lebanoni? Baada ya miaka 20 ya vita vya Iraki-Irani, miji ya mpakani haikujengwa lakini nyumba nchini Lebanoni zilijengwa kwa pesa zetu. WaIrani wengi hawawezi kumudu kwenda kwa daktari au hospitali na matokeo yake wanakufa kila siku, wakati huo huo irani inajenga hospitali nchini Lebanoni.

Mollah anaandikakwa kejeli:

WaLebanoni hawakuona ubaya wowote wa serikali ya Irani. Kama tungekuwa WaLebanoni na kupokea pesa hizo tungegeuka kuwa waunga mkono wa Jamhuri ya Kiislamu… Wanasema, hartujali ikiwa wapo madarakani baada ya ‘mapinduzi ya nguvu’ au ikiwa wanatesa watu… ili mradi wanatoa pesa.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.