Mkutano kati ya wanablogu wanaoongoza nchini Urusi na Balozi wa Irani jijini Moscow, siku tatu tu baada ya mwanablogu Hossein Derakshan kuhukumiwa kifungo cha miaka 19.5 jela kwa kile kilichoelezwa kuwa ni “kufanya propaganda zinazoipinga serikali” ulizionyesha wazi juhudi zisizoeleweka za diplomasia ya mtandaoni ya Irani nchini Urusi. Vilevile ulionyesha jinsi maslahi binafsi ya kibiashara pamoja na mtizamo taharuki uliopita kiasi wa baadhi ya wanablogu maarufu wa Urusi.
Mnamo tarehe 30 Septemba 2010, watumiaji wa LJ tema, nl, sergeydolya na wengine wachache walitembelea ubalozi wa Irani ili kukutana na “Wanablogu wa kutoka Irani”: Balozi Seyed Mahmoud-Reza Sajjdi (anayejulikana pia kama mtumiaji wa LJ sajjadi [RUS]) na Pavla Ripinskaya (anayejulikana kama pashili), mwandishi wa kitabu kinachoitwa “Incredible Iranians/Umahiri wa WaIrani)”. Sergey Dolya, mwanablogu maarufu wa masuala ya safari na mjasiriamali wa zana za kijamii za mtandaoni, alituma makala hii akionyesha alivyofurahishwa [RUS]:
Обед длился пару часов. По-русски посол господин Реза Саджджади не говорит и общался через переводчика. Вначале он рассказал нам краткую историю своей страны…
[…]
Потом мы позадавали вопросы. Похоже, что так же как и о Ливане, у нас неправильное мнение об Иране. Люди там добрые, открытые и гостеприимные. В общем, надо ехать и проверять. Господин Посол обещал помочь с визой.
В целом, встреча прошла очень позитивно. Много шутили, мороженое в конце поели. Посол подарил нам по 2 коробки фисташек (реально вкусные оказались, сладенькие) и книжку на русском языке в палец толщиной о том, как устроена политическая система Ирана. Могу одолжить почитать интересующимся.
Kisha tuliuliza maswali. Yaelekea mtazamo wetu kuhusu Irani hauko sahihi, kama jinsi ulivyo kwa nchi ya Lebanoni. Watu wa nchi hiyo ni wakarimu, wana maoni binafsi na ni wakarimu. Kwa ujumla, tunaweza kwenda ili kushuhudia wenyewe. Balozi ameahidi kusaidia kwa kushughulikia visa.
Kwa ujumla, mkutano ulikwenda vema sana. Tulitaniana sana, mwishoni tulikula malai. Balozi alitupatia maboksi mawili ya pistachio (aina ya vitafunwa kama karanga/korosho) na kwa kweli zilikuwa tamu sana, vilevile kitabu ambacho ni kina unene kama wa kidole kinachozungumzia mfumo wa kisiasa wa Irani. Ninaweza kuwaazima wale ambao wangependa kukisoma.
Mwanablogu Norvezhskiy Lesnoy, kadhalika, (kupitia makala yake)alionekana mkavu na aliyekosa dhati kama tu lilivyo gazeti la Urusi [RUS]:
В ходе беседы блоггеры обсудили перспективы развития российско-иранских отношений на современном этапе, обменялись мнениями по ряду актуальных вопросов международной повестки дня. Стороны выразили удовлетворение динамичным развитием отношений между блоггерами двух стран, подчеркнув взаимную заинтересованность в их укреплении на благо дружественных народов России и Ирана.
Tarehe ya mkutano inaashiria kwamba ilikuwa ni juhudi ya Irani kujaribu kutengeneza mwonekano wake katika macho ya ulimwengu wa blogu wa Urusi. Hakuna mwanablogu mwingine aliyeshiriki kwenye mkutano huo aliyeandika chochote kuhusiana na mkutano huo. Baadaye, Sergey Dolya alikataa kujibu maoni yoyote yaliyogusa suala la haki za binadamu nchini Irani. Ukengeuke wa wanablogu waliokubali kushiriki kwenye tukio hilo la “diplomasia ya mtandaoni” (na, hata zaidi ya hayo, baadaye kuliandikia), katika kipindi ambapo mwanablogu nchini Irani amepata adhabu kali kupindukia katika historia ya dunia, ni jambo lililomkasirisha sana [RUS] Denis Loktev, mwanahabari wa televisheni:
Российские блогеры радуются как дети, когда их приглашают посидеть за одним столом с послом Ирана, развешивают там уши лопухами под рассказы о достоинствах иранской политической системы, уходят осчастливленные пакетиком сладеньких фисташек и принимаются рассказывать благодарным слушателям, как же они раньше ошибались насчёт Ирана и какая же это на самом деле замечательная страна: http://sergeydolya.livejournal.com/219995.html
О том, почему в Иране их коллег-блогеров бросают умирать в тюрьме за критику режима, любители халявных фисташек как-то не поинтересовались.
Какой позор.
Wapenzi hawa wa pistachio za bure wameshindwa kuhoji kwa nini wanablogu wenzao nchini Irani wanatupwa jela ili kufia humo kwa sababu tu wamekosoa utawala uliopo madarakani.
Aibu gani hii.
Mwanablogu mwingine maarufu, mtumiaji wa LJ drugoi, yeye pia hakujua [RUS] afasiri vipi kwanini wanablogu wenye maelfu ya marafiki waliamua kushiriki kwenye mkutano kama huo na kushindwa kuhoji maswali kuhusu yale yanayotokea kwa ulimwengu wa blogu nchini Irani.
Mtumiaji wa LJ sumlenny alieleza [RUS]:
кстати, этот постинг Доли отлично показывает, почему все надежды на то, что блоггеры-де контролируют власть, концерны и пр. лучше СМИ – это достаточно нелепые надежды. Блоггеры – такие же нелюбопытные, манипулируемые и пр. люди, плюс к этому они не имеют даже тех небольших моральных и профессиональных тормозов, которые имеют журналисты даже в самых несвободных СМИ. Случаи успешного контроля со стороны блоггеров за властями и пр. скорее стоит отнести на случай невероятну удачных совпадений.
Katika majadala mwingine, mwanablogu iratus aliandika [RUS]:
Самое неприятное в этих людях, это то что у них нет никакой позиции. […]
Неужели вы правда ждали от этих людей неудобных вопросов г-ну послу? […] Им все равно рядом с каким флагом фотографироваться, лишь бы рейтинг не падал. А то в будущем перестанут на халявные мероприятия звать и билеты на самолеты и отели оплачивать.
Hivi, ulifikiri kwamba wangeweza kumuuliza Balozi maswali yoyote yale ya kumkera? […] Hawajali ni bendera ipi iliyopo ambayo watapigwa picha pamoja nayo, cha muhimu kwao ni kwamba umaarufu wao haushuki. Kwa kuwa kama jambo hili litatokea ina maana kwamba hakuna atakayewaalika kwenye matukio ya bure na kulipia ndege na hoteli huko siku za usoni.
Ulimwengu wa Blogu wa Urusi, kama ilivyo jamii ya Urusi, ina mfumo wa tabaka unaofuata ngazi. LiveJournal na mfumo wake wa kuwa na “marafiki” na upangaji wa viwango ambao umejikita katika mfumo huo [RUS],unawakilisha moja ya miundo ya mfumo wa tabaka unaofuata ngazi katika ulimwengu wa mtandaoni. Pengine, mfumo huo wa tabaka unaofuata ngazi unaweza kueleza vizuri ni kwa namna gani LiveJournal ilitokea kuwa maarufu sana miongoni mwa wanablogu wa Urusi.
Idadi ya marafiki, na vilevile idadi ya viunganishi rafiki na maoni, vina athari yake kwa idadi ya maoni yanayotolewa kwa mwanablogu katika LiveJournal. Umaarufu, kwa kiasi fulani, hupatikana moja kwa moja na kwa uhalisia, lakini vilevile kwa upande fulani kutokana na msaada wa mbinu mbalimbali za “kubambika” matokeo ya viwango vya ufuatiliwaji (kwa mfano, pale kundi la wanablogu wasio maarufu sana wanapotoa maoni kwenye makala za makundi maarufu zaidi). Kadiri kunavyokuwa na maoni zaidi na viunganishi, basi ndivyo nafasi inavyokwenda juu ya “mwanablogu aliye juu zaidi” katika viwango vya utoleaji maoni. Pale inapotokea tu kwamba “mwanablogu huyu aliye juu” kuingia katika orodha ya wanablogu 50 bora, basi mara moja anaanza kupata ofa kutoka kwenye wakala za masuala ya Uhusiano na mashirika ya kibiashara ili wawe wakitoa maoni kuhusu bidhaa ya makampuni hayo. Baadhi ya wakala wa Uhusiano wana mitandao yao wenyewe ya wanablogu ambao kazi yao ni kutangaza bidhaa, huduma au hata ujumbe wa kisiasa.
1 maoni