Tanzania: Matumizi ya Vyombo vya Habari vya Kijamii kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2010 Nchini Tanzania

Tanzania inaelekea katika uchaguzi wake mkuu mnamo Oktoba 31 mwaka huu na hivi sasa kampeni za uchaguzi zinaelekea kileleni. Wakati kampeni zikipamba moto, wagombea wa nafasi ya urais, ubunge na udiwani wameanza kutumia zana mpya za mawasiliano ya jamii ili kuwasiliana na wapiga kura. Sanjari na mikutano ya kampeni, ambayo hulenga watu wengi zaidi, idadi ndogo ya wanasiasa wameanza kutumia zana za mawasiliano ya kijamii kama vile blogu, picha za video za mtandaoni, Facebook na Twitter ili kukuza mawasiliano na wapiga kura.

Ni vigumu kutoa maoni yaliyo sahihi kuhusiana na athari ya kampeni hizi za mtandaoni hasa kwa kuwa hakuna takwimu za hivi karibuni kuhusu matumizi ya zana za mawasiliano ya jamii nchini Tanzania. Idadi ya Watanzania wanaotumia Intaneti bado ni ndogo kwa kulinganisha na idadi jumla ya watu. Katika nchi ambayo inakadiriwa kuwa na watu milioni 41, kunakuna watumiaji wa Intaneti wapatao 676,000 hiyo ikiwa ni sawa na asilimia 1.6 ya idadi ya watu. Katika hao wenye kuweza kutumia Intaneti, kuna watumiaji wa facebook wapatao 141,580, ambapo kati yao asilimia 74 wana umri wa kati ya miaka 18 na 34.

Hakuna uhakika juu ya nani ameanzisha utumiaji huo – iwe ni wagombea wenyewe wa urais au ubunge ama na maafisa rasmi wa timu za upigaji kampeni – kuna tovuti, blogu, kurasa za Facebook na akaunti za Twita chache, pamoja na zile za wagombea wa chama kinachotawala cha CCM. Tovuti rasmi ya mgombea urais wa chama kinachotawala cha CCM, Jakaya Mrisho Kikwete, ina kiungo cha ukurasa wa facebook wenye zaidi ya wafuasi 4,500. Pia kuna ukurasa mwingine wa facebook wa Bw. Kikwete ambao una washabiki wanaozidi 13,500.

Mgombea mwenza wa Kikwete ambaye ndiye anayewania nafasi ya Makamu wa Rais, Dkt. Gharib Bilal,yeye ana zaidi ya tovuti moja. Tovuti moja imeunganishwa na ile ya Bw Kikwete pamoja na akaunti ya Twita ya Dkt. Bilal , wakati tovuti nyingine ina kiungo kinachoelekea kwenye ukurasa wa facebook ambao ni maalumu kwa ajili ya kampeni zake.

Mmoja wa wagombea wa nafasi ya urais kutoka vyama vya upinzani, Dkt. Wilbrod Slaa wa chama cha CHADEMA anaukurasa wa facebook unaounganishwa na tovuti rasmi na ambao una washabiki wapatao 910. Kadhalika kunazaidi ya kurasa mbili za facebook ambazo ni maalumu kwa ajili ya kampeni za Dkt Slaa zikiwa na watu 9000 ‘wanaompenda’ Dkt. Slaa. Pia ana akaunti ya twita yenye twita chache mno.
Kama ilivyo upande wa Tanzania Bara, ilani za uchaguzi, picha na video za mikutano ya kampeni nazo zimetundikwa kwenye tovuti za mgombea urais wa Zanzibar wa chama cha CCM Dkt. Ali Mohamed Shein na vilevile zile za mpinzani wake mkubwa, Maalim Seif Sharif Hamadwa Chama cha Wananchi (CUF).

Kampeni hizi za mtandaoni, ambazo hutangazwa kupitia Twita na Blogu, hupandisha vipande vya picha za video kutoka katika mikutano ya kampeni na mpaka sasa zimepata watembeleaji wanaozidi 12,000 mpaka wakati wa kuandika makala haya. Baadhi ya video zinaonekana kwamba zilipandishwa moja kwa moja kutoka katika maeneo ilipofanyika mikutano hiyo, kama vile hiikutoka katika mkutano wa kampeni cha mgombea ubunge jimbo la Kigoma Kaskazini wa CHADEMA Mh. Zitto Kabwe:

Wakati huo huo video nyingine kama vile hii inayotoka kwenye mkondo wa Youtube wa January2010zaidi inaonekana kwamba ilitengenezwa kitaalamu zaidi: :

Matumizi ya majukwaa ya mawasiliano ya kijamii yamewezesha timu za kampeni kuwasiliana na kujibu maswali ya wapiga kura. Zana hizo pia zimewapa fursa Watanzania wanaoishi ng'ambo kufuatilia matukio ya nyumbani Tanzania.

Baada ya CCM kukataa kushiriki katika midahalo inayohusiana na uchaguzi, kama ilivyoelezwa na mwanablogu Shurufu Anasema, mtumiaji wa twita Issa Mwamba alimpa changamoto Kikwete:

AmbapoKikwete2010 alijibu:

Mimi binafsi nafikiri CCM kama chama huru kina haki ya kuchagua kishiriki kwenye midahalo ipi na ipi kisishiriki.

Ingawa kuna mashaka kama kweli kampeni za mtandaoni zitakuwa na athari kwa wapiga kura katika nchi ambayo utumiaji wa Intaneti ni wa kiwango cha chini, baadhi ya wanablogu kama vile Spotistarehe wana matumaini:

Je Vijijini wanasoma facebook?

Asilimia kubwa ya watumiaji wa mitandao hii wako jijini Dar Es Salaam na mikoa mikubwa kama Arusha, Morogoro, Tanga, Mwanza na kwa siku hizi mitandao inafika kote.

Jiji hili la Dar wakazi wengi ni wakuja wanatoka vijijini ambako wabunge wengi hutoka huko. Mathalani mi ni mtu wa Morogoro Kilombero, bila vyombo vya habari siwezi kujua mgombea wa Ubunge wa jimbo langu ana sera gani, lakini kama nitakuwa nasoma mawazo yake kupitia updates za mara kwa mara kwenye mitandao hii naweza nikawa mpiga debe mzuri… nikibahatika naweza washauri ninawafikia kuwa Bwana Kibonde ni mtu safi na nia ya kutukwamua anayo tumachagueni

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.