· Januari, 2013

Habari kuhusu Uandishi wa Habari za Kiraia kutoka Januari, 2013

Jukwaa la Kiafrika Lenye Makala za Bure za Kitaaluma

Januari 24, ni siku ambayo inategemewa kuwa ya kuzindua rasmi Hadithi, ambalo ni jukwaa la kuhifadhia zana za bure za kitaaluma mjini Nairobi, Kenya. Wasomi mbalimbali na wadau wa mitandao watakusanyika pamoja kujadili upatikanaji wa zana huru za kitaaluma katika elimu ya juu nchini Kenya. Hadithi itasaidia kutafuta, kuona na kushusha...

Wafalme Watatu Watembelea New York

  14 Januari 2013

Wafalme watatu walikuja na kuondoka, lakini siyo kabla ya kupita katika jiji la New York ili kusherehekea na mamia ya watoto waliojitokeza kwa ajili ya paredi. Shamra shamra hizi za Noeli, kwa karne nyingi, zimekuwa ni sehemu ya utamaduni wa watu wa Amerika wenye asili ya Karibeani na Walatini..The Three Kings came and went, but not before passing through New York City to celebrate with hundreds of children that came out for the parade. This Christmas celebration has been a part of the Caribbean and Latin American cultural traditions for numerous centuries.

Mwanaharakati wa Pakistani Khudi Ali Auawa Katika Mlipuko wa Bomu

  14 Januari 2013

Mnamo Januari 10, 2013 katika jiji la Quetta lililopo Kaskazini Mashariki mwa nchi ya Pakistani, watu 82 walipoteza maisha kwenye milipuko ya mabomu yaliyolenga eneo ambalo kimsingi lenye idadi kubwa ya Waislamu wa Shia jamii ya Hazara. Irfan Khudi Ali, mwanaharakati mashuhuri wa haki za binadamu ambaye bila kuchoka aliweka wazi uonevu wa kikabila unaofanywa kwa waShia wa Hazara nchini Pakistan, alifariki katika shambulio lililofuata. Kifo chake kimechochea watu kumpa heshima kwa juhudi zake kwa kuanzisha tena maandamano kupinga mauaji ya watu wa Shia nchini Pakistani.

Mashoga Washambuliwa Kaskazini mwa Kameruni

Oscarine Mbozo’a anaripoti [fr] katika blogu ya L'Actu kuwa shoga mmoja akiwa ameambatana na mwenzi wake walizomewa karibu na soko mnamo tarehe 6, Januari 2013, mjini Maroua, Kaskazini mwa Kameruni: Goche Lamine, mfanyabiashara wa madawa, alikamatwa na mwanafunzi wa shule ya sekondari aitwaye Sanda, mwenye umri wa miaka 17. Umati wa...