Habari kuhusu Uandishi wa Habari za Kiraia kutoka Mei, 2017
Makosa ya Uhalifu wa Mtandaoni dhidi ya Mwanzilishi wa Kampeni ya Jeshi la Manyanga Yafutwa
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Seriakali ya Jamaica amemfutia mashitaka yote matatu yaliyokuwa yakimkabili mwanaharakati La Toya Nugent, chini ya sheria ya nchi ya makosa ya uhalifu wa Mtandaoni.
Wito wa Kimataifa wa Kudai Haki Wawaunganisha Wachoraji Nchini Guatemala
Ni miezi miwili sasa tangu wasichana 41 kuuawa kwa kuchomwa moto kwenye nyumba ya kulelea watoto inayosimamiwa na serikali. Hata hivyo, serikali ya Guatemala imekuwa imekuwa ikisuasua kwenye kuchukua hatua.
Idadi Kubwa ya Raia Nchini Brazil Waungana na Kufanya Mgomo wa Kitaifa.
Waandamanaji wanashikilia msimamo kupinga mfululizo wa mabadiliko yanayolazimishwa na Rais wa Brazili Temer, mwenye wingi wa vitu vya wabunge na uungwaji mkono wa wafanyabiashara pamoja na kupoteza umaarufu wake.
Rais wa Tanzania Afukuza Watumishi 10,000 Kwa Madai ya Kughushi Vyeti
Uamuzi huo ni sehemu ya nia ya Rais John Magufuli kufanya mabadiliko kwenye utumishi wa umma.
Ajali ya Basi Yaua Makumi ya Watoto Kaskazini mwa Tanzania
Nchi hiyo ya Afrika Mashariki ina idadi kubwa ya ajali za barabarani barani Afrika.