Makosa ya Uhalifu wa Mtandaoni dhidi ya Mwanzilishi wa Kampeni ya Jeshi la Manyanga Yafutwa

Mwonekano wa baadhi ya watu waliokusanyika wakati wa matembezi ya Uwezeshwaji wa Wahanga wa Jeshi la Manyanga kwa ajili ya kukabiliana na unyanyaswaji kijinsia. Picha na Storm Saulter, imetumiwa kwa ruhusa.

Chini ya sheria mpya ya makosa ya mtandao ya nchini Jamaica, mwanaharakati La Toya Nugent alikamatwa Machi 2017 kwa kle kinachodaiwa kuwataja hadharani kuptia mitandao ya kijamii watuhumiwa wa unyanyasaji wa kijinsia. Mapema Mei 17, 2017, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP) alifutilia mbali mashtaka yake yote, na hivyo kumfanya Nugent kuwa mwanamke huru, na kuuthibitishia umma kuwa kampeni mpya ya Jeshi la Manyanga,ambayo hapo awali ilitiliwa mashaka inayoongozwa na mwanamke pamoja na wahanga wa unyanyasaji wa kijinsia wanaotumia kampeni hii kuelezea masaibu yaliyowakuta kupitia mitandaoni na kwenye jamii.

Habari hii kwa haraka sana ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii. Kwenye Facebook, mwandishi Annie Paul alitangaza:

Habari mpya!! Mwendesha mashtaka wa Serikali ametupilia mbali mashtaka yote matatu yaliyokuwa yanamkabili Latoya Nugent chini ya sheria ya makosa ya mtandao!! #Tambourine!!

Twitter nako hapakuwa nyuma:

Mtumiaji wa Twita Rachel Mordecai alichangia:

Nugent siku zote alijitahidi kuwa mkweli dhidi ya makosa ya mashitaka yaliyokuwa yanamkabili, ambayo kwa ujumla yalisomeka “matumizi mabaya ya kompyuta”. Tangu awali, wataalam wengi wa sheria walikuwa na hisia kuwa makosa yake hayakuwa na mshiko kwani sheria imetoa uwanja mpana wa tafsiri pale linapokuja suala la mawasiliano batili au ya kihalifu.

Katika mazingira ya nje ya mtandao wa intaneti, kitendo cha Jeshi la Manyanga cha kuwataja na kuwaaibisha watekelezaji wa unyanyasaji wa kijinsia kupitia kiungo ishara cha #SemaMajinaYao kingaliweza kuchukuliwa kama kitendo cha kuharibu majina ya watu. Hata hivyo, mwaka 2013, Jamaica ilibadilisha mfumo wake wa kushughulika na makosa ya kukashifu na kuyafanya kuwa ya kijamii kuliko makosa ya jinai. Kimsingi, ikiwa mtu atatuhumiwa kwa makosa ya kukashifu nhcini Jamaica, atalazimika kulipa fidia na siyo adhabu ya kufungwa gerezani.

Kama ujumbe ulivyo kwenye Twitter, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa nchi (DPP) alifafanua uamuzi wake wa kuifuta kesi hii:

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.