Ajali ya Basi Yaua Makumi ya Watoto Kaskazini mwa Tanzania

Safari y basi kwenda Arusha, Tanzania. Picha na Jerry Michalski, CC BY-SA 2.0.

Basi lililokuwa limebeba watu 40, wengi wao wakiwa ni wanafunzi wa shule ya msingi na walimu wao, liliangukia mtoni mkoani Arusha, kaskazini mwa Tanzania, na kuua watu wasiopungua 31, kwa mujibu wa taarifa za habari.

Shirika la habari la Associated Press baadae liliripoti kwamba jumla ya watu 35 walikuwa wamepoteza maisha yao, wakiwemo watoto 32, kwa mujibu wa taarifa za maafisa wa polisi.

Wanafunzi hao walikuwa kwenye safari ya kimasomo, wakitembelea shule moja wilayani Karatu mkoani humo, na baadae walikuwa na ratiba ya kutembelea moja wapo ya maajabu ya asili ya dunia, hifadhi ya Ngorongoro, kwa mujibu wa taarifa ya gazeti la Daily News.

Hawakuweza kufanikiwa. Mashuhuda wa tukio hilo wanasimulia habari za kutisha. Basi lilipopita kijiji cha Rhotia, likateremka kwa kasi kwenye eneo linaloitwa ‘Kwa-Karani’, mashuhuda waliona gari likipaa angani na hatimaye kuangukia kwenye Mto Marera, Karatu, kwa mujibu wa gazeti la Daily News. Mitandao ya kijamii ilisambaza picha za gazri hilo likiwa limeharibika vibaya.

Huzuni kwa watoto zaidi ya 30 kusemekana wamepoteza maisha yao kwenye ajali ya barabarani

“Watoto wengi, wengi wa shule wamepoteza maisha,” Theresia Mahongo, Mkuu wa Wilaya ya Karatu, aliliambia gazeti la The Citizen.

Rais John Magufuli alisema “amestushwa” na “kusikitishwa” na habari hizo. Ajali imezima ndoto za watoto hao waliokuwa wakijiandaa kulitumikia taifa lao, alisema kwenye taarifa yake kwa vyombo ya habari:

“Muhimu kwa sasa tuwaombee marehemu wote wapumzishwe mahali pema, majeruhi wapone haraka na wote walioguswa na msiba huu wawe na moyo wa subira, ustahimilivu na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu” Amesema Mhe. Rais Magufuli.

Kulikuwa na taarifa kwamba rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, alikuwa pia ametuma salamu za rambirambi kwa wale walioguswa na ajali hiyo:

Rais Kenyatta ameomba watu watulie kwa muda kuwakumbuka wanafunzi 30 waliopoteza maisha yao kwenye ajali ya barabarani nchini Tanzania, na kutuma rambirambi zake

Watumiaji wengi wa mtandao walionesha masikitiko yao kwenye mtandao wa Twita:

Inasikitisha kusikia taarifa za ajali ya basi nchini Tanzania iliyoua walimu na wanafunzi

Tanzania ni moja wapo ya nchi zenye idadi kubwa ya vifo vinavyotokana na ajali za barabarani barani Afrika. kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2015 iliyoandaliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu usalama barabarani:

Mwaka 2015, takribani watu 3,6000 walipoteza maisha yao kwa sababu ya ajali za barabarani, ikiwa imepungua kidogo ikilinganishwa na mwaka mmoja kabla, ambapo zaidi ya watu 3,900 waliripotiwa.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.