Wito wa Kimataifa wa Kudai Haki Wawaunganisha Wachoraji Nchini Guatemala

Indira Jarisa Pelicó Orellana, mmoja wa waa wahanga wa mauaji ya halaiki ya “Hogar Seguro”, mauti yalimkuta akiwa na umri wa miaka 17. Picha imechorwa na mchoraji kutoka Mexico, Claudia Navarro. Imetumiwa kwa ruhusa.

Siku ya Wanawake Duniani ya Machi 2017  ilibakiwa kuwa siku mbaya sana nchini Guatemala mara baada ya wasichana 41 kuchomwa moto hadi kufa kwenye nyumba ya kulelea watoto inayomilikiwa na serikali iliyopo nje kidogo ya jiji la Guatemala. burned to death in a blaze at a state-run home for children on the outskirts of Guatemala City. Mara baada ya kufungiwa kwenye mabweni kwa lengo la kuziua wasitoroke kwa sababu ya kukwepa vitendo vya udhalilishaji , baadhi ya wasichana inasemekana waliwasha moto kwa lengo la kuwashinikiza walinzi wafungue milango, na hata hivyo, walinzi hao waligoma kuifungua.

Makosa mengi yanayochunguzwa kwenye makazi hayo ni pamoja na uteswaji na adhabu kali. Ukweli unabaki kuwa, wanawake hawac wachanga walikuwa na umri mdogo sana kuwekwa chini ya uangalizi wa serikali. Miezi miwili mara baada ya Raia wa Guatemala kulibatiza tukio hilo jina la Hogar Seguro (Makazi Salama) ya halaiki, mamlaka za serikali zinaonekana kuchukua hatua taratibu na kwa usiri kuwawajibisha waliohusika pamoja na kufidia wahanga pamoja na familia za wahanga.

Tukio hili lilikuwa sehemu ya kuamshwa kwa ari ya baadhi ya asasi za kiraia nchini Guatemala ambazo manamo Machi 15 zilianzisha kampeni ya Kimataifa kwa kutumia kiungo habari #NosDuelen56 (“tuna maumivu ya 56 [wasichana]”). Washiriki wanasambaza picha 56, kila moja ikiwa ama ni ya msichana aliyeuawa au aliyejeruhiwa kwenye moto, michoro iliyoandaliwa na wachoraji kutoka maeneo mbalimbali duniani kwa lengo la kushinikiza serikali ya Guatemala kuchukua hatua za haraka.

Picha: Jina lako linaniuma ndani kabisa ya moyo wangu.

Ujumbe wa Twitter: Yohana Desiré Cuy Urízar alikuwa na umri wa miaka 15 wakati mauaji ya halaiki ya Hogar Seguro yalipotokea. Ufafanuzi na Baku Estrada – Guatemala #NosDuelen56

Picha: #NosDuelen56: Kampeni ya Kimataifa kwa ajili ya Wasichana hawa

Ujumbe wa Twitter: Zaidi ya vyanzo vya habari 68 tofauti vya kidigitali, redio na vituo vya televisheni vimeungana kwenye Kampeni ya Kimataifa ya kwa ajili ya wasichana hawa.

wachoraji 56 kutoka nchi 6 walishiriki kwenye [Kampeni ya Kimataifa] #NosDuelen56. Walitolea ufafanuzi wa nyuso za wasichana wa Guatemala.

Picha zote zinaweza kupatika na kusambazwa kutoka Flickr, Instagram na Facebook. Mashirika kadhaa yanaunga mkono kampeni ya kushinikiza mamlaka kuchukua hatua, yakiongozwa na shirika la moja la habari la Guatemala Prensa Comunitaria (“Chombo cha habari cha Jamii”) na kusambazwa kwa mara moja kwenye vyombo vya habari 50 na maelfu ya mitandao ya kijamii. Mtu yeyote anaruhusiwa kusambaza picha, kutengeneza nakala ngumu au hata kuzitumia kwenye maandamano yanayolenga kudai haki. Katika ukurasa wao kwenye tovuti ya Medium, Prensa Comunitaria  ilifafanua:

#NosDuelen56 es un grito por la justicia desde el arte, el periodismo, el medioactivismo y los feminismos. Es un ejercicio de memoria colectiva y de dignificación por las 56 niñas que fueron encerradas y quemadas en un hogar estatal en Guatemala el pasado 8 de marzo del presente año. De ellas, 41 murieron como resultado de este crimen femicida y 15 están con heridas de gravedad.

#NosDuelen56 ni kilio cha kudai haki kuptia sanaa, uanahabari, uanaharakati wa mtandaoni na haki za wakawake. Hili ni tukio la pamoja la kumbukumbu ya utu wa wasichana 56 waliokuwa wamefungiwa ndani na kisha kuchomwa moto kwenye nyumba ya makazi inayoangaliwa na serikali nje kidogo ya jiji la Guatemala mnamo Machi 8 mwaka huu [2017]. Miongoni mwa wasichana hawa, 41 walifariki kufuatia tukio hili la mauaji ya kijinsia na 15 wakiachwa na majeraha mabaya sana.

Guatemala inachipukia kwa kuwa na kiwango kikubwa cha mauaji ya wanawake yanayotokana na utofauti wa kijinsia pamoja na ukatili dhidi ya wanawake — wanawake 6,000 wameshakabiliwa na matukio ya kuteswa, ukeketwaji au kuuawa tangu mwaka 2000. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na kundi la utetezi lilanofahamika kama  Wanawake kwa Haki, Elimu na Kujitambua, kwa wastani, mwanamke mmoja ama wawili huuawa kila siku.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.