Idadi Kubwa ya Raia Nchini Brazil Waungana na Kufanya Mgomo wa Kitaifa.

Makutano makubwa zaidi yalikuwa huko jijini Largo da Batata katikati ya mji mdogo wa São Paulo. Picha na: Ricardo Stuckert, imechapwa kwa ruhusa maalum.

Mamilioni ya wafanyakazi nchini Brazili wako katika mgomol kupinga mageuzi  yaliyowekwa kuwadidimiza sambamba na sheria mpya za pensheni zilizochapishwa na serikali ya kihafidhina ya Michel Temer, ambaye alichukua nafasi ya Dilma Rousseff kama Raisi ya nchi hiyo mwaka mmoja uliopita baada ya utata wa mashtaka ya Raisi huyo mstaafu.

Usafiri wa umma umesitishwa kwa sehemu kwenye baadhi ya miji mingi mikuu, ukiwemo mji mkuu wa nchi hiyo, São Paulo. Wafanyakzi wa Benki, wafanyakazi katik viwanda vya mafuta, walimu na watumishi wa umma ni miongoni ya watu waliogoma kufanya kazi kwa muda upatao masaa 24 sasa, kuanzia usiku wa manane siku ya Ijumaa, mnamo Aprili 28. Wakiongozwa na mwanaharakati mmoja wa kijamii pamoja na waratibu wa biashara, ambao pia hawajaridhia mabadiliko hayo kwa umma.

Tofauti na upinzani uliowahi kutokea nchini hapo  Brazili miaka mitatu iliyopita, maandamano haya pia yanaendelea kwenye miji midogo na miji mikubwa’ kwenye vitongoji vya masikini. Waandamanaji wamezuia baadhi ya miundombinu  muhimu zinazoelekea miji mikuu  kama barabara, madaraja, viwanja vya ndege na stendi za mabasi mapema alfajiri ya leo. Wananchi wengi wameripoti siku ya leo iko kama mwishoni mwa wiki au mapumziko ya kitaifa.

Kwa mara ya mwisho Brazili kushuhudia maandamano makubwa namna hii ilikuwa mnamo mwaka 1996 pale ambapo serikali ya Nchi hiyo ilikuwa chini ya  Raisi mwingine aliyeleta kivumbi nchini hapo. Kwenye ukurasa wa Twitter, hashtags zilikuwa hivi #GreveGeral #BrasilEmGreve siku nzima ya Ijumaa.

Waandamanaji wa Belo Horizonte, Jiji la Nne kwa ukubwa huko Brazili. Pich na: Mídia Ninja CC BY-SA 2.0

Wiki iliyopita, Katika chemba ya Manaibu  walipitisha mageuzi hayo ya mfumo mzima wa wafanyakazi kwamba muda wa kufanya kazi umeongezeka kutoka masaa 44 kufikia masaa 48 , kutoa adhabu kwa makampuni yanayofukuza waajiri, hali iliyopelekea waajiriwa hao kutowashtaki waajiri wao.

Muswada ni sehemu ya mfululizo wa mageuzi hayo iliyoshinikizwa kwa haraka na Temer, ambaye hufurahiashwa na wingi wabunge walioko upande wake , pia msaada anaopata sekta ya biashara nchini hapo, bila kujali kuzama kwa umaarufu wake wa kisiasa. Orodha ya wapiga kura iliyotolewa wiki iliyopita na Ipsos  imeweka idhini yake binafsi katika faranga ya asilimia 4. Miswada mingine ilipitishwa na kuwa sheria mwaka jana ilkiwemo kufungia matumizi ya umma  na sheria inayoinua vizuizi kwenye vyanzo vya nje. Katika mjuma yajayo, mkutano unatarajiwa kupiga kura juu ya mageuzi ya taratibu za pensheni.

Serikali insema kwamba mageuzi haya ni muhimu kwa nchi ya Brazili kukaunta nakisi  za makusanyiko ya wabrazili na yalitangazwa kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwaka  2015 na chama kimoja cha siasa kwa jina PMDB katika makabrasha yenye kichwa cha habari “Bridge to the Future.” yaani “Daraja la Baadae” Mpango huu ulitolewa kabla chama hakijamaliza muungano wake kwa kipindi cha miaka 12 na chama cha wafanyakazi — Kulazimika kuvunjika kwa muungano huo kulisababisha mkutano kumshtaki  Dilma Rousseff easily kirahisi mnamo April 2016. Rousseff alichaguliwa kwa kura zilizokadiriwa kwa asilimia 54 ya wapiga kura wote  October 2014 na jukwaa la tofauti, lililokuja na maswali kuhusu uhalali wa mageuzi mapya ya serikali.

Skendo ya rusha ambayo haikuweza kukwepeka, na madokezo yanayohusisha baadhi ya viongozi wa vyama vikubwa akiwemo Temer mwenyewe, imeongeza hali ya kutoridhika kwa umma na kuiweka nchi katika hali ya sintofahamu mpaka utakapofanyika uchaguzi mkuu mwingine mnamo 2018. Ambapo ni dhahiri kwamba Temer hataruhusiwa kujihusisha katika uchaguzi huu, hii ni kutokana na hatia iliyomkumba ,kuvunja sheria za uchaguzi mwaka 2014, kuongoza wakosoaji kuweka wazi that kwamba hivi sasa hayupo kwenye orodha ya wapiga kura taraji, kama anavyoshinikiza umaarufu wa sera za taifa.

Kielelezo cha yanayojiri katika mji wa São Paulo ukanda wa Kusini mapema asubuhi ya leo. Picha na: Mídia Ninja CC BY-SA 2.0

Wengi hawajapata neema ya kugoma hivi leo. Vikundi vya kuhifadhiana kama Movimento Brasil Livre pamoja na Vem pra Rua, ambavyo vilikuwa mstari wa mbele kushtaki upinzani mwaka 2015 hadi 2016 na kukubaliana ma mageuzi,wanasema maandamo ni sehemu tu katika jukwaa la siasa  kwa vyama vya wafanyakzi. Wote wameanza kampeni kwenye mitandao ya kijamii kuita watu na kupata mistari ya kuongea, wkati wa kampeni, Ambayo kwa ujumla inapelekea kuongezeka kwa fujo kwenye maeneo matupu, wamawalaani waandamanaji  “magaidi.”

Muandamanaji wa São Paulo. Picha: Mídia Ninja CC BY-SA 2.0

Polisi wametawanya baadhi ya makusanyiko makubwa wakitumia mabomu ya machozi na  risasi za mpira, wakiacha makusanyiko mengne bila kuwagusa. Huko São Paulo, polisi wamewazuia wanaharakati 16 kutoka kitengo cha Makazi, kinatetea swala zima la Makazi na ambacho kimefanya mambo kwa kiwango kikubwa nchini hapo Brazili, zimeripotiwa kuwashutumu kwa “chama jinai.”

Huko Rio de Janeiro polisi walitawanya mkusanyiko mwingine mkubwa wa watu jioni ya jana.

Wakati waandamanaji wengi kusambazwa, makusanyiko makubwa zaidi yalikuwa siku ya Ijumaa jioni katika sehemu  ua biashara mjini São Paulo na waandamanaji walikuja karibu na myumba ya Michel Temer.

Maandamano katika mji wa Salvador. Picha imepigwa na Mídia Ninja CC BY-SA 2.0

Maandamano madogo kuwaunga mkono waandamanaji wa Kibrazili yalitokea katika baadhi ya miji mikuu huko  Europe c, ikiwemo Berlin.

‘Maandamano ya ughaibuni huko Berlini kuunga mkono waandamanaji nchini Brazili #brasilemgreve pic.twitter.com/6ATXjS6SJN

— Luiza Prado (@luizaprado) April 28, 2017

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.