· Februari, 2013

Habari kuhusu Uandishi wa Habari za Kiraia kutoka Februari, 2013

Mgomo wa Nchi Nzima Wamshitua Rais wa Malawi

Rais wa Malawi Joyce Banda atupilia mbali shinikizo la kujiuzulu mara baada ya mamia ya maelfu ya wafanyakazi wa umma kuandamana kwa wiki mbili kuishinikiza serikali kuongeza mishahara, hali iliyopelekea kufungwa kwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Malawi na kusababisha hali ya taharuki mahospitalini na mashuleni.

28 Februari 2013

Uhuru wa Vyombo vya Habari Nchini Myanmar Bado ni Giza

Uamuzi wa Myanmar wa kuivunja bodi katili ya ukaguzi ilisifiwa na makundi mbalimbali ya watu kama njia ya kuelekea kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari nchini humo. Lakini, waangalizi wa uhuru wa vyombo vya habari waliainisha vitisho na mashambulio wanayokabiliana nayo waandishi wa habari wanaoishi nchini Myanmar.

25 Februari 2013

Bangladeshi: Raia Wakutana Kudai Haki Itendeke

Kidogo kidogo, makutano ya Shahbag katika mji mkuu wa Bangladesh, Dhaka yamefurika watu wenye lengo la kutaka haki kufuatia ukatili uliofanywa mnamo mwaka 1971 wakati wa harakati za vita vya kutafuta uhuru pamoja na kudai hukumu ya kifo kwa wahalifu wa vita.Drop by drop, the Shahbag intersection in Bangladesh's capital city Dhaka has become an ocean of people, demanding justice for the atrocities committed during the country's 1971 liberation war and death penalty for war criminals.

17 Februari 2013

Hali ya Hatari kwa Watoto nchini Syria: Namna Utakavyo Saidia.

Hadi sasa,inakadiriwa watoto 4,355 wameshauawa katika mgogoro unaoendelea hivi sasa nchini Syria. Mapema wiki hii, tulitoa taarifa juu ya madhila wanayokabiliana nayo watoto wa Syria kufuatia vita hii inayoisambaratisha nchi yao vipande vipande. Leo tunaangalia namna ambavyo watu wanaweza kusaidia kukabiliana na baadhi ya changamoto wanazokumbana nazo.

12 Februari 2013