Bangladeshi: Raia Wakutana Kudai Haki Itendeke

Kidogo kidogo, makutano ya Shahbag katika mji mkuu wa Bangladesh, Dhaka umefurika watu wenye lengo la kutaka haki sawa kufuatia ukatili uliofanywa mwaka 1971 wakati wa harakati za vita vya kudai uhuru pamoja na hukumu ya kifo kwa wahalifu wa vita.

Inakadiriwa kuwa zaidi ya watu 500,000 wamekusanyika huko Shahbag.

Siku kumi zilizopita, Wanablogu pamoja na Mtandao wa Wanaharakati wa Mtandaoni (BOAN), waliitisha maanamano mara baada ya katibu mkuu wa Chama cha Kiislam cha Bangladeshi Jamaat-e-Islami Abdul Quader Mollah kupatikana na makosa ya kivita aliyoyafanya mwaka 1971. Alihukumiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai mnamo tarehe 5 Februari 2013 kutumikia kifungo cha maisha akiwa gerezani kwa makosa 334 ya mauaji, kubaka pamoja na uchomaji moto wa vitu mbalimbali.

Kwa kuwa sheria ya Bangladeshi inaruhusu mtu kunyongwa hadi kufa kwa makosa ya ukatili, watu wengi walitegemea kuwa Quader Mollah angehukumiwa kunyongwa hadi kufa. Kwa kuwa hili halikutokea, watu waliamua kuingia mitaani pamoja na Facebook ili kupinga hatua hiyo.

Mshairi maarufu na Profesa katika Chuo Kikuu cha Jahangirnagar, Khaled Hossain anategemea kuwa harakati za Shahbag zitakuwa na mafanikio. Katika ukurasa wake wa Facebook anaandika kuwa:

লোভ থেকে বা লাভের আশা থেকে উত্থিত নয় এ অভিনব চৈতন্যের জোয়ার। সমবায়ী শুভচেতনার এ এক অভাবিতপূর্ব নান্দনিক বিস্ফোরণ। বিজয় ছাড়া আমাদের আর কোনো প্রাপ্য নেই।

Mwamko huu sio kwamba unatokana na tamaa za kutaka utajiri au faida ya vitu. Huu ni muonekano wa matokeo ya mkusanyiko wa mawazo chanya. Hatuna cha kupoteza zaidi ya kupata mafanikio.

Mwanablogu, mwandishi na mwalimu, Moom Rahaman anamtaka kila mmoja kufika katika makutano ya Shahbag:

যে সব তরুণ সুস্থ আছেন, দেশে আছেন, অথচ এখনো শাহবাগে জাননি, তাদেরকে জানাচ্ছি আপনারা ইতিহাস থেকে দূরে আছেন, বর্তমান থেকে দূরে আছেন, ভবিষ্যত থেকে দূরে আছেন। এখনো সময় আছে, আমাদের পাশে এসে দাঁড়ান। এখন যৌবন যার, শাহবাগ যাবার তার শ্রেষ্ঠ সময়।

Vijana walioko jijini na walioshindwa kufika Shahbag, tafadhali tambua kuwa uko mbali sana na historia, uko mbali sana na wakati huu na pia uko mbali sana na wakati ujao. Lakini bado unayo nafasi ya kujiunga nasi. Wale vijana wadogo, huu ni muda muafaka wa kwenda Shahbag.

Tausif Hamim ni kijana akeshaye katika kuunga mkono maandamano. Vaskar Abedin aweka maoni ya Hamim:

নিয়ম করে তিন বেলা শাহবাগ যাই, স্লোগান দেই, ক্লান্ত হয়ে গেলে নখ দিয়ে চুলের খুশকি খুটি, আশে পাশে তাকাই, মুগ্ধ হয়ে দেখি ল্যাম্প পোস্টগুলো এক একটি ফাঁসি কাষ্ঠ, সেই কাষ্ঠে ঝুলছে কাদের মোল্লার প্রতিকৃতি, স্লোগান দেয়া আপুটার সাথে নতুন করে বর্নমালা শিখি- “স” তে সাকা চৌধুরী, তুই রাজাকার, “গ” তে গোলাম আজম, তুই রাজকার। ক্ষুধা পেলে বাসায় আসি, ভাত খাই, তারপর আবার শাহবাগ যাই, বিকাল গড়িয়ে সন্ধ্যা নামে, ফাঁসির স্লোগান তীব্র হয়, সন্ধ্যা নামলে মিছিলের উপরে মশাল জ্বলে সেই মশালের আলোতে পাপমুক্তির গন্ধ থাকে, এখানে সেখানে উল্টে পড়া মশালগুলো তুলে নিয়ে আমি এক জায়গায় জড়ো করি, পরে থাকা কেরোসিনের উপর ছড়িয়ে দেই খবরের কাগজ, আবার ক্লান্ত হই, ১০ টাকার বাদাম খাই, মোমবাতির আগুনে পোড়াই বাদামের খোসাগুলো।…

Ninafik aShahbag mara tatu kwa siku, ninatamka kwa sauti kubwa kauli mbiu mbalimbali, ninapochoka, huwa ninakuna kichwa changu, ninatazama pande zote, ninaangalia kwa mshangao kuwa, milingoti ya taa imekuwa milingoti ya kunyongea watu. Kikaragosi cha mfano wa Quader Mollah kinaning’inia kwenye mlingoti huo. Ninajifunza maneno mapya- S ikisimama badala ya Saka Chowdhury, wewe ni Razakar, G badala ya Golam Azam, wewe ni Razakar. Ninapohisi njaa, huwa ninarudi nyumbani, ninakula chakula cha mchana na kurudi tena Shahbag. Jioni inapofika, kauli mbiu zinazidi kuongezeka, kadri giza linapozidi kuingia, mienge inatoa harufu mbaya kana kwamba ni adhabu, ninakusanya mienge yote iliyokwisha tumika, na kuweka makaratasi kwenye mafuta ya taa yaliyomwagika chini, ninapokuwa nimechoka zaidi, ninakula korosho na kuchoma maganda ya karanga kwa kutumia mishumaa inayowaka.

In the Picture Lucky Akter shouting slogans. Image by Firoz Ahmed

Lucky Akter akitamka kwa sauti kubwa kauli mbiu mbalimbali. Picha na Firoz Ahmed. Haki miliki Demotix (11/2/2013)

Baadhi ya vituo vya televisheni vinaonesaha vipindi kuhusiana na maandamano haya yanayoendelea kushika kasi. Kutokana na matangazo haya, Lucky Akter, mwandamanaji aliye katika mstari wa mbele kabisa amekuwa maarufu kutokana na kauli mbiu zake motomoto. Uingereza-Bangladeshi Morshed Akhter anaandika:

আজ থেকে ‘লাকী আখতার’ নামের মেয়েটি আমার বোন। আর এভাবেই ‘লাকী’-রা আমাদের বোন হয়ে যায়, হয়ে যায় ‘আত্মার আত্মীয়'। অফুরান ভালবাসা তোমাদের জন্য।

Kuanzia leo Lucky Akter ni dada yangu. Na kwa namna hii, Lucky Akters amekuwa dada yetu, “ndugu wa karibu”. Ninakupenda sana.

Shimul Bashar, mwandisshi wa habari wa kituo cha televisheni cha kujitegemea ana mategemeo kakubwa kufuatia #maaandamano ya Shahbag

আমি আবার বলছি, শাহবাগের এইসব দিন ইতিহাস হবে। জীবনে এর চেয়ে বড় পাওয়া আমার নেই। মা, আমার চোখে ঘুম আসেনা। আমি শাহবাগের কথা ভাবি। আমার তার মুখ মনে পড়ে।

narudia kusema kuwa, siku hizi za kukusanyika Shahbag zitakuwa ni sehemu ya historia. Sina jambo lolote kubwa katika maisha yangu zaidi ya hili. Mama, siwezi kulala. Ninaendelea tu kufikiri kuhusu Shahbag. Ninazikumbuka tu nyuso za watu.

Watu wengi kutoka katika vyombo vya kufanyia maamuzi waliunga mkono maandamano haya, lakini Dr. Muhammad Yunus aliyetunukiwa tuzo ya Nobeli hadi sasa bado amekaa kimya. Azad Master alitoa taarifa hii:

নন নোবেল বিজয়ী জাফর ইকবাল স্যার আমাগো সাথে তার সহধর্মিণীকে নিয়ে এসে মঞ্চে উঠে তুই রাজাকার বলে স্লোগান দিতে পারেন । কিন্তু নোবেল বিজয়ী ডক্টর ইউণূস সাব রামুর মতো এইবারও মৌন ব্রত পালন করছেন।

Non-Nobel Dr. Zafar Iqbal ambaye hana tuzo ya Nobeli, ameshapanda jukwaani na kusema kwa sauti kubwa kauli mbiu. Lakini Dk. Yunus anakaa kimya hata katika kipindi hiki.

School student are protesting. Image by Zakir Hossain Chowdhury. Copyright Demotix (11/2/2013)

Wanafunzi wa shule wanaandamana. Picha na Zakir Hossain Chowdhury. hakimiliki Demotix (11/2/2013)

Saikat Shuvro Aic anahoji Chama cha Kizalendo cha Bangladeshi (chama kikuu cha upinzani) – kuhusu msimamo wake kuhusiana na maandamano yanayoendelea:

হায় বিএনপি! না আছে গলায় কোনও আওয়াজ, না আছে চোখে কোনও জ্যোতি! ইয়া মাবুদ এলাহী, দলটারে তুমি রক্ষা কর. .

Oh BNP! Hawana sauti, wala hatma ya maandamano haya, au mwono wa mbali! Eeh Mwenyezi Mungu, tafadhali, kisaidie chama hiki.

Wengi wanafikiri kuwa maandamano haya yanaungwa mkono na serikali. Wengine wanafikiri kuwa maandamano haya yanaonesha hali ya kushindwa kwa serikali. Lakini Bijoy Mazumdar haafiki:

রাজনীতির জনতাকে ভুল বুঝবার কোন অবকাশ নেই।
জনতার রাজনীতি মানুষের জন্য। জনতার রাজনীতি অন্যায় , নির্যাতন, শোষণের বিরুদ্ধে। জনতার রাজনীতি ক্ষমতার জন্য নয়, ক্ষমতাকে দুর্নীতিমুক্ত করার জন্য। শাহবাগে যার অন্দোলন করছে, তাদের আন্দোলন কোন দলকে শক্তিশালী করার জন্য করছে না, তাদের এই আন্দোলন ন্যায় প্রতিষ্ঠার আন্দোলন।

এই আন্দোলন বাংলাদেশের তরুণ প্রজন্মের চৈতন্যের ফসল। [..]

কারো কাছে মনে হচ্ছে এই অন্দোলন, শাসক দলের নানাবিধ ব্যর্থতাকে আড়াল করার অপচেষ্টা।

আমার কাছে এর একটা ভিন্ন উত্তর আছে।

এখন থেকে ৪২ বছর আগের অপরাধের শাস্তি দাবী করেছে যে জনতা, সে জনতাই আরেকদিন দেশের সম্পদ লুটপাটের জন্য যারা দায়ী তাদের শাস্তি দাবীতে সোচ্চার হয়ে উঠবে।

এ জনতাই সেই জনতা যারা ১৯৭১-এ উত্তাল হয়ে উঠেছিল, স্বাধীনতাকে ছিনিয়ে এনেছিল, ২০১৩-এ সেই জনতাই আবার সোচ্চার হয়ে উঠেছে, আরেকটি অর্জনের জন্য।

Katika siasa, hakuna kikomo cha kuelewa tofauti kwa kile watu wanachokihitaji. Siasa ya watu ni kwa ajili ya watu. Siasa ya watu ni kinyume na kutokutenda haki, kuwanyima uhuru wa mawazo na kuwakandamiza. Siasa ya watu si kwa ajili ya madaraka, ni kwa ajili ya kuufanya uongozi uondokane na rushwa. Wote wanaoandamana huko Shahbag, hawafanyi hivyo ili kukinyang’anya chama chochote madaraka. Mapambano yao ni kwa ajili ya kuleta haki sawa kwa wote.

Maandamano haya ni ya kukiamsha kizazi cha vijana [..]

Baadhi wanafikiri kwamba maandamano haya ni mkakati wa chama tawala kuficha mapungufu yake katika maeneo mbalimbali.

Nina jibu ambalo ni tofauti.

Wote wanaoungana na kushinikiza upatikanaji wa haki kwa kosa lililodumu kwa miaka 42, siku moja, mkusanyiko huohuo wa watu watapaza sauti zao dhidi ya watu wanaojihusisha na rushwa iliyo kithiri.

Huu ni mkusanyiko ule uliopaza sauti mnamo mwaka 1971 na kutupatia uhuru kamili. Mwaka 2013, kusanyiko la namna hii limeshaibuka, mara hii, kwa dhumuni jingine, kutafuta haki.

Nyimbo, mashairi na maigizo mafupi ya kuchekesha huandaliwa kila siku. Mwimbaji maarufu na mbunge wa Bengali ya Magharibi nchini India Kabir Suman ameonesha kuunga mkono katika maandamano ya #Shahbag kwa kutunga nyimbo kama vile “ matakwa ya wengi” na” Usiku kucha Shahbag.”

Kila siku, kurasa mpya za facebook zinaanzishwa kuunga mkono na kupinga harakati hizi. Zile zinazounga mkono maandamano haya ni kama harakazi zaShahbag na Eneo la Projonmo na zile zinazopinga maandamano ni Sauti za Wazalendo na Bamboo Castle.

Waandamanaji wameapa kuendelea kukaa Shahbag hadi hapo madai yao yatakapo fanyiwa kazi.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.