Bulgaria: Pamoja na Serikali Kujiuzulu Maandamano Yapamba Moto

Siku ya Jumapili, Februari 24, 2013 makumi ya maelfu ya watu wa Bulgsria waliandamana kupinga rushwa, gharama kubwa za matumizi ya nishati pamoja na umasikini. tens of thousands of Bulgarians protested against corruption, high utility bills and poverty. Jiji la Varna lililo pwani ya Bulgaria lilitangazwa kuwa ndilo jiji la maandamano: zaidi ya watu 40,000 walijitokeza katika jiji hilo siku ya jumapili kwa ajili ya maandamano hayo ya jumapili. Takribani watu 15,000 walijitokeza katika jiji la Plovdiv kwa ajili ya maandamano. Wakati ikiwa ni vigumu sana kujua haswa ni idadi gani ya watu waliojitokeza kwenye maandamano ya Februari 24, vyanzo vya kiuanaharakati vinasema kuwa, walikuwepo watu zaidi ya 200,000 nchini kote.

Huko Sofia, baadhi ya kauli mbiu zilikuwa ni: “Tuuchome moto ukiritimba!”; “watu wa Bulgaria, amkeni! Kwa ajili ya demokrasia ya kweli!”; “Mwisho wa mauzauza, Kila siku ni harakati za kiraia!”; “ Sisi Wabulgaria, Waturuki, Waroma, Waamerika – sote ni raia wa Bulgaria! Lazima tujizatiti kupinga upotoshaji wa kisiasa!”

The Feb. 24 protest in Sofia. Photo by Ruslan Trad.

Maandamano ya Februari 24 huko Sofia. Picha na Ruslan Trad.

Hii hapa ni video ya maandamano ya huko Sofia, iliyoandaliwa na mwandishi wa makala hii:

Maandamano ya Sofia yalienda sambamba na sherehe ya kutwazwa kwa Neofit, askofu mkuu mpya mteule wa kanisa la Orthodox la Bulgaria; jiji lilizizima, hakukuwa na usafiri wa umma, isipokuwa kwa usafiri wa treni wa chini ya ardhi. Dakika chache mara baada ya kutawazwa, Askofu Mkuu Neofit aliahidi kuombea amani na mshikamano kwa ajili ya watu wa Bulgaria. Mshikamanno huu aliouonesha Askofu ulipokewa vizuri na waandamanaji, wakati uungaji mkono huu haukupokewa vizuri na Rais Rosen Pleveliev, aliyekuwa akihutubia umati mkubwa wa watu huko Sofia.

Waandamanaji walivitaka vyama vya siasa kutopotosha au kujihusisha na maandamano.The protesters called political parties not to manipulate or get involved in the protests. Wakati wa maandamano huko Veliko Tarnovo, kuna wakati wawakilishi fulani wa wanasiasa walifukuzwa [bg; video]. Stanislava Stefanova aliandika [bg]:

Hawaelewi kuwa hawana nafasi kwenye maandamano haya???? Hivi inaeleweka vizuri kuwa hatuwahitaji???

Kufuatia kujiuzulu kwa kushtukiza kwa serikali ya Boyko Borisov mnamo Februari 20, kulikokuja mara baada ya maandamano yaliyotanguliawhich came after an earlier protest kuhatarisha amani zaidi, wanaharakati wa harakati za maandamano waliitisha mkutano katika jiji la Sliven na walikubaliana mambo wanayoyahitaji: sio kuliahirisha Bunge; Rais anapaswa kuwateua wataalamu watakaoiunda serikali mpya, badala ya kuifanya kuwa serikali ya mpito, kuandaa mswada wa ushirikishwaji wa wananchi utakaoruhusu uhusika wa asilimia 50 ya raia katika taasisi zote, kurudisha serikalini asilimia 51 ya sekta zote za nishati, kuisimamia kampuni ya Nishati ya Bulgaria (BEH), ili isiikandamize sekta ya nishati; kuitisha mkutano mkuu wa Bunge pamoja na kuandaa mkakati wa kuwarudisha tena wabunge.

Lada Dimitrova aliandika [bg] maoni yake katika kumbukumbu ya picha za maandamano ya Februari 24 kwenye ukurasa wa “Ukinzani” ( “Saprotiva”) (“Resistance”):

Sijali sana ni nani atakuwa kiongozi, jambo la muhimu kwangu ni kuishi kwa amani!

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.