Wananchi wa Costa Rica wametoa maoni kwenye mtandao wa Twita kuhusu tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.6 (Mercalli) lililoikumba nchi hiyo tarehe 5, mwezi wa Septemba, 2012, saa 8:42 za mchana. Mshindo wa tetemeko hilo lililoathiri zaidi sehemu ya Guanacaste, ulifika mpaka kwenye miji ya jirani ya Liberia na San Jose.
Watumiaji wa mtandao wa Twita nao wanaripoti kwamba tetemeko hilo la ardhi lilidumu kwa muda mrefu kiasi. Raia watumiao mtandao wanatumia alama habari za #temblorcr na #terremotocr kujadili tukio hilo.
Kama Ariel Arburola (@arielarburola) [es] alivyotangaza kwenye Twita:
@arielarburola: Casi corro pero me dió tiempo de poner #temblorcr
Taarifa kuhusu madhara ya tetemeko zinaingia, hata kupitia Twita. Sergio Pacheco (@lafoto) [es] aliandika mistari kadhaa kuhusu uharibifu wa nyumba ya dadake mjini Montezuma, karibu na kitovu cha tetemeko hilo:
@lafoto: la casa de mi hermana en Montezuma en Guanacaste con el piso levantado #temblorcr
Baadhi ya mitandao ya simu za mikononi zimezimwa, Cristian Cambronero (@cambronero) [es] anavyoripoti::
@cambronero: Caída la red de Movistar, el ICE funciona parcialmente #terremotocr
Fabián Calvo (@FabianCalvo) [es] akajibu:
@FabianCalvo: @cambronero Acá por el contrario, yo tengo Movistar y puedo llamar a Claro y a líneas fijas del ICE, a los celulares Kolbi no puedo del todo
OVSICORI (Taasisi ya Kosta Rika ya Kuchunguza Volkeno na Mitetemeko ya Ardhi) imeripoti kwamba mwambao wa Rasi ya Nikoya inaweza kuinuka kwa urefu wa mita moja kwa ajili ya mtetemko wa ardhi, El Periódico ya Kosta Rika (@elperiodicocr.com) [es] inaripoti:
@elperiodicocr.com: Terromoto levantó la Penínzula [sic] de Nicoya en por lo menos un metros, dice Marino Protti, del OVSICORI.
Signali hai za idhaa zinasikika kwenye ADNfm radio [es], ambapo watu wanapiga simu kuripoti ukatizaji wa huduma za umeme, kuanguka kwa paa za vigae, na uharibifu, ingawa vifo bado havijaripotiwa.
Tahadhari ya moja kwa moja ya tsunami imetolewa kwenye sehemu ya Pasifiki na Chile pia, lakini Tume ya Kitaifa ya Mambo ya Dharura (CNE) imeibatilisha kwenye ufuko wa Pasifiki wa Costa Rica.
Kupitia Twita na vyombo vya habari, kama vile idhaa ya ADN.fm, raia watumiao mtandao wanawasihi wenye habari kutumia mitandao ya jamii kama Twita kuhabarishana.
Rais wa nchi, Laura Chinchilla (@Laura_Ch) [es] aliondoka ili aende kutafuta habari kutoka kwa Tume ya Kitaifa ya Mambo ya Dharura:
@Laura_Ch: Ante dificultades en el sistema de telecomunicaciones me dirijo a CNE para recibir informe sobre seismo q sacudió al país.