· Agosti, 2010

Habari kuhusu Uandishi wa Habari za Kiraia kutoka Agosti, 2010

Tunisia: Picha ‘Zilizochakachuliwa’ ni Dalili ya Hali Halisi katika Vyombo vya Habari vya Kitaifa

Utumiaji vyombo vya habari vya kitaifa nchini Tunisia kama chombo vya kupigia propaganda ni jambo ambalo limeripotiwa vya kutosha. Ushahidi wa hivi karibuni kabisa wa utumiaji mbaya wa vyombo vya habari umewekwa bayana na wanablogu wa nchi hiyo mnamo tarehe 20 Agosti baada ya magazeti ya Le Temps na Assabah kuchapisha ripoti kuhusu taasisi ya hisani ya Zeitouna kutuma msaada wa kibinadamu wa chakula kwa waathirika wa mafuriko nchini Pakistani.

Malaysia: Je, Uhuru wa Habari Unaelekea Wapi Sasa?

  23 Agosti 2010

Picha uliyonayo ni kwamba Malaysia inaweza kuwa ni moja ya nchi zinazokua haraka kiuchumi katika bara la Asia, lakini je unafahamu kuwa ilikuwa katika nchi tatu za mwisho (nchi ya 131) kwenye masuala ya uhuru wa vyombo vya habari? Je wananchi na vyama vya upinzani vinavyopigana dhidi ya uchujwaji wa habari wanapata ahueni? Tutajua ukweli kwa kuangalia hali ya sasa ya uhuru wa vyombo vya habari nchini Malaysia.