China: Pato la Taifa Linaongezeka, Matumizi Katika Huduma za Jamii je?

Ishara ya kuwa uchumi wa China upo karibu na kuwa wa pili kwa ukubwa duniani imejitokeza leo kutokana na toleo la takwimu za ukuaji (uchumi) za Japani katika robo ya pili ya pili.

Je pesa zote zinakwenda wapi, mwanachama wa jukwaa la uchumi la Sohu BRY anaonekana kuuliza hilo katika makala hii ya wiki iliyopita, “Kwa nini Wachina hujitunzia akiba kiasi hiki wakati wote?”, akianza kwanza kwa kulinganisha mifumo ya huduma za afya ya Australia, Sweden na Thailand na ule wa China:

在我国,虽然正在的推进全民医保制度有助于缓解“看病贵”的问题,但保障之外的余额仍足以让一个家庭变得一无所有甚至负债累累,除非你能保证一辈子不得大病。

Nchini China, wakati mfumo wa bima ya afya kwa wote unaotekelezwa sasa umesaidia kupunguza tatizo la ulanguzi katika huduma za afya, ikiwa tu hautaweza kupata ugonjwa wowote mkubwa wakati wa maisha yako, gharama za malipo zaidi ya bima zinatosha kuiacha familia bila ya chochote, au hata (kuiacha) na deni.

Na gharama ndogo linganifu za elimu ya baada ya sekondari katika nchi kama Uingereza, ufaransa na India:

而在我国,大学学费近20年的时间里上涨了约25倍,而同期城镇居民人均年收入只增长了4倍,大学学费的涨幅几乎10倍于居民收入的增长。一个人本科4年最少花费2.8万元,相当于贫困县一个农民20多年的纯收入,这还没有考虑吃饭、穿衣、医疗等费用。

Nchini China, mafunzo ya chuo kikuu yamepanda kufikia mara 25 ya vile ilivyogharimu chini ya miaka 20 iliyopita, nab ado katika kipindi hicho hicho wastani wa mshahara wa wakazi wa mijini na wale wa Karibu na mijini ilipanda mara nne tu, ikimaanisha kuwa gharama za elimu ya chuo kikuu zinaongezeka kwa kasi mara 10 zaidi ya vipato vya wakazi hao. Miaka minne ya masomo ya shahada, mtu atapaswa kutumia angalau RMB 28,000, ambazo ni sawa na kipato cha miaka ishirini cha mkulima anayetokea katika maeneo yaliyokumbwa na umasikini. Hii haijumuishi gharama nyingine kama vile za chakula, mavazi au huduma za afya.

Akafuatia na hali ya malipo ya taifa ya uzeeni nchini China na kwingine:

蒙古、朝鲜、古巴等实行计划经济的社会主义国家采取的是国家保险型的养老保险制度,国家宪法把以养老为主要内容的社会保障制度确定为国家制度,退休金支出全部由国家和企业承担,个人不交纳养老保险费。我国现阶段,国家机关事业单位实行的是国家保险型的养老保险制度,企业单位实行的是自保公助型的养老保险制度,而占全国人口多数的农民和城镇无业居民(或称灵活就业人员)要么游离于社会养老保险制度之外,要么个人必须承担全部20%的缴费。

如果上述三座大山仍不足以说明中国人爱储蓄的理由,那就加上住房。现在的房价之高足以让一个中等收入的家庭花掉大半辈子的积蓄,或者当一辈子房奴。

中国人爱储蓄是为了明天在使劲榨取今天。不是中国人守财,而是自己给自己在做保险,是想给子孙传下更多的财产。在社会保障体系还不够完善的今天,中国人只有以更忘我的奋斗,来换取一家人和下一代人富足安定。

Nchi za Kisoshalisti zenye uchumi uliopangwa kama vile Mongolia, korea kaskazini na Cuba kila moja inatekeleza mfumo wa pensheni unaotegemea bima ya taifa, mfumo wa malipo ya akiba ya jamii ambao umetengenezwa katika mfumo wa kitaifa kupitia katiba za nchi hizo; gharama za kuritaya zinatolewa na taifa, bila ya anayepokea kulipa ada za pensheni. Nchini China kwa hivi sasa, wafanyakazi wa serikali wanatumia mtindo wa bima ya taifa katika mfumo wa malipo ya uzeeni. Wakulima na wakazi wa mijini wasio na ajira pamoja na wakazi wa vijijini (wakijumuishwa wale ambao hawana ajira za kudumu), ambao ndio wanaounda kundi la walio wengi nchini, ama wanaachwa nje ya mfumo wa malipo ya uzeeni au vinginevyo wanagharamia 20% ya mishahara yao wao wenyewe.

Ikiwa milima hiyo mitatu siyo sababu tosha za kufafanua ni kwa nini Wachina wanapenda sana kutunza akiba, basi unaweza kuongezea (gharama za) nyumba. Bei za nyumba hivi sasa zimepanda kufikia mahali ambapo familia zenye kipato cha kati zinabidi kuchagua ama kutumia zaidi ya nusu ya akiba yao, au kuwa watumwa wa mikopo ya nyumba kwa maisha yao yote.

Sababu inayosababisha Wachina kutunza akinba wakati wote ni kuwa kila kitu kinachominywa leo hutumiwa kesho. Wachina sio watu wanaohodhi pesa, bali ni kwamba wanajiwekea bima, wanajaribu kuwaachia watoto wao kitu. Huku mfumo wa bima wa jamii ukiwa na mapungufu kama ilivyo leo, chaguo pekee la walilo nalo Wachina ni kuhangaika bila kuzijali nafsi zao ili kwamba waweze kuwapa familia zao na vizazi vijavyo raha na uhakika.

Makala inayohusiana: benki zinaelekea kufanya kama ilivyotarajiwa.

(Picha katika makala hii imechukuliwa kutoka katika picha hii ya noti ya RMB 100 iliyopigwa na mtumiaji wa Flickr Comer Zhao)

1 maoni

  • Ni kweli kabisa China imepanda kiuchumi chiasi kwamba inashika nafasi ya pili,kwa upande wangu hili halishangazi kwa sababu ukiwaona wachina namna wanavyotumia nguvu katika kazi zao,utaona kwamba kuongezeka kwa uchumi wao si jambo la leo.Sasa nataka kuwambia waafurika kuiga mfano china na ndipo tutaendelea,tuna lasilimali,madini ya thamani,kwa nini hatuendelei nasi kama Marekani au Uchina? Wanamtandao wenzangu nina blog yangu:www.vickange.blogspot.com,yitembelee uniachie maoni yako kuhusu niliyoandika pale.Enyi ndugu zangu, na Rwanda inazidi kuongozeka kiuchumi na hili ni jambo linalositahili pongezi.Tuache ghasia za kila wakati na tutafutie nchi zetu maendeleo na amaani,ikiwa si hivyo tunapoteza wakati wetu kwa bure.Nawaombea heli na fanaka katika mnayotenda yote.Ahsanteni.

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.