Mashindano ya Video: Intaneti Kama Chombo cha Kueneza Amani

Mfumo wa Intaneti umependekezwa kwa ajili ya kupata Tuzo ya Amani ya Nobel kwa mwaka 2010. Kama sehemu ya mjadala unaoendelea kuhusu mchango wa Intaneti katika jamii nzima ya binadamu, Condé Nast na Google Ireland wameungana na kuandaa mashindano haya ya video ana mshindi atapata fursa ya kusafiri na pia video yao kuoneshwa kupitia MTV ya Italia.

Masharti ya kushiriki kwenye mashindano hayo ni mepesi, ili kuyasoma kiukamilifu fuata kiungo hiki:

Video isiwe ya urefu unaozidi muda wa dakika tano (5) katika ujumla wake; Video inaweza kuwa kwa lugha yoyote lakini itengenezewe tafsiri ya Kiingereza kwa chini; tafsiri hiyo iwe sahihi na inayosomeka vema; video ilenge zaidi kuonesha ubunifu katika kuonyesha namna gani Intaneti inaweza kuwa chombo chenye ufanisi katika kueneza amani kama ilivyoelezwa kwenye Ilani ya Intaneti kama Chombo cha Kueneza Amani(kwa kifupi I4P Manifesto) iliyochapishwa kwenye mkondo huu www.youtube.com/internetforpeace.

Tarehe ya mwisho ya kuwasilisha ni 1 Septemba mwaka huu, hata hivyo, kura na umaarufu wa video zitakazotumwa mtandaoni ni baadhi ya vigezo vitakavyotumika kuamua kumpata mshindi, kwa hiyo, kama hujatuma video yako, ni afadhali ufanye hivyo mapema! Unaweza pia kutazama mkusanyiko wa video zilizokwishatumwa hapa na kupigia kura ile unayoipenda zaidi.

Majaji Gilberto Gil, Yoani Sanchez, Gabriele Salvatores, Ory Okolloh, Ai Wei Wei, Nobuyuki Hayashi (Nobi), Nadine Toukan ndiyo watakochagua video itakayoshinda mashindano haya, na watazingatia viwango vya ubunifu, utaalamu uliotumika, idadi ya kura ilizopata kutoka kwa watu mbalimbali, uasilia katika ubunifu na ni kwa kiwango kipi cha usahihi video hiyo inafasiri ilani ya I4P.

Hapa unaweza kuona video mbili katika zile ambazo tayari zimeingizwa kwenye mashindano:

Kikundi cha vijana wenye umri wa mabarubaru wa Kipalestina na Israeli ambao wamekuwa wakifanya kazi pamoja kwa miaka 3 sasa wakiimba na kuandaa video za muziki unaohamasisha Amani.

Yuri anayetoka Urusi anaandaa video kuhusu fikra gandi za kitaifa na jinsi gani intaneti iinavyosaidia kuondoa fikra hizo na kuonyesha vile watu walivyo kweli.

Kwa hiyo, tazama video ya Ilani ya Intaneti kama Chombo cha Kueneza Amani ili uhamasike kushiriki, tuma video yako na pigia kura video unayoipenda zaidi!

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.