Ufilipino: Maoni ya Wanablog Juu ya Elimu ya Ya afya ya Uzazi

Nyuki akichavusha ua huko Baguio, Philippines – haki miliki Jay Suasin kwenye Flickr (Imetumika kwa ruhusa)

Mwaka huu wa masomo serikali ya Philippines inatekeleza mpango wa elimu ya uzazi kwenye shule za umma unaofadhiliwa na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya watoto na vijana. Elimu hiyo imefanyiwa majaribio katika shule teule nchini kote na itakuwa na mada kama afya ya uzazi, kujikinga na VVU/UKIMWI na Uzazi wa mpango.

Kanisa Katoliki limepinga vikali mpango huo. Na wanablogu wametoa maoni juu ya suala hilo.

Tom Martin anauliza kama elimu ya ngono inafaa kufundishwa “darasani au nyuma ya mti?”

Hakuna mzazi atakayeweza kuwa na udhibiti mahsusi juu ya pahali ambapo mwanae atajifunza kuhusu ngono na jinsi ninavyoona mimi mzazi mwenye busara atapenda mwanae apate elimu hiyo kutoka kwenye shule na kutoka kwa mwalimu aliyefuzu vizuri kuliko kujifunza kuhusu hilo toka kwa watoto wenzie nyuma ta mti.

The Pinoy Catholic anatoa msimamo unaofanana na ule wa viongozi wa kanisa na kwa nguvu zote anapendekeza kuwa elimu ya ngono ibaki kuwa jukumu la wazazi.

A Filipina Mom Blogger anahadharisha kuwa si wazazi wote wanaojua namna ya kuzungumza na watoto wao juu ya masuala ya ngono:

“Hatuwezi kuchukulia kuwa wazazi wote wanajua namna ya kujadili ngono kwa uwazi. Baadhi yao wanaweza kuwa hawana elimu hivyo kushindwa kuelewa muundo na mfumo wa uzazi, na hivyo kushindwa kuelewa juu ya njia asilia za uzazi wa mpango.”

The Catacomb anapendekeza kuwa elimu hii ifundishwe kwa wazazi badala ya watoto.

Kwanini tusiwaache hawa watoto kwanza… Au labda serikali ijaribu kuweka sheria ya kudhibiti malezi, ambayo kwayo ndani yake wazazi wapewe mafunzo endelevu au warsha ambazo zitawawezesha kwa kuwapa elimu inayofaa katika kuwapa watoto wao muongozo mzuri wakati wanakua. Hii itazuia watoto kuwa kwenye nafasi ya kuamsha hisia zao za ngono bali pia itawapa wazazi nafasi ya kuwa karibu na watot wao, kuwa nao kwa muda mwingi, kuwaangalia kwa Karibu kama inavyotakikana, na kukuza upendo…

The x-piles anaamini kuwa wale wanaopinga elimu hiyo wanatakiwa kuvishambulia vyombo vya habari kwanza.

Kanisa linaweza kuwa limekosea kwa kutoangalia ni nini hasa nini chanzo cha kile kinachodaiwa kuwa kizazi cha waliopotoka ki-ngono – vyombo vya habari. Uhalifu na ngono vinaoneshwa wazi kabisa kwenye michezo ya luninga na filamu na hivi vyote vinafonzwa na vijana na watoto pia. Hivi vyote vina uwezo wa kubadili akili inayokua ya vijana, na kuwafikisha kwenye kuchanganyikiwa juu ya lipi ni sahihi na lipi si sahihi.

Wakati huohuo, Quod Dixit Dixit anahoji kinachoisukuma serikali katika kutekeleza mpango huo.

Haipo wazi kwangu iwapo hatua hii ya serikali inapata imetokana na fikra yake kuwa chanzo cha umasikini ni idadi kubwa sana ya watu nchini Ufilipino na hivyo ni lazima kasi ya kuzaliana ipunguzwe (N.B.: Siku zote huwa naamini kuwa msingi mkuu wa umasikini ni ubadhilifu na rushwa pia uharibifu wa mazingira usiodhibitiwa.)

Kundi la wanawake Gabriela linauona mpango huo kama hatua yenye muelekeo sahihi..

Memorandum Namba. 26 ya Idara ya Elimu (DepEd), iliyoruhusu vitini vya kufundishia elimu ya ngono, ingeliweza kuwa hatua chanya, iwapo kitengo hicho kinge endesha mchakato wa kushauriana na wadau mbalimbali kabla ya kuanza kutekeleza mpango huo. Hilo lingehakikisha kwamba mpango huo hautatekelezwa bila kujali, na kwamba misimamo yote imewekwa maanani. Kwa upande wetu, GABRIELA, Chama Cha wanawake Gabriela na SALINLAHI vipo tayari kuwa sehemu ya mchakato wa kushauriana na kutoa ushauri kwa kutumia uzoefu na ujuzi wetu katika elimu ya jinsia na masuala ya kujamiiana kwa wazazi na watoto.

Ducky Paredes, hata hivyo anaamini kuwa, mpango huu umeshafika mwisho kutokana na kuteuliwa kwa Buruda Armin Luistro FSC kuwa Waziri wa Elimu katika utawala mpya wa Aquino.

Je huu ndio mwisho wa ruzuku ya UN kwenye mradi huu? Inawezekana. Hatuwezi kutarajia mtawa wa Kikristu akaruhusu ufundishwaji wa elimu ya ngono kwa watoto wadogo na wanafunzi wa sekondari ukichukulia kuwa wengi katika Kanisa Katoliki wanaamini kuwa masomo ya kuhusiana na ngono na uzazi yataleta mamba zisizotarajiwa kwa wanafunzi.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.