Mimi ni mhitimu wa shahada ya elimu. Naishi mjini Morogoro, nikijishughulisha na shughuli za ujenzi wa taifa letu changa. Napendelea kusoma hasa makala za wanaharakati wa mtandaoni na kuandika makala kila nipatapo fursa ya kufanya hivyo.
Ni mpenda maendeleo wa kweli nikiamini kuwa maendeleo huanza na fikra bora. Natamani kuona siku moja kiswahili kinakuwa moja ya lugha kubwa mtandaoni, na hii ndio sababu nimeamua kuwa mmoja wapo wa wanatimu ya Swahili Lingua. Kwa pamoja tunaweza!
makala mpya zaidi zilizoandikwa na mdoti
Uzbekistan: Mchezo wa Siasa katika Facebook
Facebook inaonekana kuanza kuchukua jukumu muhimu katika siasa za Uzbek. Hata hivyo , facebook ni imekuwa ni zaidi kwa ajili ya michezo na akaunti za kugushi kuliko chombo kuwa chombo cha harakati za kiraia. Ekaterina anaripoti.
Mexico: Wanafunzi Wawili Wauawa Kwenye Maandamano Huko Ayotzinapa
Wanafunzi wawili, Jorge Alexis Herrera Pino na Gabriel Echeverría de Jesús, waliuawa tarehe 12 Desemba 2011, wakati wa maandamano ya wanafunzi wa shule ya vijijini ya Raúl Isidro huko Ayotzinapa, mji mkuu wa Guerrero, Chilpancingo, nchini Mexico. Mitazamo yenye utata kuhusu yalioyotokea imechapishwa mtandanoni.
Uarabuni: Hongera Tunisia!
Human rights activist Moncef Marzouki, 66, has been elected as Tunisia's new interim president today. His appointment, which was followed by a moving acceptance speech, was noted by netizens from across the Arab world, who cheered on Tunisia's progress towards democracy, wishing the same for their countries.
Iran: Yu Wapi Mwanafunzi Mwenzangu?
Several empty chairs in Iran's universities were formerly occupied by students who have now vanished or been expelled. This year Tahkim Vahdat, a leading student protest group, called for an “Empty Seat Campaign” on December 7 to remember the victims of religious and government repression in universities.
Mexico: Mwanamke wa Miaka 20 ni Mkuu Mpya wa Polisi katika Mji wa Kaskazini mwa Mexico
Valles García ni mwanamke aliyeolewa mwenye umri wa miaka 20 anayesoma masomo ya makosa ya jinai na uhalifu; vile vile ni mkuu mpya wa polisi wa Práxedis, Chihuahua, mji uliopo umbali wa kilometa 100 (maili 62) kutoka Ciudad Juárez, mji wenye uhalifu zaidi nchini Mexico.
Watu wa Uruguay Waomboleza Kifo cha Mwanamuziki José Carbajal, ‘El Sabalero’
Mwimbaji na mtunzi José Carbajal, anayejulikana kwa jina la utani kama “el Sabalero,” amefariki kutokana na shambulio la moyo mnamo Oktoba 21 akiwa na umri wa miaka 66. Carbajal anachukuliwa kuwa gwiji na utambulisho wa utamaduni wa Uruguay. Mwaka huu alikuwa akifanya kazi na wasanii wengine katika mradi wa Kompyuta Moja ya Mapajani kwa Kila Mtoto nchini Uruguay Uruguay, Mpango wa Ceibal, ili kutumbuiza kwenye maonyesho kwa ajili ya watoto wa shule nchini kote.
Moroko: Mtoto Mwanablogu Asalimia Ulimwengu
Salma alianza kublogu akiwa na umri wa miaka sita ili kuwasiliana na ndugu na marafiki. Chii ya usimamizi wa wazazi wake, mwanablogu huyu mdogo wa Moroko anapendelea kuandika hadithi fupi fupi na kuielezea dunia matukio anayokumbana nayo kila siku shuleni.
Ufilipino: Maoni ya Wanablog Juu ya Elimu ya Ya afya ya Uzazi
Mwaka huu wa masomo serikali ya Philippines inatekeleza mpango wa elimu ya uzazi kwenye shule za umma unaofadhiliwa na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya watoto na vijana. Na wanablogu wametoa maoni juu ya suala hilo.
Korea Kusini: Maombolezo ya Kitaifa ya Mwanamwali wa Kivietnam
Mwanamwali mdogo wa Kivietnam aliuwawa na mumewe wa Kikorea nchini Korea. Wanablogu wa Korea wanatoa rambirambi zao kwa kifo kibaya cha mke huyo mwenye umri mdogo huku wakiitaka serikali kutokomeza eneo hili lisiloonekana kwa urahisi la haki za binaadamu, linalohusiana na wachumba kutoka nchi za kigeni.
Udhibiti Nchini Singapore
Singapore imesababisha kelele kubwa baada ya kupiga marufuku filamu ya aliyewahi kuwa mfungwa wa kisiasa na kumkamata mtunzi Mwingereza wa kitabu kilichoandiaka kuhusu adhabu ya kifo nchini humo. Wanablogu wanajadili.