Malaysia: Je, Uhuru wa Habari Unaelekea Wapi Sasa?

Je, ni nchi ipi katika orodha hii ambayo imepotea njia? Tanzania, Uganda, Zambia na Malaysia. Sawa, tuchukulie kwamba mimi ni mwandishi mtukutu ambaye niko kama ninataka kukashifu ufahamu wako wa jumla kuhusu nchi mbalimbali unazozijua. Kwa hiyo, Malaysia ni moja ya nchi zenye uchumi mzuri katika eneo la Kusini Mashariki ya Bara Asia, ina miundo mbinu iliyojengeka zaidi, ina kiwango cha chini cha umaskini, aaaah… unaweza kusema kwamba ina demokrasia zaidi pia. Lakini, ama kwa hakika ni nchi iliyopotea njia, maana Malaysia inaangamia tena chini ya Tanzania, Uganda na Zambia hasa katika kushika nafasi gani kwenye masuala ya uhuru wa vyombo vya habari.

Kama matukio ya uhuru wa vyombo vya habari yanavyozidi kujiri nchini Malayasia, kuna masuala 3 yanayojitokeza bayana:

1) Vyama vya siasa vya upinzani vitaongeza upinzani wao kupitia vyombo vya habari vya mtandaoni, baada ya kupewa nafasi finyu katika vyombo vya habari vya magazeti na televisheni.

2) Licha ya kuwepo madai au ushahidi wa kuunga mkono uwepo wa vyombo huru vya habari, bado serikali inaendelea kuwa na mkono wenye nguvu katika udhibiti wa vyombo vya habari hasa kupitia sheria za utoaji habari na upigaji chapa.

3) Uchujaji wa habari hauwezi kuwa na nguvu iwapo mawasiliano ya Intaneti yatabaki bila kuchujwa. Idadi inayokua ya watumiaji wa Intaneti na uandishi ulio huru wa mtandaoni ni mambo yatakayokuwa na athari katika ushawishi wa umma na kuiweka serikali chuni ya shinikizo.

Mapema mwaka huu yalipotoka matokeo ya upimaji uhuru wa vyombo vya habari, wanasiasa wa upinzani walikuwa wa kwanza kutoa maoni yao kupitia tovuti za uenezaji habari za vyama na blogu zao. Ukosoaji wao wa mtandaoni uliongezeka sana hasa baada ya serikali kuchelewesha uamuzi wa kuleta upya majarida ya upinzani, na kufungiwa kwa vibonzo vya kejeli za kisiasa; huku mambo yote hayo mawili yakichochea hali ya kutoridhishwa kwa watu na upekenyuzi kupitia vyombo vya habari vya mtandaoni. Raia mmoja, Lai alijibu akisema:

Sababu iliyotolewa na serikali, amini usiamini, ni kwamba ‘yaliyochapishwa yanaweza kuwafundisha watu kukaidi dhidi ya viongozi na sera za serikali'…Vibonzo (katuni) vinaweza kusababisha watu kuasi? Ala, kumbe! Hii ni silaha mpya iliyogunduliwa, au siyo?

Halafu, jambo la kuvutia, licha ya mkakati wa kutumia vyombo vya habari vya mtandaoni kukosoa uchujaji habari, moja ya majimbo yanayo ongozwa na upande wa upinzani liliamua, kwa hakika, kupeleka bungeni muswada wa sheria ya Uhuru wa Habari ili kuweka wazi taarifa kwa manufaa ya umma kwa kila mtu. Anil alisema wakati akimkaripia mwakilishi wa serikali ya jimbo hilo aliyeukataa muswada huo:

Leo ni siku ya kihistoria katika nchi hasa tunapotaka kuwa na jamii ya watu wanaowajibika zaidi …

Kadiri tovuti za vyombo huru vya habari na vile vya kiraia vinavyozidi kuchapisha taarifa zaidi nchini hapa, Gopal Krishnan alitabiri:

Licha ya kuwepo majibu haya ya kimabavu dhidi ya sauti mbadala, kwa hakika, serikali haina budi kuutambua ubatili (bila kutaja matokeo ya kisiasa) wa kuendelea kubana uwepo wa fursa kwa uandishi wa habari na utoaji maoni ulio huru. Mpaka kufika mwaka 2009, zaidi ya asilimia 65 ya nyumba nchini Malaysia tayari zilikuwa zimeunganishwa na mtandao wa Intaneti. Zaidi ya jambo hili, siyo tu kwamba tumeshuhudia kuchipuka wa vyombo vidogovidogo vya habari vya mtandaoni na vyanzo vikishindana katika kuchukua muda tunaotumia mtandaoni, kumekuwa na mfumuko wa uandishi wa habari wa kiraia wa mtandaoni na vyombo vya habari vya kiraia, ambavyo, vyote kwa pamoja kwa kweli vimeunda ukweli mmoja mpya wa kisiasa nchini.

Hatimaye, uhuru wa vyombo vya habari si kitu ambacho serikali au vyama vya upinzani vinaweza kujiamulia, lakini linahusu raia wanaodai kupata ukweli na waandishi wanaotaka kuripoti kuhusu ukweli. Kama Attan alivyosema:

Kama nilivyosema, hata kuwe na nini, sisi waandishi wa habari ndiyo tutakaopoteza – serikali ya Najib inazidi kuyafungia magazeti, Guan Eng (kiongozi wa chama cha DAP) anayapiga marufuku, huku Anwar akituburuza mahakamani.

5 maoni

 • Uhuru wa vyombo vya habari si swala la Malaysia pekee.Nchini Rwanda,watangazaji mara nyingi hulalamika kuwa wananyanyaswa katika kazi zao za utangazaji habari,lakini kwa upande wangu kama msomi wa utangazaji habari katika chuo kikuu cha Rwanda,naona watu hawajui maana ya FREEDOM OF SPEECH.Badhi yao hufikiri kwamba kusema lolote kwa kutumia njia mbali mbali ndiwo uhuru.La, sikubaliani nao.Kwanza tujue tunaishi katika mazingira gani? Tunataka maendele ya nchi zetu kupitia utangazaji unaoshugurikia maendeleo bila kuchonganisha watu.Mfano nchini Rwanda media zilichangia katika mauaji yaliyoangamiza maisha ya watu zaidi ya miliyoni,basi kweli waandishi habari wapewe nafasi ya kusema lolote watakalo?Simba,lazima watu kwanza maana ya freedom of expression yaani uhuru wa maneno.

 • Ndugu DUSABEMUNGU

  Asante sana kwa hoja zako. Nakubaliana na wewe kwamba ‘freedom of speech’ haina maana ya ‘uhuru wa kuongea lolote na popote’ – kile mtu anachokiongea hakina budi kuwa hoja ya maana (kwa maana ya kwamba mtu anawajibika kwa hicho anachokisema) ambayo anaweza kuisimamia (kwamba iko ndani ya sheria zinazokubalika – kwa kuanzia na natural justice). Asante kwa kusoma makala hapa na kutoa maoni yako. Tuendelee kufanya hivyo. Asante. Simba.

 • A

  Simba, vinawezekana ukanitafutia kazi kama nilivyokuambia najifunza utangazaji habari nataka kuwa mwandishi wa tovuti hiyi au unitafutie kazi nyingine. Anuani yangu ni _angevict69@yahoo.com

 • Ndugu Ange

  Asante kwa maoni yako. Kuhusu kazi katika tovuti hii. Wote wanaofanya kazi katika tovuti hii ni watu wa kujitolea. Kila mmoja pale alipo, popote ulimwenguni, anaandika au anatafsiri kwa kujitolea na kisha kutuma makala hayo kwa mhariri anayesimamia ukurasa fulani, kwa mfano, ukurasa huu wa Kiswahili. Kwa hiyo, ingefaa uwasiliane na mhariri wa ukurasa huu kwa maelekezo zaidi.

  Binafsi, nitafurahi kuanza kusoma kazi ambazo pengine wewe utakuwa umeziandika au kuzitafsiri.

  Nakutakia kazi njema.

  Simba

 • shaban kaluli

  mbona ulaya kiongozi akilalamikiwa kwa tuhuma yoyote ile anajiuzulu bara la africa kuna nini jamani?

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

 • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.