Tunisia: Picha ‘Zilizochakachuliwa’ ni Dalili ya Hali Halisi katika Vyombo vya Habari vya Kitaifa

Utumiaji vyombo vya habari vya kitaifa nchini Tunisia kama chombo vya kupigia propaganda ni jambo ambalo limeripotiwa vya kutosha. Vyombo vya habari vya kiraia vya nchini humo vimekuwa makini katika kuchunguza na kufuatialia matukio mengi tu ambapo taarifa zimepindishwa kwa makusudi huku machapisho ambayo yanaikosoa vikali serikali yakifanyiwa mchujo mkali. Ushahidi wa hivi karibuni kabisa wa utumiaji mbaya wa vyombo vya habari umewekwa bayana na wanablogu wa nchi hiyo mnamo tarehe 20 Agosti baada ya gazeti la Le Temps [fr] ambalo huchapishwa pia kwa Kiarabu kama Assabah kuchapisha ripoti kuhusu taasisi ya hisani ya Zeitouna kutuma msaada wa kibinadamu wa chakula kwa waathirika wa mafuriko nchini Pakistani. Ili kuonyesha vielelezo katika ripoti hiyo na ushiriki wa mfanyabiashara mmoja, Sakhr El Matri, ambaye pia ni mkwe wa rais, akishiriki katika mchakato huo, Le Temps lilichapisha picha ikimwonyesha Sakhr El Matri akikagua shehena ya msaada kabla haujapakiwa kwenye ndege:

Picha iliyochapishwa kwenye gazeti la Le Temps ikionyesha picha ‘iliyochakachuliwa’ miongoni mwa picha zilizo kwenye tovuti ya Nawaat.org

Blogu ya jamii ya Nawaat inaelezea viashirio vilivyo kwenye picha hizo vinavyoonyesha kwamba picha hizo zimechezewa [fr]:

Il ne faut pas être un expert pour déceler au premier coup d’œil que la photo a été “retouchée” et que le gendre du président a “atterri” dans cette image par le biais d’un grossier copier-coller. En plus de l’exposition et du sens des ombres qui ne sont pas raccord avec l’exposition générale de la photo, on peut parfaitement déceler la manche de Sakhr El Matri qui cache une partie du coude de l’homme avec la chemise bleue alors que ce dernier est au premier plan !

Nawaat inaeleza kwamba inafurahisha (kwa maana ya kukebehi) kuona kwamba walau toleo la Kiarabu la gazeti hilo lilifanya kazi maridadi zaidi katika kuchezea picha hizo:

Assabah, la version arabe du quotidien, a publié la même photo mais avec un bidouillage légèrement amélioré mais qui reste tout de même parfaitement visible. Quand on agrandi à l’endroit de l’anomalie de la première photo on voit que le bras du mécène passe derrière le coude de l’homme en chemise bleue, comme le voudraient les lois de l’optique

Assabah, ambalo ni toleo la Kiarabu la gazeti hilo, nalo lilichapisha picha hiyo hiyo lakini ikiwa imechezewa kwa kutumia programu ya photoshop kwa umakini zaidi kidogo ingawa bado ilikuwa rahisi kuona uchezewaji huo. Mtu anapokuza zaidi eneo tata la picha hiyo, anaweza kuona kwamba mkono wa kulia sasa unakuwa nyuma ya kiwiko cha mtu aliyevaa shati la buluu, ambalo ni jambo lililo sawa na utaratibu wa kawaida wa jicho kuona

Picha ile ile iliyochapishwa kwenye Assabah huku ikiwa imechezewa tofauti kama ilivyotumwa na Nawaat.org

Ukweli ni kwamba picha zilizochezewa ziliumbuliwa mtandaoni uliwafikia wahariri kwani kwa haraka picha hizo ziliondolewa na nyingine kuwekwa badala yake katika toleo la mtandaoni la gazeti hilo. Picha ya video iliyotumwa kwenye Facebook ilimwonyesha Sakhr El Matri akikagua ndege yenye msaada wa kibinadamu, hata hivyo, ni vigumu kueleza kama video ilichukuliwa kabla au baada ya picha za gazetini kuchapishwa. Ni jambo la kustaajabisha kwamba picha zilizochakachuliwa zinatumika katika magazeti makubwa mawili ya hadhi ya kitaifa tena hovyo hovyo namna hiyo huku kumbe picha halisi zingeweza kuchukuliwa kutoka katika picha ya video. Ikumbukwe pia kwamba Sakhr El Matri anahusika moja kwa moja katika uongozi wa magazeti yote hayo mawili. Wanablogu wa Tunisia pia wamekuwa wakijiuliza iweje Sakhr El Matri, ambaye ni raia wa kawaida, aruhusiwe kufika katika eneo zinakotua na kupaa ndege katika kile kilichoonekana kama kiwanja cha ndege kilicho katika kambi ya kijeshi. Mtumiaji wa Twita wa Tunisia Lilopatra vilevile anajiuliza je ilikuwa ni ndege ya aina gani ambayo taasisi ya hisani ya Zeitouna ilitumia kusafirisha msaada huo wa kibinadamu wa chakula kwenda Pakistani. Anaongeza:

Si on se met dans la position du protecteur à chaque fois,cela retardera la maturité & la capacité de prise de décision du citoyen.#Tunisie

Kama wakati wote tukitazama mambo kwa jicho la mtu aliye juu, basi mchakato wa kukomaa na uwezowa raia wa kufanya uchaguzi utapunguzwa kasi sana. #Tunisia

Kwa bahati mbaya, picha hizi zilizochakachuliwa ni dalili tu ya taarifa nyingine nyingi za ‘kutengeneza’ nchini Tunisia. Kwa mfano, mwaka 2009, shirika la habari la Tunis Afrique Press (TAP) ) liliripoti kwamba Tunisia ilishika nafasi ya332 kati ya nchi 165 katika kipimo cha utulivu wa kisiasa kwa mujibu wa utaifiti ulioendeshwa na The Economist Intelligence Unit (Kitengo cha Upelelezi cha The Economist). Tatizo lililopo ni kwamba kipimo hicho kwa kweli kilionyesha kwamba Tunisia ilishika nafasi ya 134 yaani nafasi mia moja chini ya hiyo iliyochapishwa katika utangulizi wa makala.

MAENDELEO MAPYA: Ni muhimu kuweka wazi, kama msomaji alivyoonyesha, kwamba orodha hiyo inaziweka nchi dhaifu zaidi kwanza. Kwa hiyo ni sahihi kusema kwamba Tunisia ni nchi ya 32 kati ya zile zilizoimarika kisiasa. Matumizi ya orodha inayoanzia mwisho kama ilivyoelezwa na EIU inafafanuliwa naNawaat kama ifuatavyo:

Bien que…renversante, cette « interprétation » de l’index est surement due à « un souci de clarté » de la part de la TAP. On les comprend. Parler « d’instabilité » dans le pays de « la sécurité et de la stabilité », selon la formule officielle, risque de… « déstabiliser » le lecteur

Wakati ambapo [orodha] hiyo iko… “juu chini”, jinsi TAP ilivyowakilisha orodha kwa mtindo huo ni kwa ajili ya “kuweka wazi” na hivyo inaeleweka. Baada ya yote, kuongelea suala la nchi kuyumbayumba kama nchi hiyo inavyojulikana, na kuelezwa na maofisa wa serikali, usalama na uimara wa nchi unaweza… “kumyumbisha” msomaji

Taswira ya Matokeo ya Kipimo cha Utulivu wa Kisiasa kwa mujibu wa EIU kama ilivyopatikana kutoka Nawaat.org

Mwaka 2007, taasisi hiyo hiyo ya habari, ilipatwa na hatia ya kutia chumvi taarifa [fr] iliyodai kwamba gazeti la International Herald Tribune lilichapisha ripoti ya ukurasa mzima kuhusu mfumo wa elimu wa Tunisia, zikiwemo makala mbili kuhusu namna serikali inavyojitahidi kuwa na mfumo bora wa elimu kwa ajili ya raia wake na umuhimu wa elimu katika maendeleo ya taifa. Hata hivyo, waliacha kipengele muhimu, walisahau kutaja kwamba hakukuwahi kuwepo na hizo makala katika gazeti hilo la IHT upande wa habari bali kulikuwa na tangazo lililojaza ukurasa mzima katika sehemu ya matangazo ya kulipiwa [fr].
Makala halisi za TAP kuhusu matokeo ya Kipimo cha Utulivu wa Kisiasa na ripoti ya IHT hazipo tena kwenye mtandao.
Tunisia mara nyingi imekuwa ikisifiwa kwa kuwa na uchumi motomoto ulio huru na unaolenga kusafirisha nje ya nchi bidhaa wakati huo huo ikikosolewa vibaya sana kwa mfumo wake wa siasa za kiimla. Matokeo ya Kipimo cha Kiwango cha Demokrasia katika gazeti la The Economist la mwaka 2008Tunisia iliangukia katika kundi la nchi zenye utawala wa kiimla na ilishika nafasi ya 141 kati ya nchi 167 ambako utafiti ulifanyika.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.