Habari kuhusu Uandishi wa Habari za Kiraia kutoka Novemba, 2009
Somalia: Kuufahamisha mtandao wa waandishi na wanablogu wa Kisomali
Kituo cha habari cha Somalia ni jukwaa la waandishi na wanablogu wa Kisomali wanaoishi ndani na nje ya Somalia. Kituo kinasambaza machapicho ya habari na kuchapisha blogu zilizoandikwa na waandishi wa habari.
Afrika Kusini: Kikaragosi Kiliochoathirika na VVU Kwenye Kipindi cha Sesame Chaelimisha Kuhusu Ukimwi
Wakati kipindi cha watoto cha Mtaa wa Sesame (Sesame Street) kikisherehekea maadhimisho ya miaka 40 mwezi huu, kwa kizindua msimu wake mpya leo, kikaragosi kizuri kinachovutia cha Muppet katika toleo la Afrika Kusini kinaendelea kusaidia kupambana na kuelimisha kuhusu VVU/UKIMWI.
Azerbaijan: Baada ya Hukumu ya Wanablogu wa Video
Siku chache baada ya hukumu ya vijana wanaharakati wawili wa blogu za video huko Azerbaijan, wanablogu wengine wanaanza kuongea kwa sauti juu ya kifungo cha Adnan Hajizade na Emin Milli....
Paraguay: Wenyeji Wanyunyiziwa Dawa za Kuua Wadudu kwa Ndege
Huko Mashariki mwa Paraguay, jumla ya watu 217 wa jumuiya ya wenyeji ya Ava Guaraní walianza kusumbuliwa wakionyesha dalili mbalimbali za kiafya zinazoaminika zilisababishwa na unyunyiziaji wa makusudi wa dawa za kuua wadudu hasa baada ya wao kuwa wamegoma kuhama kutoka katika ardhi waliyoirithi kutoka kwa mababu zao.
Marekani: Mauaji ya Fort Hood Yasababisha Kumulikwa kwa Waislamu Walio Jeshini
Shambulizi la upigaji risasi la kushtukiza lililofanywa na mwanajeshi wa Jeshi la Marekani, Meja Nidal Malik Hassan, na kusababisha vifo vya watu 13 na kujeruhi wengine 31 katika kambi ya kijeshi ya Fort Hood, jimbo la Texas, kwa mara nyingine limesababisha Waislamu nchini Marekani kumulikwa - hasa wale wanolitumikia jeshi.
Philippines: Mti wa Dita Waokoa Maisha ya Watu 36 Wakati wa Mafuriko
Mti wa aina ya Dita huko Manila mjini uligeuka kuwa "Mti wa Uzima" wakati ulipotumika kama kimbilio na wakazi ambao walitegwa kwenye nyumba zao wakati wa janga la kimbunga na mafuriko ya hivi karibuni. Somo: Usikate miti.
Venezuela: Kukutana na kazi za msanii Jesus Soto
Kazi za msanii wa Kivenezuela Marehemu Jesus Soto zinapaswa kuguswa na kujizamisha ndani yake ili kuzielewa. Wachache waliwahi kutembelea kazi zake kwenye makumbusho wameandika uzoefu wao.
Cameroon: Wezi “wakarimu” na Malipo kwa Kutumia Salio la Simu
Karibu wakazi milioni 20 wa Cameroon wanakabiliwa na kiwango kinachoongezeka cha unyang’anyi. Majambazi wameweza hata kuyavamia makao makuu ya taifa ya polisi na Wizara ya Mambo ya Nje katika mji mkuu wa Yaounde.
Video: Dunia Yaadhimisha Kuanguka kwa Ukuta wa Berlini
Leo ni Kumbukumbu ya 20 ya kuanguka kwa Ukuta wa Berlini, kizingiti madhubuti cha kiusalama ambacho kiliwahi kuligawa jiji la Berlini katika pande mbili za Mashariki na Magharibi huko Ujerumani. Leo tunaonyesha baadhi ya picha za video zinazotoka pande mbalimbali za dunia zinazopandishwa ili kusherehekea siku hii na nini ukuta huo ulimaanisha siyo Ujerumani tu bali duniani kote.
Ofisa Aweka Wazi Ufisadi wa Polisi kupitia Mtandao
Mnamo tarehe 6 Novemba, afisa wa polisi katika Idara ya Mambo ya Ndani huko Novorossiysk alitumia tovuti yake binafsi kuwasiliana na Waziri Mkuu Vladimir Putin na kuzungumzia matatizo lukuki yanayowakabili maafisa wa polisi nchini Urusi.