Azerbaijan: Baada ya Hukumu ya Wanablogu wa Video


Siku chache baada ya hukumu ya vijana wanaharakati wawili wa blogu za video huko Azerbaijan, wanablogu wengine wanaanza kuongea kwa sauti juu ya kifungo cha Adnan Hajizade na Emin Milli. Wanaharakati hawa wa mtandaoni watatumikia vifungo vya miaka miwili na mwingine miaka miwili na nusu gerezani baada ya mashitaka ambayo wengi wanayaona kama yenye nguvu za kisiasa na ni katika kujaribu kuwanyamazisha wasemaji kwenye nchi hiyo.

Wanaungana na wengine kama Urais wa Jumuiya ya Ulaya, Baraza la Bunge la Ulaya, Shirika la Usalama na Ushirika la Ulaya, Shirika la kupingania Haki za Binadamu la Human Rights Watch, Amnesty International na Waandishi wasio na mipaka na wengine wengi wanaoishutumu hukumu hiyo.

Shirika la Amnesty International vilevile limewatangaza vijana hao wawili kama wafungwa wa dhamira. Interesing times, “mradi wa mtandaoni unaofuatilia jitihada za kudhibiti na kuzuia upatikanaji huru wa mtandao duniani kote,” waliyaweka mashtaka katika muktadha.

matumizi ya mabavu ya hivi karibuni yaliyoonyeshwa na nguvu za dola nchini Azerbaijan hayaachi shaka yoyote kwamba wote, waandishi na wanablogu wanatumia haki yao ya kujieleza kwa uhuru ilhali wanajua hatari inayowakabili.

[…]

Shukrani kwa shinikizo la kimataifa kama vile barua ya WPFC na nyingine nyingi, serikali ya Azeri imelazimishwa kuwatoa waandishi hao gerezani.

Lakini kitendo hiki cha hivi karibuni cha uonevu dhidi ya wanablogu wawili hakiachi tena wasiwasi kwamba, kama wakiachwa wenyewe, maafisa wa serikali wa Azerbaijan wataendelea na njia zao za kinyanyasaji.

Notes from Abroad naye pia hashangazwi na hukumu hiyo:

Jumanne, wanablogu wawili vijana walihukumiwa kifungo jela –mmoja kwa miaka miwili na nusu, na mwingine kwa maika miwili– kwa mashitaka ya kipuuzi ya uhuni. Suala zima ni aibu –likiendeshwa na malengo ya kisiasa, lakini haishangazi.

[…]

Kwa kuwa Azerbaijan ni utawala wenye utajiri mkubwa wa mafuta, nchi za Magharibi zimekuwa makini mno katika majibu yake kwa kitendo hiki kisichokuwa cha kidemokrasia kilichofanywa na serikali ya Azeri.

Serikali ya Azeri ni lazima ikemewe kwa nguvu zote na nchi zote za demokrasia duniani kwamba tabia ya aina hii hikubaliki.

Mwanablogu The Blogar, hata hivyo, anakaribia kukosa maneno:

Kwa hiyo hukumu imetolewa.
Emin na Adnan sasa ni rasmi kwamba ni ‘wahuni’.
Ninakosa cha kusema hapa.
Kama inavosemekana kuwa vyombo vya habari vya jamii vilihusika katika kuwatia ndani, vilihusika na kueneza habari mitaani kuhusu uvunjifu wa haki lakini havikuweza kubadili akili za mfumo wa sheria uliooza wa Azerbaijan.
Usicheze na Ilham.

[…] Mawazo yangu yako na fanilia zao pamoja na wao wenyewe.

Hata hivyo, kukiwa na rufaa inayokaribia kukatwa na uwezekano wa hatua zitakazochukuliwa na Mahamakama ya Haki za Binadamu ya Ulaya, L4L, blogu mpya ya lugha ya Kiingereza ya Azeri, inasema kwamba huu ni mwanzo tu:

Nini cha kufanya baada ya hapa? Awali ya yote tusikome. Tuendelee kufanya kazi kuelekea uhuru wa marafiki zetu na kuelekea kwenye uhuru wa raia wote wa Azerbaijan […] Adnan na Emin hawakuonyesha woga na sisi hatupaswi kuwa chochote chini ya majasiri na wenye kutia moyo.

[…]

Huu hauwezi kuwa mwisho. Vyote vinaanza sasa.


Parvana Persiani na David Sasaki wa Jukwaa la Dunia la kublogu la Global Voices on lin, Bucharest, Romania © Onnik Krikorian / Oneworld Multimedia 2009

Wakati huo huo, kwenye pembe za Kongamano la Dunia la Kublogu mjini Bucharest, Romania, Global Voices Online ilifanya mahojiano yaliyoshindikana na Parvana Persiani, Mjumbe wa Heshima wa Bodi ya OL! Vuguvugu la vijana wa Azerbaijani ambalo rafiki yake wa kiume, Adnan Hajizade aliyefungwa sasa, ni mshiriki mwanzilishi.

Habari mpya zitakuwa zilitundikwa kila zikipatikana. Wakati huo huo, habari kamili ya kukamatwa, mashitaka na kufungwa kwa Adnan Hajizade na Emin Milli zinapatikana kwenye sehemu ya Azerbaijan ya Global Voices Online na kwenye blogu ya OL! (Kwa Kiingereza na Kiazeri). Alama ya #EminAdnan pia inatumika kwenye Twitter.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.