Waandamanaji wa Amani Kutoka Helmand Wanatarajia Kubadilisha Historia ya Afghanistan

Picha ya maandamano ya amani iliyochukuliwa kutoka kwenye tovuti ya chombo cha habari cha Etilaatroz na kutumiwa kwa ruhusa.

Mwaka 2017 katika Afghanistan, jumla ya watu 10,453 walilipotiwa kuathiriwa na bomu la kujitoa mhanga — 3,438 walifariki na 7,015 walijeruhiwa. Ukiacha wakazi wa mji mkuu, Kabul, ni wakazi wa jimbo la kusini la Helmand ambao walikuwa na hali mbaya zaidi.

Kikundi cha matembezi ya amani cha Helmand kinaongozwa na vijana kutoka katika jimbo la Helmand kinaeleza hadithi ya kazi ya kuchosha ya vita na mwangaza wa maisha mazuri unaotafutwa kwa kizazi kijacho katika nchi iliyosambaratika kwa vurugu.

Matembezi yamefika Kabul baada ya kutembea kilometa 700 kupitia majimbo manne hatarishi sana nchini Afghanistan ambayo ni –Helmand, Zabul, Ghazni na Maidan Wardak. Njiani waandamanaji walifanya mikutano na wanakijiji na kuwaeleza madhumuni ya matembezi yao. Walianza wakiwa watu 7 lakini waliungwa mkono na watu 59 wengine wakiwa katika safari yao.

Waandamanaji wa amani wakiwasili. Walitembea kutoka Helmand kuelekea Kabul kutafuta amani na usalama wa nchi yao ya asili. Wapendwa hawa ni wakukaribishwa na kusifiwa. Lengo, uaminifu na juhudi yao ni vya ajabu. Ninatumaini sauti yao itasikika na watapata matokeo yanayohitajika.

Helmand ni jimbo la kimkakati kwa serikali na Watalibani. Mara nyingi inafikiriwa kuwa wakazi wa Helmand wanaishi na waasi wanaotawala eneo kubwa la Helmand zaidi ya serikali.

Matembezi yalilenga kuondoa dhana hiyo.

Kikundi hiki cha watu kutoka vijijini kilizidi kukua kipindi wataliban walipokuwa wakipiga mabomu katika Helmand mwezi Machi na kuua watu 15 na wengine kujeruhiwa.

Kwanza, wanaoishi katika mahema waliwekwa Helmand na majimbo mengine ya : Herat, Nimruz, Farah, Zabul, Kandahar, Uruzgan, Ghazni, Paktia, Kunduz, Kunar, Nangrahar, Balkh, Parwan, Daykundi, Maidan Wardak, Bamyan na and Jawzjan. Na baadaye njaa ikawapiga.

Matembezi kutoka jimbo la Helmand kuelekea kabul yalikuwa na maombi makuu manne :

  1. Kuheshimu mwezi mtukufu w a Ramadhani, pande zote zinazohusika katika vita lazima zisimamishe vita. (Mwezi wa ramadhani umemalizika wiki iliyopita lakini pamoja na kustisha vita, wataliban wameanza kuvamia maeneo ambayo serikali inayatawala);
  2. vituo maalumu na anuani kwa ajili ya mazungumzo ya amani inabidi yaainishwe kwa pande zote zinazohusika katika vita, na mazungumzo ya amani yanapaswa kuanzishwa;
  3. Kuhusu maadili na maslahi ya kiislam na ya taifa, hatua za makusudi za kuunda mfumo unaokubalika na pande zote lazima zichukuliwe;
  4. Muda maalumu wa makubaliano kwa pande zote zilipo katika vita lazima upangwe ili majeshi ya kimataifa kutoka Afghanistan yaweze kuondoka.

Kuelekea Kabul waandamanaji wamekuwa wakipokelewa na watu kwa furaha sana. Watu wengine wamekuwa wakiwapokea kwa maua na nyimbo za amani.

Tarehe 30 mwezi Mei 2018, Matembezi ya amani kuelekea Kabul yameongelewa sana katika mitandao ya kijamii na wanaume, wanawake, vijana wa kiume na kike wa makabila yote

Hazara wasichana jimbo la Ghazni wakiwa wamesimama kwenye mstari kukaribisha wavulana wa jimbo la Helmand ambao wamenzisha matembezi ya karibu km 600 wakiomba amani. Ujumbe mahsusi ni “vita na vurugu hazijui ukabila” Kila mmoja ni mhanga wa katika Afghanistan

Terehe 8 Juni 2018, Mji wa Kabul unasubiri kuwa mwenyeji wa matembezi ya amani ya Helmand ArtLordsWorld ananakshi maeneo mfululizo kwa picha mbalmbali kwenye barabara kuu inayoelekea Kabul kwa ukaribisho mashujaa wa amani matembezi ya amani ya Helmand kuelekea Kabul

Tarehe 4 mwezi Juni 2018, matembezi ya amani ya Helmand sasa yapo Kabul. Mama na mimi tulienda kuwasalimia. Walikuwa mbele ya jengo la Msikiti na madrasa wakiangalia shule ya Habibia. Kuwaona ilikuwa wakati wa furaha na uponyaji kwangu na kwa mama. Acha tuwakaribishe Kabul kwa upendo na kuwaunga mkono

Tarehe 19 mwezi Juni waandamanaji walikutana na Rais Ashraf Ghani , sio katika Ikulu ya rais ya kifari iliyoko Kabul kama maafisa walivyokuwa wameeleza bali mtaani, mahali ambapo matembezi yao yalianzia. Waandamanaji wamesema, wataliban wamekataa kukutana nao rasmi hadharani ingawa wamekutana na kuongea njiani na wapiganaji wa kikundi hicho,.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.