Habari kutoka 23 Novemba 2009
Afrika: Haki za Wanawake
Sokari anaandika kuhusu Toleo Maalum la Masuala ya Wanawake la Pambazuka linaloangalia miaka 15 iliyopita tangu mkutano au Jukwaa la Vitendo mjini Beijing pamoja na mustakabali wa haki za wanawake...
Brazil: Mtazamo wa Wakazi wa Vitongoji Maskini
Katika makala hii, tunasikia mitazamo ya wanahabari raia kutoka mradi wa Viva Favela kuhusiana ya vurugu inayotokana na mihadarati huko Rio de Janeiro na jinsi inavyofagia makazi ya walalahoi, kama wanavyoiona mbele ya milango ya nyumba zao.
Afrika Kusini: Kikaragosi Kiliochoathirika na VVU Kwenye Kipindi cha Sesame Chaelimisha Kuhusu Ukimwi
Wakati kipindi cha watoto cha Mtaa wa Sesame (Sesame Street) kikisherehekea maadhimisho ya miaka 40 mwezi huu, kwa kizindua msimu wake mpya leo, kikaragosi kizuri kinachovutia cha Muppet katika toleo la Afrika Kusini kinaendelea kusaidia kupambana na kuelimisha kuhusu VVU/UKIMWI.
Azerbaijan: Baada ya Hukumu ya Wanablogu wa Video
Siku chache baada ya hukumu ya vijana wanaharakati wawili wa blogu za video huko Azerbaijan, wanablogu wengine wanaanza kuongea kwa sauti juu ya kifungo cha Adnan Hajizade na Emin Milli....