Habari Kuu kuhusu Wasifu wa Wanablogu
Habari kuhusu Wasifu wa Wanablogu
‘Mwanablogu Mzuri Lazima Awe na Sifa za Asili za Waandishi Wazuri wa Habari’
Dorothée Danedjo Fouba, mshindi wa tuzo ya “Blogu Bora ya Teknolojia Afrika, iliyotolewa Tuzo za Uandishi wa Kiraia za Telkom-Highway Africa 2013“, alizungumza na Dibussi Tande (@dibussi) kuhusu maendeleo yake katika tasnia hii, na sifa zinazohitajika ili kufanikiwa.
Madagascar: Global Voices katika Kimalagasi Yapiga Hatua Kubwa
Mradi wa Lingua wa Global Voices katika lugha ya ki-Malagasi umechapisha mtandaoni posti yake ya 5,000. Mradi huo ulianza mwezi Septemba 12, 2007 ukiwa kati ya miradi ya mwanzo kabisa ya Mradi mkubwa wa Lugha za Kiafrika. Kwa sasa mradi huo unaendeshwa na watafsiri wa ki-Malagasi wapatao 16 miongoni mwao...
Wapiga picha wa Kiafrika, waandishi na wasanii wapata sauti zao kwenye blogu
Kadri Waafrika wengi wanavyozidi kugundua nguvu ya kublogu kama zana ya kutoa maoni kwa kiwango cha dunia nzima, tarakimu ya wanablogu imeongezeka na pia maudhui yanayopewa kipaumbele. Kwa tarakimu hiyo ya kukua kwa blogu, wasanii wengi wa Kiafrika wamejiunga, na ongezeko kubwa likionekana kwenye blogu za mashairi kama ilivyo kwa upigaji picha unaochipukia na blogu za sanaa za maonyesho. Tunazipitia baadhi.
Kutambulisha Sauti Zinazotishwa
Leo, kitengo cha utetezi cha Global Voices, kinazindua tovuti mpya inayoitwa Threatened Voices, yaani, Sauti Zinazotishwa ili kusaidia kufuatilia unyamazishaji wa uhuru wa kujieleza wa mtandaoni. Inaonyesha ramani ya dunia na mwingiliano wa saa unaosaidia kuonyesha taarifa za vitisho na ukamataji unaofanywa dhidi ya wanablogu duniani kote, na ni mhimili mkuu wa kukusanyia taarifa kutoka katika asasi na wanaharakati walioamua kujitoa muhanga kwelikweli.
Blogu za Afrika Zapendekezwa Kupokea Tuzo ya Bloggies 2009
Blogu zilizopendekezwa kwa ajili ya Tuzo ya Tisa ya Zawadi za Weblog: Mapendekezo ya blogu katika mashindano ya Bloggies ya 2009 yalifunguliwa tarehe 1 Januari na kufungwa tarehe 19 Januari. Kwa mujibu wa waandalizi, mashindano hayo ya Bloggies ni mashindano ambayo yamedumu kwa muda mrefu zaidi mtandaoni, na mapendekezo pamoja na uchaguaji wa washindani katika fainali, ni juu ya msomaji wa blogu. Mshindi hupata senti 2,009 za Marekani! Je, ni mabloga gani wa Kiafrika waliopendekezwa kwa ajili ya kinyang'anyiro cha blogu bora zaidi?