Blogu zilizopendekezwa kwa ajili ya Mashindano ya Tisa ya Zawadi za Weblog: Mapendekezo ya blogu katika mashindano ya Bloggies ya 2009 yalifunguliwa tarehe 1 Januari na kufungwa tarehe 19 Januari. Kwa mujibu wa tovuti ya waandalizi, mashindano hayo ya Bloggies ni mashindano ambayo yamedumu kwa muda mrefu zaidi mtandaoni, na mapendekezo, pamoja na uchaguaji wa washindani katika fainali, ni juu ya msomaji wa blogu. Mshindi hupata senti 2,009 za Marekani!
Blogu tano zimependekezwa katika kinyang'anyiro cha blogu Bora Zaidi:
Blogu ya Being Brazen: Hii ni blogu iliyoko Afrika ya Kusini. Wasifu wa mwanablogu huyo unaelezwa:
Sitabiriki, huota ndoto za mchana, umri wangu ni katika miaka ya 20, ninaamini katika mapenzi, Mungu na nguvu ya maneno, nina mawazo huru na pengine kucheka ndio dawa bora kuliko zote. Sipendi kuruka angani [kupanda ndege], sehemu zenye watu wengi, kupanga foleni, kadhalika sipendi wadudu. Hujikwaa nikavaa viatu virefu. Ninaandika ili kuepuka wehu.
Blogu ya AppAfrica: Hii ni tovuti ya habari mpya mpya zinazohusu ubunifu wa Kiafrika, elimu na ujasiriamali kwenye teknolojia:
Blogu ya Glad To Be A Girl: Ni mwanablogu wa Kiafrika ya Kusini anayekaa mjini Johannesburg.
Huchambua wehu wangu na hujisifu kwa akili zangu! Unyonge [kutopenda makuu] unanichirizika ndoo kwa ndoo :) kejeli ndiyo silaha yangu ninayoipenda. Wakristu, Waislamu & Wayahudi wanaamini katika Mungu mmoja zaidi ya yule ninayemuamini.
Blogu ya West Africa Wins Always: Hii ni blogu ya mwanablogu Pauline, mwanahabari ambaye amekuwa akiishi nchini Ivory Coast tangu mwaka 2003.
Na blogu ya mwisho ni ile ya Scarlett Lion: Yeye ni mwanahabari aliyeko nchini Liberia.
Kwa mujibu wa maneno yake mwenyewe:
Mpiga picha, mwandishi, ripota. Napita maishani nikiwa na jicho linalolenga kutengeneza historia na kuiorodhesha. Awali katika nchi ya Uganda na sasa katika Liberia. Blogu hii inakuletea udadisi na maoni. Pamoja na picha.
Upigaji kura utafungwa tarehe 2 Februari na washindi watatangazwa mwezi Machi mjini Austin, Texas, huko Marekani katika Tamasha la South by South West Interactive.