Habari kuhusu Uandishi wa Habari za Kiraia kutoka Novemba, 2015
GV Face: Kuhusu Beirut na Paris, Kwa nini Majanga Mengine Yanatangazwa Zaidi Kuliko Mengine?
Katika toleo la wiki hii la mazungumzo ya GV, tutajadili rangi, siasa za vifo na miitikio isiyo na usawa yanapotokea majanga duniani kote.
Global Voices Yashikamana na Watetezi wa Uhuru wa Kujieleza nchini Morocco
Jamii ya Global Voices yataka kutendeka kwa haki dhidi ya watetezi saba wa uhuru wa kujieleza wanaoshitakiwa nchini Morocco kwa makosa ya “kuhatarisha usalama wa ndani wa Taifa.”
Mitaa ya Paris Inavyonikumbusha Mitaa ya Beirut
"Hatujapata kitufe cha 'salama' kwenye mtandao wa Facebook. Hatujapata salamu za pole usiku wa manane kutoka kwa watu maarufu zaidi duniani pamoja na mamilioni ya watumiaji wa mtandao..."
Jamii ya Lumad Nchini Ufilipino Yasimama Kidete dhidi ya Uonevu
“Jeshi la Ufilipino liliharibu shule yetu. Pia, lilichoma majengo ya ushirika wetu wa kilimo. Nilijikuta nimefungwa gerezani na sasa nimeshitakiwa kwa kusingiziwa kosa la utekaji. Tuna hamu ya kuipata tena ardhi yetu tuliyoirithi kutoka kwa mababu zetu."
Sassou-Nguesso Aungana na Marais Wengine wa Maisha Barani Afrika
Vijana wa Kongo (Brazaville) wanapinga jaribio la Rais Sassou-Nguesso kugombea kwa awamu nyingine
Muziki Wamsaidia Mwanamke wa Ki-Hindi Kujikwamua Kiuchumi
Tritha Sinah anaongoza bendi iitwayo Tritha Electric. Amekulia Kolkata na anasema muziki umekuwa njia ya kujipatia uhuru wa kifedha.
Michoro Yaonesha Harakati za Raia wa Ufilipino Wakipambana na Ukandamizaji
Nchi ya Ufilipino ina idadi ya raia wazawa wanaokadiriwa kufikia milioni 14. Wengi wa raia hawa wanaoishi maeneo ya vijijini wapo katika hatari kubwa ya kuathiriwa na uharibifu unaotokana na shughuli za uchimbaji madini, harakati za utafutaji maendeleo pamoja na matumizi ya nguvu za kijeshi.
Irani Yaanza Kutoa Huduma ya Bima ya Afya kwa Wakimbizi
Wakimbizi wanaotoka Afghanistani nchini Irani inakaribia kuwa milioni 1, wakati inakadiriwa kuwa wakimbizi wasioandikishwa ni kati ya milioni 1.4 na 2 wanaoishi na kufanya kaz nchini humo.
Wanablogu wa Zone9 Wasema, ‘Kushikiliwa kwetu Kumefunua Yaliyojificha Nchi Ethiopia’
"Kwa wale waliotufunga gerezani na ambao walitusababishia madhila haya, hata kama hautuombi msamaha, sisi hatuna kinyongo."
Mwanafunzi wa Irani ‘Awekwa Ndani’ kwa Sababu ya Anayoyaandika Facebook
"Maafisa wa mahakama ...wasiwakamate vijana na kuwapa hukumu kubwa kila wanapokosoa. Kijana wangu alitakiwa awe darasani anasoma hivi sasa."