Habari kuhusu Uandishi wa Habari za Kiraia kutoka Juni, 2009
Honduras: Zelaya Akamatwa na Kuondolewa Madarakani
Nchini Honduras siku ilianza na habari zinazosema kwamba Rais Mel Zelaya amekamatwa akiwa nyumbani kwake na wanajeshi wenye silaha mnamo siku ya kupigwa kura tata ya maoni. Siku chache kabla, Zelaya alimuondoa madarakani mkuu wa majeshi. Maoni yanatofautiana kutokea yale yanayosema kwamba hali iliyopo ni sawa na mapinduzi ya kijeshi mpaka yale yanayosema kuwa hii ilikuwa ndio njia pekee ya kukomesha jitihada za Zelaya za kutaka kugombea urais kwa awamu nyingine tena.
Togo Yafuta Adhabu ya Kifo
Bunge la Taifa la Togo limepiga kura ya kukomesha adhabu ya kifo na kuifanya nchi hiyo kuwa mwanachama wa 15 wa Umoja wa Nchi za Afrika kuipiga marufuku adhabu hiyo.
Uchaguzi Wa Irani Katika Picha
Uchaguzi wa rais nchini Irani utafanyika tarehe 12 Juni. Ni watu wanne tu kati ya watu zaidi ya 400 waliojiandikisha ambao wamepewa idhini rasmi na Baraza la Walezi kuwa wagombea katika uchaguzi. Macho makali ya wanablogu-wapiga picha yamenasa nyakati na taswira katika mitaa ya Irani ambako watu walikuwa wakiwapigia debe wagombea wanaowapenda.
Malawi: Wasikilize wanablogu wa uchaguzi Malawi
Wamalawi wanapiga kura katika uchaguzi wa Raisi na Bunge. Baadhi ya wanablogu walipatiwa mafunzo na PenPlus Bytes, Taasisi ya kimataifa ya Uandishi wa TEKNOHAMA kwa ushirikiano na New Media Insitute kwa lengo la kuangalia na kutoa maoni yao kuhusu uchaguzi huo kwa kutumia blogu, teknolojia ya twita na simu za viganjani. Hebu na tuziangalie blogu zao, ambazo zimehifadhiwa katika Potal ya chaguzi za Afrika. Poto hii hutoa taarifa za kutosha kuhusu chaguzi mbalimbali katika nchi za kiafrika.
Uganda: Mke wa Rais ateuliwa kwenye Baraza la Mawaziri
Mabadiliko ya hivi karibuni katika Baraza la Mawaziri limewafanya wanablogu wa Uganda kuanza kubashiri matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2011. Moja ya uteuzi aliofanya Rais Yoweri Museveni ni ule wa kumteua mke wake, Janet, kuwa Waziri wa Nchi wa Karamoja. Eneo hili liko kaskazini-mashariki mwa Uganda na kwa miongo mingi limegubikwa na migogoro na umaskini uliokithiri.